Imekuwaje Ibrahim Ajib ana miaka 26 wakati alisoma darasa moja na mdogo wangu mwenye miaka 36

Imekuwaje Ibrahim Ajib ana miaka 26 wakati alisoma darasa moja na mdogo wangu mwenye miaka 36

mwengine huyu hapa
image-2023-01-17-12:31:36-800.jpg
 
[emoji1787][emoji1787] nimecheka Sana Kuna jamaa angu mmoja tumesoma high school darasa moja yupo ihefu nilishangaa kumuona team ya taifa under 20
Wanamichezo wengi nchini TANZANIA wanaosaini mikataba ya kazi wanadanganya umri.


Mjomba wangu alishadanganya umri sana, alikuwa na vyeti vya kuzaliwa takribani 20
 
Kuna umri wa kwenye michezo na umri halisi. Formula rahisi ya kujua umri wa mchezaji ni unachukua umri wake ongeza 7. Akisema ana miaka 25 basi jumlisha 7 utapata umri halisi au uliopishana kidogo. Football na riadha ndo mabingwa wa hii michezo ya umri. Kuna mwanariadha alikuwa na mke na watoto wawili ila akaiwakilisha nchi kwenye Junior championship ambao ni chini ya miaka 17
 
Be nice, kama hajakuchukulia nafasi yako muache yuko kwenye utafutaji, Labda kama ni mpinzani wako naweza kuelewa upande wako wa mtazamo. Bongo tunavyotafuta ugali magumashi ni mengi kweli kweli, Mtu anasoma may be hadi for 6 hapo ana 20 years tuseme.. Aje atafute timu ya kucheza atengeneze CV hadi aje kupata kilabu cha kuchezea professional anakua na miaka mingap? requirement zinatakaje na tunamlaumu vipi huyu kijana ambaye ameamua kudanganya umri ili angalau apate miaka 10 ya kukaa kwenye game?

Be nice, na kama nchi tufanyie kazi umri wa kukaa mashuleni na tujali umri wa vijana kuanza maisha. Nchi zingine mbona wana policy safeguarding haya mambo?
 
Back
Top Bottom