Imekuwaje magazeti yote ya leo kutumia picha moja?

Imekuwaje magazeti yote ya leo kutumia picha moja?

Labda imetoka ikulu au tibisiii

Ziara ni nyingi waandishi wametulia home wanasubiri kudukua
 
Siku hizi ktk kanisa katoliki tunasalimiana hivyo kama ishara ya kutakiana amani na heri, zamani kabla ya korona tulikua tunapeana mikono, baba askofu alimwinamia mh rais Samia kama ishara ya kumkaribisha nyumbani kwake na kumtakia amani awapo mahali pale, rais alitakiwa kujibu kwa kuinama pia kuonesha amepokea, nadhan sio utamaduni wake (mama) Wala wa dini yake, ndo maana alifunga mikono na bila shaka alitamka maneno fulani ya kuonesha ameitikia salamu, hapo hakuna kosa kutoka upande wowote ule, kila mtu alifanya kile kilichopo ktk mazingira yake, Imani yake na nafsini mwake, kufanya tofauti na unachokiamini ndio kosa. Asante mama kwa heshima uliyompa mzee kwa kuacha majukumu yako yote ya kitaifa na kimataifa ukaenda kijijini ngara kushiriki shughuli hiyo muhimu, hakika umemheshimisha sana mzee na umeliheshimisha kanisa katoliki, sasa panga na safari ukamsalimie baba mtakatifu Francis kama wenzako wote walivyofanya ukimwacha mtangulizi wako.,Asante sana Mama.
 
Hii siyo coincidence hata kidogo. Wengi wamechangia hapa lakini naona hawajagundua hili ni janga kubwa kwa nchi. Haya magazeti yote ina maana yanapokea amri kutoka sehemu moja na wahariri wake wote wanaweza kuwa ni watumishi wa kitengo!
Inaweza kuwa pia ni mapungufu ndani ya magazeti yenyewe . Hata hivyo kitaalum ya uandishi wa habari siyo dhambi ku share picha.
 
Naona Gay fulani la Raia Mwema limemshupalia Meya wa Moshi kwa habari za kutunga na kulazimisha. Anaenda kumsemea kwa viongozi wa dini kila kukicha ni front page news wakati huyo Meya hayo yote kafanya nje ya kazi kwenye maisha yake binafsi.
 
Wahariri siku hizi wanasifia kila kitu hakuna weledi tena.

Club ya wahariri wakikutana lao moja,wanakubaliana kuandika story moja ambayo itamfurahisha mtawala.

Fuatilia lile suala la Mbowe na wenzake kunyimwa chakula.

Magazeti yote yalikuja na story za kebehi “Mbowe alia njaa”.Unaweza kuona ni jinsi gani vyombo vyetu vya habari vilivyofilisika kiuwezo na kifikra.

Magazeti yetu yamekuwa hovyo kuliko kipindi chote cha uhai wa taifa hili.

Magazeti yetu hayawezi kuandika habari za Ngorongoro.
Habari za kero za muungano.
Habari za bunge dhaifu
Habari za wabunge 19
Habari za kina za kesi ya Mbowe
Habari kwanini uwekezaji wa ATCL
Habari za kina za ukopaji wa Serekali
Habari za kina za mgao wa fedha JMT/SMZ
Habari za Katiba mpya
Habari za chaguzi zetu
Habari za ukatikaji wa umeme
Habari upigaji fedha za umma

Ukisoma magazeti yetu au ukitazama TV zetu habari kubwa ni michezo na kusifu !.
 
Kajisa Katoliki tangu kuwepo kwa corona huwa hatushikani mikonobya amani, bali huinamiana hivyo. Amani kwako
 
Acha uongo

2,000
Magazeti karibu yote kwenye front page yameweka picha ikimuonesha askofu Niwemguzi akimuinamia SSH, je hii picha imetoka wapi na kusambazwa na nani.

Je ina uhusiano na kujilinganisha na Mungu?
Kama huyaoni hayo magazeti niliyoyaweka basi nadhani umetoka Mirembe, bado ujapona.
 
Hii siyo coincidence hata kidogo. Wengi wamechangia hapa lakini naona hawajagundua hili ni janga kubwa kwa nchi. Haya magazeti yote ina maana yanapokea amri kutoka sehemu moja na wahariri wake wote wanaweza kuwa ni watumishi wa kitengo!

Ipo hivi, hiyo ni kazi ya Maafisa Habari wa Ikulu kuhakikisha picha zitazotumika hazina ukakasi kuendana na hadhi ya Urais.

Wapiga picha wa Ikulu, wanapopiga hizo picha PRO's wanachagua na kuwatumia Wahariri! Actually, ni hali ya kawaida ulimwenguni japo ethics za uandishi haziruhusu hali hiyo. Lakini mediA zitafanyaje iwapo hiyo ndiyo burning issue na picha waliyopewa ndiyo hiyo?? Si kwamba wameigana ila ndizo walizopewa
 
Magazeti yetu ni hovyo tu. ''Waandishi'' wengi ni tia mchuzi kwangu pakavu!
 
Back
Top Bottom