Imepita miaka 7 toka tumeachana, jana kanitumia SMS ya kejeli

Imepita miaka 7 toka tumeachana, jana kanitumia SMS ya kejeli

Mueleze mkeo kuwa una mtoto, Huyo mwanamke kinachomsumbua ni mtoto kukosa baba. Akimuangalia anakukumbuka ni vile hana busara.
 
Tili'chee boss, lakka?
Uyo inaonyesha uko alipo hakuna kilicho muendea sawa.
Na hapo mtoto kashalishwa sumu na mama yake na atakuchukia tu.
Yote kwa yote usijaribu kubishana nae wala kujihusisha na kelele zake.
Mtoto akishakomaa akili atakutafuta tu labda usiwepo duniani, ila jitahidi pia kumhudumia mtoto.
Boss nilibe vo kukamba, vinasiliza naluta manje apa, zikomo.
 
Wakuu mulibwanji? Mambo huku ni tabulele laaa.... Nilipokuwa chuo nlikuwa kwenye mahusiano na mdada mmoja wa Kiha nlimpenda sana na tulifanikiwa kupata mtoto 1, kiukweli nlitamani ndo awe wife kumbe nilikuwa najiandalia bomu hasa alipotangulia kupata kazi.

Alikuwa kasomea ualimu, nilianza pewa maneno makali sana kama mwanaume suruali, shetani, ilifikia hatua naambiwa nanuka. Nilijipanga nikaamua kuondoka zangu nilimuachia kila ktu nlichopata nae. Mtoto alimkatalia akasema ili nimchukue nihakikshe nimemuua nikamwambia mtoto nimekupa sasa ni wako.

Lakini ajabu visa vikawa haviishi, alikuwa akinitumia sms za kunitukana sana na maneno mengine ya hovyohovyo, sikuwa namjbu zaidi ya kumpuuza. Alianza watafuta ndugu na marafiki zangu anawaambia tuhuma kibao kuhusu mimi hiyo ni baada ya kuwa nlishaondoka.

Nilishangaa sana kwanini bado ananifatilia wakati namuaga aliniambiaga sepa huko. Ajabu hata nilikuwa nikibadili namba atapambana ataipata na ataanza kunitumia ma sms ya matusi mpaka kunitukania wazazi wangu.

Sasa imepita miaka 7 toka nimeachana nae, nilishaoa na nina mtoto 1 tayari nikajua mwenzangu alishasahau na pengne ana bwana ake maana umepita muda sasa wala hata sijui chochote kuhusu maisha yake. Jana usiku saa tatu. Nashangaa inaingia sms ya kejeli kucheck namba nikagundua ni ile ya yule muha ex wng.

Nilishangaa sana huyu mtu mbona imepita miaka mingi sana bado ana mambo yaleyale ana matatzo gani. Kwa kweli hata sikumalizia soma sms ile nilifuta hata sikuijbu kbs. Wakuu mtu kama huyu ni nini kinamsumbua. Je ni hasira au bado ananipenda au ananichukia tu? Karibu kwa maoni yenu.

Mnapendana, rudianeni, sisi hatuna shida, kiburi ni jambo baya sana, mnapendana ila mna viburi.
 
Kausha

Ukijibu ndio utampa moto.

Amekosa attention anaitafuta kwako.

Dawa ya Wanawake wa dizaini ni kula bonge la buyu

Usibadiki namba kabisa

Yaani kausha kama sio wewe.

Atachoka mwenyewe yaani hata usimblock.

Na meseji zake usizisome kabisa zikiingia tu FUTA bila kuzifungua.

Na simu yake usipokee.

USIMPE ATTENTION YAKO MWANAMKE MPUMBAVU UTAKUWA UNAMP BICHWA.
 
Asijaribu kukutana na mpumbafu Kama yule Ni vyema akanendelee kuwa kimya Hadi kiama

Usimuandekeze mwanamke mpumbafu
Akutane nae ajue hali ya mtoto wake..
Ila kama akiendelea kukaa kimya pia inaweza ikawa big issue yule mwanamke akijua jamaa anapo kaa na kuja kumwalibia kabisa....
 
Magonjwa ya akili yapo kabisa, watu huugua bila kujijua Sasa mshaachana Bado anakufuatilia huoni kuwa ana ugonjwa wa akili huyo!.
 
Kausha

Ukijibu ndio utampa moto.

Amekosa attention anaitafuta kwako.

Dawa ya Wanawake wa dizaini ni kula bonge la buyu

Usibadiki namba kabisa

Yaani kausha kama sio wewe.

Atachoka mwenyewe yaani hata usimblock.

Na meseji zake usizisome kabisa zikiingia tu FUTA bila kuzifungua.

Na simu yake usipokee.

USIMPE ATTENTION YAKO MWANAMKE MPUMBAVU UTAKUWA UNAMP BICHWA.
kweli kabisa Mangungo II mwanamke yeyote anayekuchukulia poa, revenge yako kali ni kutokumpa attention na mikausho mikali. ukifanya hivyo lazima achanganyikiwe. Hakuna kitu kinamuuma mwanamke kama kumkalia kimya na kumchunia kama wadau wengine wanavyosema.
 
Huyo mwanamke alianza kukutukana baada ya kupata bwana mpya na kama ilivyo kawaida ya kanuni ya karma na sasa bwana wake amemuacha na hana pakujifariji kabisa na kitendo chako cha kutokumjibu ndio kinamfanya awe chizi…
Kamwe usimjibu lakini hakikisha umemwambia kila kitu huyo mkeo mpya…hakikisha umemwambia kila jambo maana kinachofata ni kumtukana mkeo…..!

Ila nimehisi harufu ya wewe bado kumpenda huyo mwanamke…usininukuu vibaya lakini nimehisi bado unampenda….kama hayo ndio kweli yanakusumbua kutoka kwake hakika nasihisi harufu ya upendo kati yenu nasiku si nyingi usipotafuta njia ya kumpotezea mazima hakika hiyo ndoa yako mpya ya miaka saba itakuwa historia!

Kamwe ,Kamwe,Kamwe,Kamwe usimrudie mwanamke aliyekuacha au aliyekusaliti maana utajuta maisha yako yote!

Yani zamani tulijenga sana imani kwa Walimu lakini sasa nao wamekuwa majanga kabisa…sijui nini kimewapata?
kweli awe makini, kwa maelezo ya jamaa inaonesha bado anampenda. hivi unawezaje kurudiana na ex wako.
 
Wakuu mulibwanji? Mambo huku ni tabulele laaa.... Nilipokuwa chuo nlikuwa kwenye mahusiano na mdada mmoja wa Kiha nlimpenda sana na tulifanikiwa kupata mtoto 1, kiukweli nlitamani ndo awe wife kumbe nilikuwa najiandalia bomu hasa alipotangulia kupata kazi.

Alikuwa kasomea ualimu, nilianza pewa maneno makali sana kama mwanaume suruali, shetani, ilifikia hatua naambiwa nanuka. Nilijipanga nikaamua kuondoka zangu nilimuachia kila ktu nlichopata nae. Mtoto alimkatalia akasema ili nimchukue nihakikshe nimemuua nikamwambia mtoto nimekupa sasa ni wako.

Lakini ajabu visa vikawa haviishi, alikuwa akinitumia sms za kunitukana sana na maneno mengine ya hovyohovyo, sikuwa namjbu zaidi ya kumpuuza. Alianza watafuta ndugu na marafiki zangu anawaambia tuhuma kibao kuhusu mimi hiyo ni baada ya kuwa nlishaondoka.

Nilishangaa sana kwanini bado ananifatilia wakati namuaga aliniambiaga sepa huko. Ajabu hata nilikuwa nikibadili namba atapambana ataipata na ataanza kunitumia ma sms ya matusi mpaka kunitukania wazazi wangu.

Sasa imepita miaka 7 toka nimeachana nae, nilishaoa na nina mtoto 1 tayari nikajua mwenzangu alishasahau na pengne ana bwana ake maana umepita muda sasa wala hata sijui chochote kuhusu maisha yake. Jana usiku saa tatu. Nashangaa inaingia sms ya kejeli kucheck namba nikagundua ni ile ya yule muha ex wng.

Nilishangaa sana huyu mtu mbona imepita miaka mingi sana bado ana mambo yaleyale ana matatzo gani. Kwa kweli hata sikumalizia soma sms ile nilifuta hata sikuijbu kbs. Wakuu mtu kama huyu ni nini kinamsumbua. Je ni hasira au bado ananipenda au ananichukia tu? Karibu kwa maoni yenu.
Akikutukana tena mfungulie kesi
 
Back
Top Bottom