Imeshindikana vipi kuwapa tenda DP world au shirika lingine kuwa train kwa vitendo watanzania kusimamia bandari kwa miaka miwili kisha wao kuondoka?

Ndio imeshindikana Sasa kwani hiyo Bandari si imekuwa inasumbua sua kwa miaka zaidi 60 Sasa hakuna jipya?

Kwanza Kuna sekta gani ambayo Tanzania inafanya Kwa ufanisi? Kuanzia sekta za biashara Hadi Huduma za jamii ni hovyo tuu..

Kote huko Kuna Wataalamu waliobobea ila hulka na tabia za Watzn ndio shida tupu.
 
Kabla ya kutrain watanzania kusimamia bandari iundwe sheria kali ya maadili ya utumishi wa umma kama zile za china. Amini amini nakwambia shida sio technolgy shida ni uadilifu wa watumishi wetu kuanzia waziri wa wizara husika katibu mkuu hadi mlinzi gettini hapo bandarini
 
Tatizo ni kuwa mwizi wa yeboyebo mnamchoma moto hadharani,

Maliasili wanahukumu wazee wenye asali Lita 20 na kuwanywesha mpaka wafe, wakikuta na nsha au nyama pori wanakulisha mbichi mpaka iishe

Ila majizi makubwa unasikia mkurugenzi kaiba hela za mradi wote badala yake kahamishwa

Siku mkiwafunga majizi hao na kuwaanika hadharani kwa wizi wao Yaani unapeleka mahakamani kila mwizi na kufungwa bila kikomo hapo watashika adabu

Hili ndio tatizo letu kubebana
Watoto shukeni wanapigwa kisa kafeli ila mwalimu anaiba lunchbox ya mtoto anakula vyote

Nina uchungu sana na nchi yangu ila sina la kufanya
 
Bado Taifa linahitaji
Ukomboz
Mapinduz
Mageuzi
Watu wapya



Kesi za walalahoji ndio hupelekeshwa.
 
Hivi kwanini hatutaki kukubali sababu zinazosababisha kukwama kwa kupata faida kubwa na uendeshaji wenye tija?
Mbona jawabu ni kutokuwa waaminifu
Tuwe waadilifu na tufanye kazi bila wizi, Haki tutafika mbali sana
Exactly, tatizo sie Watz, kutokana na experience uaminifu na tabia ya wizi Kwa wengi wetu ni kama chanda na pete, hivyo kusimamia mambo yetu ni shida....
 
Bila taasisi imara ni ngumu sana kudhibiti watoto
 
Sahihi kabisa 100%
 
Waarabu wataongeza ufanisi wa Bandari kufikia full capacity.

SGR itashiba wenye Maloli watashiba hata hiyo TAZARA itashiba.
 
Mbona mnakwepa kuwataja waliotufikisha hapo? Adui mkubwa wa taifa letu mbona anajulikana? Hebu tuache unafiki!
Tukimtaja mara kwa mara inakuwa tunamfanyia promoshen !
 
Natamani hata sekta zingine zingebinafsishwa watanzania wizi wizi Sana natamani hata MSD angepewa mwekezaji tu ufanisi ungekuepo hivi hamuoni jinsi TBL ya wazungu inovoenda vzr hapa Tanzania ,, inabidi as a nation tuwe full capitalist nation
 
Niambie baada ya miaka 60 ya Uhuru Mtanzania ameweza kitu gani? Hata baada ya wengi kusoma na kusomeshwa nje ya nchi ni kipi wamekiweza kinachoendana na uwekezaji huo?
Tena bandari ni kitu kidogo sana, mimi ningeshauri hata pale Ikulu na bungeni wangetafuta raia wa kugeni watuongoze.
Tena afadhali hata Ikulu tuna mtu ana Uzanzibar na u-Oman ndiyo angalau mambo yanaenda enda. Angekua Mtanzania pure tungekwama mazima huku tunashangilia na kuitana mawe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…