Imethibitika sasa Corona iko mitaani Dar. Napata shaka kwanini Serikali sasa wako Dodoma ghafla hivi

Imethibitika sasa Corona iko mitaani Dar. Napata shaka kwanini Serikali sasa wako Dodoma ghafla hivi

Kwani walikupa sababu mkuu au unajiongeza?
Wapo kazini tu, maana corona ikikutaka hata uwe kijijini sitimbi itakutafuna tu.
 

Kama wanadhani kwa wenzetu hizo sports centres na hotels kubwa zinazotengwa kuchukua wagonjwa ni mzaha; au nchi zingine kuwataka nurses wa mwaka wa mwisho kuingia kazini bila kuhitimu na medical staff wote walio retire warudi makazini ni kwa sababu ya mzaha we got another thing coming.
 
Kulingana na Makonda jana, Watanzania Mungu anatupenda sana hawezi kufa mtu.
Kwa akli yake mbovu anaamini hivyo. Eti Tsunami haikutupata, kimbunga na Ebola hatukupata itakuwa haka kakorona? Yaani anaona watz ni wateule wa Mungu na hakuna baya ambalo linaweza kutupata. Anafikiri huko kote ambako watu wanateketea kwa kasi hawamjui Mungu? Au anafikiri Mungu anaishi Tz tu?
Huyu DAB kuna kitu hakiko sawa kwa mkichwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... siku ile pale Ubungo interchange mbele ya camera akikagua "maendeleo ya kazi"; akatangaza rasmi kusitisha mbio za mwenge; akatangaza rasmi corona haijaingia Tanzania lakini jioni ya siku hiyo hiyo waziri wa afya akatangaza corona kuingia kupitia KIA/Arusha;

then huyoo nduki akaelekea Morogoro kukagua daraja na kutumbua watu then hakurudi tena Dar since then hadi alipoonekana akiwa amelala juu ya mawe/miamba Dodoma nikajua zile zilikuwa drama za kukimbia gonjwa!
 
Iko mitaa gani?, tuanze kutimua mbio

Sent using Jamii Forum's by simcard

Umeambiwa iko Dar(Jiji Lote na viunga vyake)k.m. Ikulu ya Magogoni, Kigamboni,Kariakoo hasa mitaa ya Msimbazi na Kongo,Ubungo,Mwenge,Mbagala,Temeke,etc...!
Wewe unafikiri kwanini Magufuli amegeuka ghafla kuwa Mjusi Kafiri wa kukaa kwenye Mawe na KUPIGA picha za Selfie akiwa Dom? Dar haikaliki baba kutokana na Kirusi Cha Covid-19!
Ni hatari Sana...!
 
jd41, Je, Mbowe alificha ugonjwa wa korona nyumbani kwake (mwanae mgonjwa) kwa siku 5, pamoja na kwamba mama wa mtoto ni daktari?

Lawama za kitoto hizo!!
 
Makonda ka Break the news!! wacha tuone maana Rais alitamka kabisa kwamba Hakuna mtu yoyote wa kuongelea huu ugonjwa isipokuwa Yeye, Waziri mkuu na Waziri Ummy tu.

Haya sasa toto la baba lishaharibu - wacha tuone.
 
Ni kweli yawezekana Corona ipo mitaani, lakini uongo kusema serikali ipo Dodoma eti kisa Corona. Serikali ilishahama siku nyingi Dar es salaam. Hata rais alishahamia Dodoma siku nyingi tu, kama una kumbukumbu sawa, hata uchaguzi wa serikali za mitaa alijiandikisha Dodoma na siyo Dar es salaam.
 
Mtu ambae alikuwa haelewi kuwa Corona kishaingia Tanzania, hiyo atakuwa poyoyo wa mwisho.

Corona hayupo Dar Tu, Corona yupo Tanzania nzima na hata Dodoma yupo.

Dodoma serikali haikuhamia leo wala jana. Ni poyoyo tu asiyeelewa kuwa serikali ilishahamia Dodoma siku nyingi.

Kila mtu anatakiwa achukuwe hatua za salama za kujilinda yeye na wengine. Msingoje serikali iwafanyie kila kitu. Serikali yenyewe ni binaadam kama sisi na wao pia hawapo salama kwa corona.

Tusiwe wajinga.

Hatutaki serikali itufanyie kitu ingawa ni jukumu lake kufanya kitu.

Serikali inatakiwa kutoa taarifa za kweli kwa wananchi wake. Kumbuka ban ya Marekani imechangiwa na kuficha taarifa za mgonjwa wa Ebola.

Leo hii Italia wanalia kama watoto wadogo kwa janga la corona.

Uzuri hii kitu haichagui umri, wadhifa wala uwezo wa kiuchumi, hivyo hata hao wanaoficha jamaa kesha gonga hodi mlangoni mwao.

Ugonjwa upo na unaendelea kupenya hadi vijijini.....baridi haijaanza ila cases za pneumonia zipo na zinakula maisha ya watu....Jiongezeni Watanzania...Wanasiasa hawana huruma, wako kwa ajili ya matumbo yao.
 
Hivi mnaamini kabisa kwamba amekimbia Covid-19?

Kwani kabla ya mlipuko wa huu ugonjwa hawakuwa wanaenda Dodoma?

Kwahiyo Covid-19 haipo Dodoma au haitafika Dodoma?

Acheni propaganda za ajabu!
Na hata hivyo, Corona ingeanzia kigoma Kwa mfano, Kwa maoni ya mtoa mada angelisema Kwa nini viongozi wasihamie huko!!!

Mbona ni kama wanatulazimisha kuwaita wajinga!!!
 
Bila lockdown haponi mtu.
Kama Wachina na teknolojia waliyo nayo wali introduce Lockdown na bado 3200+ wakafa....seuze Tanzania and other African countries??
Kwa sasa Mmarekani mwamba #2 wa Teknolojia ameanza kuhangaika na alikuwa akiwacheka Wachina kwa kuwaambia CORONA VIRUS NI VIRUSI VYA WACHINA......!!!
Mungu hadhihakiwi...Makonda must watch his silly mouth otherwise he gonna experience as same as Trump in the USA....!
 
Back
Top Bottom