Imethibitika sasa Corona iko mitaani Dar. Napata shaka kwanini Serikali sasa wako Dodoma ghafla hivi

Imethibitika sasa Corona iko mitaani Dar. Napata shaka kwanini Serikali sasa wako Dodoma ghafla hivi

Makonda karopoka bila kujua ametoa siri, Corona ipo mitaani Dsm, ndio maana Rais akaenda kujificha kwenye mawe Dodoma, matokeo yake uropokaji wa Makonda unaleta tension kwa wakazi wa Dsm, wakati lengo la serikali lilikuwa watu wasijue kama Corona ipo mitaani Dsm.

Kutafuta sifa za kijinga kumemuaibisha na kuwaaibisha wote waliohusika kutoa taarifa za mtoto wa Mbowe, na Mbowe nae kamalizia kwa msumari mtoto wake hajatoka nje ya nchi mwaka mzima, kwahiyo kaipatia humu humu ndani, sasa kazi ipo kwa wakazi wa Dsm kujihakikishia usalama.

Sent using Jamii Forums mobile app
To make long story,short. Dawa ya corona ni kujificha kwenye mawe tu, hakuna namna nyingine.
Ama kweli "Ujinga Mzigo"😂😂😂
 
Mbona wengine hawakutajwa na hata kama walitajwa majina yao mbona mbowe ikawa ni station ya mabasi? Makonda ni mpumbavu kuwa kutokea katika nchi hii familia ya mbowe wajihadhari sana na hawa wakina Makonda yawezakana mwanae akapekewa huu ugonjwa tu ili wapate cha kusema najiuliza kwanini Makonda afurahie hili jambo?kuna walakini ndani yake ila kwa tahadhari kubwa sana mbowe na familia yako waadui zenu ni wengine mno sasa huu ugonjwa ndiyo silaha yenu kuwamaliza kwa hawa wanaojiita wanamjua mungu kuliko wengine. NARUDIA TENA MBOWE MBOWE MBOWE KUWA MAKINI NA FAMILIA YAKO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ok upo dar so wht? unataka tulog out city au? ugonjwa upo ila hauna madhAra makubwa kwa sabAb ya taahadhAri zinazochukuliwa na serikal...

kunawatu hum hamfikrii vyemA madhara yA kulockdown city... serikali inataarifa nyingi kuliko mimi na ww...

ni kwel upo ila hauna madhara...
 
Je, huu ni uzalendo?

Je, watarudisha mafoleni yao Dar corona ikipita?

Je, kweli mnafikiri tutaendelea kuwa na imani na nyie?

Mnakimbia mji for a leason wanaobaki waumie peke yao?

Nawakumbusha tu ugonjwa haukimbiwi wacha sisi tupukutike. tusiwaone Dar wakati wa starehe bakini uko uko dodoma hata corona ikipita tusiwaone town.
 
Ukiangalia takwimu za nchi zenye matatizo ya Corona wanatoa mbili kuna zile za vipimo vilivyofanyika tayari ambapo idadi ni ndogo mfano nchi inaweza sema kuna watu 8000.

Watu hao wanatumia takwimu za estimate ambapo wanajua mtu mmoja anaweza ambukiza watu kadhaa kupitia hizo za pili wanaweza kadiria labda maambukizi ndani ya nchi nzima hayawezi kuwa chini ya watu 82000.

Hizo takwimu za makadirio ndio zinatumiwa kama kigezo cha decision making Corona inaweza pita kwa wengi kama homa ya kawaida tu; hila wengi pia wanaweza ambukiza wengi zaidi wakiachwa wazagae tu na risk ya kuwakumba vulnerable groups inaongezeka na hili ndio kundi linalojaza mahospitali.

Sie bado wanasiasa wanachukulia poa kuja hadharani na kusema wanaamini hakuna kesi ata moja; waliopo wote wamepona badala ya kubaki na imani kuna watu huko mtaani wanasambaza kama umeshaingia na tunaelekea kwenye pandemic ya ndani.
 
Hatarioz....iko Dar na takwimu zao za maambukizi zinatia shaka. Halafu mtoto wa baba, anapiga kampeni danganyifu..

badala ya kuhimiza kujikinga na nini cha kufanya endapo utahisi una maambukizi. Eti atapuliza dawa, anafikiri hii ni malaria, dengue au kipindupindu?

Everyday is Saturday 😎
Angalia hiko kipande ujue takwimu sahihi ya nchini.
 

Attachments

  • VID-20200325-WA0003.mp4
    1.3 MB
Je huu ni uzalendo? Je watarudisha mafoleni yao Dar corona ikipita? Je kweli mnafikiri tutaendelea kuwa na imani na nyie? mnakimbia mji for a leason wanaobaki waumie peke yao? nawakumbusha tu ugonjwa haukimbiwi wacha sisi tupukutike.
Raisi wa wanyonge kawakimbia wanyonge, acha korona iwanyonge wanyonge
 
Ukiangalia takwimu za nchi zenye matatizo ya Corona wanatoa mbili kuna zile za vipimo vilivyofanyika tayari ambapo idadi ni ndogo mfano nchi inaweza sema kuna watu 8000.

Watu hao wanatumia takwimu za estimate ambapo wanajua mtu mmoja anaweza ambukiza watu kadhaa kupitia hizo za pili wanaweza kadiria labda maambukizi ndani ya nchi nzima hayawezi kuwa chini ya watu 82000.

Hizo takwimu za makadirio ndio zinatumiwa kama kigezo cha decision making Corona inaweza pita kwa wengi kama homa ya kawaida tu; hila wengi pia wanaweza ambukiza wengi zaidi wakiachwa wazagae tu na risk ya kuwakumba vulnerable groups inaongezeka na hili ndio kundi linalojaza mahospitali.

Sie bado wanasiasa wanachukulia poa kuja hadharani na kusema wanaamini hakuna kesi ata moja; waliopo wote wamepona badala ya kubaki na imani kuna watu huko mtaani wanasambaza kama umeshaingia.
 

Attachments

  • VID-20200325-WA0003.mp4
    1.3 MB
Back
Top Bottom