Imepita miaka 7 toka tumeachana, jana kanitumia SMS ya kejeli

Imepita miaka 7 toka tumeachana, jana kanitumia SMS ya kejeli

Choosen85

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
1,143
Reaction score
2,475
Wakuu mulibwanji? Mambo huku ni tabulele laaa.... Nilipokuwa chuo nlikuwa kwenye mahusiano na mdada mmoja wa Kiha nlimpenda sana na tulifanikiwa kupata mtoto 1, kiukweli nlitamani ndo awe wife kumbe nilikuwa najiandalia bomu hasa alipotangulia kupata kazi.

Alikuwa kasomea ualimu, nilianza pewa maneno makali sana kama mwanaume suruali, shetani, ilifikia hatua naambiwa nanuka. Nilijipanga nikaamua kuondoka zangu nilimuachia kila ktu nlichopata nae. Mtoto alimkatalia akasema ili nimchukue nihakikshe nimemuua nikamwambia mtoto nimekupa sasa ni wako.

Lakini ajabu visa vikawa haviishi, alikuwa akinitumia sms za kunitukana sana na maneno mengine ya hovyohovyo, sikuwa namjbu zaidi ya kumpuuza. Alianza watafuta ndugu na marafiki zangu anawaambia tuhuma kibao kuhusu mimi hiyo ni baada ya kuwa nlishaondoka.

Nilishangaa sana kwanini bado ananifatilia wakati namuaga aliniambiaga sepa huko. Ajabu hata nilikuwa nikibadili namba atapambana ataipata na ataanza kunitumia ma sms ya matusi mpaka kunitukania wazazi wangu.

Sasa imepita miaka 7 toka nimeachana nae, nilishaoa na nina mtoto 1 tayari nikajua mwenzangu alishasahau na pengne ana bwana ake maana umepita muda sasa wala hata sijui chochote kuhusu maisha yake. Jana usiku saa tatu. Nashangaa inaingia sms ya kejeli kucheck namba nikagundua ni ile ya yule muha ex wng.

Nilishangaa sana huyu mtu mbona imepita miaka mingi sana bado ana mambo yaleyale ana matatzo gani. Kwa kweli hata sikumalizia soma sms ile nilifuta hata sikuijbu kbs. Wakuu mtu kama huyu ni nini kinamsumbua. Je ni hasira au bado ananipenda au ananichukia tu? Karibu kwa maoni yenu.
 
Kifuatacho atasnza kumsumbua na kumtukana mkeo ili akuharibie tu ndoa yako, usiulize namba ataipata wapi. Hizo ndio akili za wasaidizi wa kufanana na sisi Mungu aliotupa.

Yeye anapenda mkiachana usifanikiwe kitu chochote

Yeye anakuwa chakaramu lakini anaota mwanaume mpole, mcha Mungu
 
Kifuatacho atasnza kumsumbua na kumtukana mkeo ili akuharibie tu ndoa yako, usiulize namba ataipata wapi. Hizo ndio akili za wasaidizi wa kufanana na sisi Mungu aliotupa.

Yeye anapenda mkiachana usifanikiwe kitu chochote

Yeye anakuwa chakaramu lakini anaota mwanaume mpole, mcha Mungu
hilo nimelijua muda sn nliamua namba ya wife watu wa ukaribu nao upande wng ndugu jamaa marafk wasiwe nayo kbs hlo nimelishnda hawez ipata hata yng kuna hatua nataka chukua kuanzia sasa. Hakika tulipewa wasaidz wa ambao wamekuja kushrikiana na shetan kutumaliza wanaume.
 
Huyo mwanamke alianza kukutukana baada ya kupata bwana mpya na kama ilivyo kawaida ya kanuni ya karma na sasa bwana wake amemuacha na hana pakujifariji kabisa na kitendo chako cha kutokumjibu ndio kinamfanya awe chizi…
Kamwe usimjibu lakini hakikisha umemwambia kila kitu huyo mkeo mpya…hakikisha umemwambia kila jambo maana kinachofata ni kumtukana mkeo…..!

Ila nimehisi harufu ya wewe bado kumpenda huyo mwanamke…usininukuu vibaya lakini nimehisi bado unampenda….kama hayo ndio kweli yanakusumbua kutoka kwake hakika nasihisi harufu ya upendo kati yenu nasiku si nyingi usipotafuta njia ya kumpotezea mazima hakika hiyo ndoa yako mpya ya miaka saba itakuwa historia!

Kamwe ,Kamwe,Kamwe,Kamwe usimrudie mwanamke aliyekuacha au aliyekusaliti maana utajuta maisha yako yote!

Yani zamani tulijenga sana imani kwa Walimu lakini sasa nao wamekuwa majanga kabisa…sijui nini kimewapata?
 
Shida ni wewe kutokumjibu.
Hicho kitu kinamtafuna akili kisawa sawa.

Mybe umuulize ana shida gani au anataka mahitaji ya mtoto.

Pia panga ukutane nae na umwambie status yako wewe sasa hivi ili asije kuku haribia.
Asijaribu kukutana na mpumbafu Kama yule Ni vyema akanendelee kuwa kimya Hadi kiama

Usimuandekeze mwanamke mpumbafu
 
Back
Top Bottom