Imekaaje Rais Samia kwenda na kiti chake kwenye ibada leo tarehe 14.10.2022 mkoani Kagera?

Imekaaje Rais Samia kwenda na kiti chake kwenye ibada leo tarehe 14.10.2022 mkoani Kagera?

Kwa hili nakushauri tena soma unachotetea Vs Wanachokosoa kama vinaendana. Kiti cha Rais ni mamlaka, na Kanisa ni mamlaka pia. Kupeleka kiti cha Urais kanisani ni kama kupqmbanisha mamlaka. Unapoingia kwenye nyumba ya ibada unakuwa chini ya mamlaka ya Kanisa. Ndo maana ratiba inayofuatwa humo ni ya Kanisa na siyo ya Serikali. Mimi Huwa sifutilii vitu vidogo, lakini kwangu Jambo la kiimani ni kubwa Sana. Sijawahi kumuona Kikwete kaingia msikitini akaomba Mswala wake toka Ikulu. Hata Samia ameenda msikitini akiwa anakaa kwenye Mswala wa msikiti husika. Tuwashauri viongozi wetu unyenyekevu kwenye masuala ya kiimani na hasa unapoona jnahudhuria Imani isiyo yako unatakiwa kuwa makini Sana.
Umeiona picha ya Hichilema na ya Baideni wakiwa kanisani? Hawakupungukiwa chochote kukalia mabenchi Kwa Muda mfupi kuonyesha usawa wa kibinadamu mbele Mungu.
Taratibu tutaanza kuona Waziri Mkuu akienda kumsalimia Mbunge mgonjwa hospitali kinabebwa kiti cha Ikulu.
Thread closed by Tate Mkuu at 12:41 pm.
 
Mkuu, mimi nitakuuliza, jana Samia aliingia kanisani kama muumini wa dhehebu au kama Rais wa JMT?

Umetoa mfano wa Magufuli kwenda kanisani, Magufuli alikuwa anaenda kanisani kama Rais wa kama muumini wa kawaida?
Yaani ni hivi; Kanisa Katoliki lina taratibu zake. Hata kama wewe siyo muumini wake, unaruhusiwa kuingia! Isipokuwa ni lazima ufuaye baadhi ya masharti.

Mojawapo ni hilo la kuwekewa sehemu yako ya kukaa, kwa utaratibu wao! Na siyo kwa utaratibu wako! Ndiyo maana nimekumbusha tukio la jana liliwahi kutokea huko nyuma!


Kilichofuata ilikuwa ni kwa Rais wa wakati huo kuahirisha kuhudhuria sherehe aliyo alikwa na Kanisa, baada ya kuzuiliwa kistaarabu tu, kuingia na kiti chake maalum Kanisani.
 
Akikujibu ipasavyo naenda Kunya ( Kuukweka ) Mubashara ( Live ) kabisa MP 1 Lugalo Dar es Salaam au 92KJ Sanga Sanga Morogoro mchana huu kweupe.
Nimeshamjibu ipasavyo! Kama vipi uanze sasa hilo zoezi, haraka iwezekanavyo. Kuna vijana wangu wanakusubiri hapo Lugalo kwa hamu na shauku kubwa.
 
Mbona malalamiko yanazidi au mlikua mmemtegea mama samia mafuta ya mbuzi katoliki kwenye viti vyenu?
 
Kiprotokali, Kiusalama na kwa Tukio husika la Kiongozi wa Nchi GENTAMYCINE sijaona tatizo lolote lile la Rais Samia (Muislamu) kuingia Kanisani (Ibadani) pamoja na Kiti (Viti) akiwa na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango katika Nyerere Day ya Jana huko kwa Watani zangu Wapendwa Wahaya Mkoani Kagera (Bukoba)

Ni kweli huyu Mama (Rais) huwa tunamkosoa sana (nami nikiwemo) tukiwa na Lengo la Kumjenga kwakuwa tunampenda ila naanza kuona Sasa kuwa Watanzania tunaanza Kumuonea na kuwa na Nongwa zetu za ama Kiimani (Dini) na Wivu wetu.

Hivi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Hayati Rais Mstaafu Mkapa na Hayati Rais Dk. Magufuli tena Wote wakiwa ni Wakristo Wakatoliki Wenzangu walikuwa hawaingii Misikitini?

Mbona Hayati Rais Dk. Magufuli alikuwa hadi anaingia Misikitini na 'Mamitambo' mengi ya Kiusalama kutoka kwa Watendaji wake na mlikuwa hamsemi chochote na iweje leo iwe Nongwa kwa Rais Samia kufanya hivyo Kanisani?

GENTAMYCINE ni Mtu wa Haki na Ukweli halafu sipendi Unafiki au kuona Mtu asiye na Kosa ama anaonewa au anasakamwa kwa mambo ya Kipumbavu (Kijuha) kutoka kwa Wapuuzi.

Mwacheni Mama (Rais Samia) afanye Kazi na kama ni Kumkosoa basi kuwe ni kwa Tija ili Kumjenga na Kumsaidia na siyo Kumsakama na Kumuonea tu kwa kila Kitu akifanyacho.

Kwako Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan tafadhali nakuomba tuzoee tu Sisi (Miswahili) kwani hatuna Jema wala Shukran hivyo Wewe endelea tu kuchapa Kazi na tambua ya kuwa Wanao Tukuka akina GENTAMYCINE tuko nyuma yako na tunakukubali na hata ukiniona nakupiga Dongo jua nataka tu Kukusahihisha mahala ila sikuchukii kabisa hata Malaika wa Mbinguni wanajua.

Macho na Masikio yote tu ni Sudan!!!
We jamaa nakuona mtu wa mrengo wa kushoto tu lakin leo nimekueelewa sana bob!!

Ntaaanza kufikilisha kichwa changu juu ya post zako
 
Nilikuwa nasema haijalishi nyumba ya ibada au kijiji ,kitingoji, wilay ,mkoa na nchi kwa ujumla lazima utakuja taratibu fulani ukienda against lazima patazua mjadala ...ukileta utaratibu mpya hata kama hauna maana mbaya lazima utaleta mtafaruku haya ndo Yale ya wapemba pia kupinga ujenzi wa kanisa ..
So mnayo haki ya kupinga na kutetea kulingana na taratibu zenu.
 
Leo katika maadhimisho ya baba wa taifa hayati Julius Kambarage Nyerere amefanyiwa ibada na viongozi mbalimbali mkoani Kagera akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN.
Minongo'no mikubwa imekuja baada ya yeye kupewa kiti chake kwenye nyumba ya ibada. Hii naona kama nyumba ya ibada haiaminiki kwa kile kilichofanyika ka sababu ya usalaama wake? Au hii ni kawaida kwa kiongozi mkuu wa nchi.

Au kitendo kilichofanyika ni kawaida kwa mkuu wa nchi kupewa kiti chake?

Nimeuliza tu iliniweze kufahamu kama jambo hili ni la kawaida kwa wakuu wa nchi kuingia kwenye nyumba ya ibada na viti vyao.

View attachment 2387240
Hawaachiani maji mezani🤣😅😅JK
 
Ukicheza tu vibaya na madhabahu, iwe kwa maneno au kwa vitendo, hauchelewi kuwa "one term president"

Ni bora kutàfuta uwakilishi, kuliko kuonyesha wewe kuwa ni maarufu na mkuu katika nyumba hizi za ibada. Yule mwenye kujiinua nafsi yake hutezwa, na mwenye kijishusha nafsi yake mbele za Mungu huinuliwa.
Lakini hii si inatokana na nia iliyoko moyoni mwa Mhusika? Hana nia ya kujiinua.

Nakumbuka Siku Jpm alibishana na Padre pale St Peters nilishangaa sana.

Hizi Doctrine hata kama si za Mungu wa kweli lalini zina nguvu......devine powers
 
Leo katika maadhimisho ya baba wa taifa hayati Julius Kambarage Nyerere amefanyiwa ibada na viongozi mbalimbali mkoani Kagera akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN.
Minongo'no mikubwa imekuja baada ya yeye kupewa kiti chake kwenye nyumba ya ibada. Hii naona kama nyumba ya ibada haiaminiki kwa kile kilichofanyika ka sababu ya usalaama wake? Au hii ni kawaida kwa kiongozi mkuu wa nchi.

Au kitendo kilichofanyika ni kawaida kwa mkuu wa nchi kupewa kiti chake?

Nimeuliza tu iliniweze kufahamu kama jambo hili ni la kawaida kwa wakuu wa nchi kuingia kwenye nyumba ya ibada na viti vyao.

View attachment 2387240
Hiyo ni protocol ya nchi. Wewe ulitakaje?
 
Back
Top Bottom