Zainab j
JF-Expert Member
- Sep 24, 2018
- 1,817
- 2,362
Uzuri Rais au serikali ishawajua watanzania wengi Wana ugonjwa wa akili, kwahiyo Wala usidhani Kama wanawafuatilia hizo kelele zao,Kiprotokali, Kiusalama na kwa Tukio husika la Kiongozi wa Nchi GENTAMYCINE sijaona tatizo lolote lile la Rais Samia (Muislamu) kuingia Kanisani (Ibadani) pamoja na Kiti (Viti) akiwa na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango katika Nyerere Day ya Jana huko kwa Watani zangu Wapendwa Wahaya Mkoani Kagera (Bukoba)
Ni kweli huyu Mama (Rais) huwa tunamkosoa sana (nami nikiwemo) tukiwa na Lengo la Kumjenga kwakuwa tunampenda ila naanza kuona Sasa kuwa Watanzania tunaanza Kumuonea na kuwa na Nongwa zetu za ama Kiimani (Dini) na Wivu wetu.
Hivi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Hayati Rais Mstaafu Mkapa na Hayati Rais Dk. Magufuli tena Wote wakiwa ni Wakristo Wakatoliki Wenzangu walikuwa hawaingii Misikitini?
Mbona Hayati Rais Dk. Magufuli alikuwa hadi anaingia Misikitini na 'Mamitambo' mengi ya Kiusalama kutoka kwa Watendaji wake na mlikuwa hamsemi chochote na iweje leo iwe Nongwa kwa Rais Samia kufanya hivyo Kanisani?
GENTAMYCINE ni Mtu wa Haki na Ukweli halafu sipendi Unafiki au kuona Mtu asiye na Kosa ama anaonewa au anasakamwa kwa mambo ya Kipumbavu (Kijuha) kutoka kwa Wapuuzi.
Mwacheni Mama (Rais Samia) afanye Kazi na kama ni Kumkosoa basi kuwe ni kwa Tija ili Kumjenga na Kumsaidia na siyo Kumsakama na Kumuonea tu kwa kila Kitu akifanyacho.
Kwako Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan tafadhali nakuomba tuzoee tu Sisi (Miswahili) kwani hatuna Jema wala Shukran hivyo Wewe endelea tu kuchapa Kazi na tambua ya kuwa Wanao Tukuka akina GENTAMYCINE tuko nyuma yako na tunakukubali na hata ukiniona nakupiga Dongo jua nataka tu Kukusahihisha mahala ila sikuchukii kabisa hata Malaika wa Mbinguni wanajua.
Macho na Masikio yote tu ni Sudan!!!
Walishupalia suala la Tozoo, sasaivi washalisahau wamerukia ishu ya Masanja na mkewe, na tayari wanajifanya wao Wana DNA za macho tu kujua baba halisi wa kila mtoto,
Sasa mkuu GENTAMYCINE hao watu utasema wazima kichwani?