Imethibitishwa shilingi Milioni moja na elfu hamsini imetumwa kwa Mama yangu Mzazi

Imethibitishwa shilingi Milioni moja na elfu hamsini imetumwa kwa Mama yangu Mzazi

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Hayo sio maneno yangu, bali ni maneno ya Vodacom Mpesa, wakinijulisha kuhusu muamala nilio ufanya asubuhi ya leo.

Miaka kadhaa iliyo pita hela hii ningeiweka kwenye akaunti ya Mr. Muggetta in the name of school fees.

( Nilikuwaga fala Mie.. Nizomeeni Kwa ufala nilio kuwaga nao)


Wewe unaesoma thread hii nakutamkia, siku moja mama ako mzazi atakuomba elfu Kumi ila wewe utamtumia Milioni Kumi.

Sema " NAPOKEA".

Breaking News: Meseji ya Bimkubwa hii hapa👇👇👇👇👇

Baba nashukuru Sana Mungu akubariki wewe na watoto wako. Ulipo toa Mungu akuzidishe mara millioni.

Me : Ameen 🙏🙏
 
Si tunashindana haya tuendelee unajua hapo nilituma ngapi?
Screenshot_20250128_125531_Messages.jpg
 
Umefanya vema ndugu, na kama huo ndio uwezo wako kwamba ungempeleka Magetta Pre & Primary school usingeweza kumtumia mama 50k basi ni sawa. Kuna waliopeleka Magetta na wanatumia wazazi, kuna waliopeleka Msigani Primary school na hawawezi kutuma 10k kwa mama.

Ndio maisha, tukubali kwamba kuna madaraja kwenye haya maisha.
 
Si tunashindana haya tuendelee unajua hapo nilituma ngapi?
View attachment 3216414

Mkuu hongera Sana. You are the true son of your father.

Kuhusu kushindana Mimi sishindani. I am just inspiring.

Siwezi kushindana na fake profiles.


Anyways wazo lako Sio baya pia tukishindana kuwapa mama zetu hela wanufaika watakuwa mama zetu na Baraka zitakuja kwetu pia.

Ni wazo Zuri Sana kianzishwe kipindi kipewe jina " Mcheki Bi Mkubwa" Kwenye kipindi unaalika watu mbalimbali mnapiga story then mwisho wa siku wanatuma live hela kwa Mama zao.
 
Kuna siku mtu akijamba atakuja kusema mbona Leo ushuz unanuka sana ? Hivi kumpa mzazi wako hela ni jambo la kuanzishia uzi kweli ? Mbona mambo ya kawaida ambayo kila mtu anafanya kwa jinsi/namna anavyoona ? Jf imekuwa ya underrated sana nowdays,,, ! Hii ulitakiwa upeleke Facebook ukapate likes na comment
 
Back
Top Bottom