Imetajwa kwamba uchawi ni mdudu ambaye ameitafuna sana Kigoma na watu wake, ndio sababu ya watu wengi kutokurudi nyumbani

Imetajwa kwamba uchawi ni mdudu ambaye ameitafuna sana Kigoma na watu wake, ndio sababu ya watu wengi kutokurudi nyumbani

Kigoma Region Tanzania

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
230
Reaction score
611
Imetajwa kwamba uchawi ni mdudu ambaye ameitafuna sana Kigoma na watu wake, ndio sababu ya watu wengi kutokurudi nyumbani, point ya 1.

Watu wa Kigoma hawana tofauti na Mayahudi wa Israel, tofauti yao ni kwamba watu wa Kigoma wana ardhi ila mayahudi walikosa ardhi.

Kigoma ina watu makini sana katika kila nyanja ndani ya nchi hii kutokana na kutapakaa kwao, talanta zao, elimu zao, nguvu zao na harakati zao kama ilivyo kwa mayahudi ni watu makini sana duniani kote.

Lord Rothschild, alipoliona hilo akaamua kuanzisha harakati za kuwakusanya Mayahudi na kuwaeleza kwamba 'Sisi ni wachache sana, lakini nguvu yetu imetapakaa duniani kote lau kama tutaamua kuikusanya nguvu hii sehemu moja tutakua na uwezo wa kuendesha Dunia hii'' kisha akatoa msululu wa mifano kadhaa wa kadha ya wayahudi waliokua na uwezo sehemu mbalimbali za dunia.

Harakati za Mayuhudi kujirudi na kuunganisha nguvu zao sehemu moja ndio ikaitwa 'Uzayuni'. ''Zionism' ni harakati za Lord Rothschild, kuwakusanya mayahudi popote pale walipo kuwaleta sehemu moja ambayo ni Israel' point ya 2

Kuwanukuu Mayahudi haina maana ya kuunga mkono kinachoendelea huko Mashariki ya kati, ila ni kutaka kuunganisha falsafa hii kwa watu wa Kigoma ambao wanahisi uchawi ni sababu kuu ya watu kuukimbia mji na kushindwa kuwekeza nyumbani.

Sisi kama watu wa Kigoma tunaweza kuishi popote pale tutakapo, lakini Nguzo yetu kuu ya marejeo ikawa ni ardhi yetu ya Kigoma. Ili kitu kiwe nguzo ni lazima kiwe imara haswa, na ili kiwe imara hakina budi kujengwa na kuendelezwa hata kama wewe hauishi hapo.

Tutafute mafanikio popote tulipo lakini tujitahidi walau asilimia 10 ya kile tunachopata kwa mwaka tukirudishe Nyumbani kwenye Nguzo zetu kuu, iwe ni fadhila na kafara kwa kile tunachokifanya mbali na nyumbani.

380367498_741495861322569_8916787361050469411_n.jpg
 
Mda unavyozidi kwenye huu utambulisho wa kikabila utakuja futika kabisa , tunaoana na kuzaliana na watu wa kutoka jamii mbalimbali .
 
Mda unavyozidi kwenye huu utambulisho wa kikabila utakuja futika kabisa , tunaoana na kuzaliana na watu wa kutoka jamii mbalimbali .
Ndio ukabila utafutika kabisa ,maana wengi wanakimbilia mjini
 
Back
Top Bottom