Imetimia miaka kumi tangu nianzishe ukoo wangu, maendeleo ni mazuri

Imetimia miaka kumi tangu nianzishe ukoo wangu, maendeleo ni mazuri

Binafsi naionaga karma kama haina uhalisia, imagine dhulma na mauaji wanayofanya wanasiasa duniani kote bt still wanakula bata na familia zao miaka nenda rudi, je karma ina ubaguzi? Nipe darasa kidogo mkuu.
Karma...ni kitu halisi...Kuna jamaa anafanya utafiti Marekani...KWA UFUPI
mfano.watoto wasio na hatia wameuawa wakiwa shule...mtafiti kafuatilia kagundua kumbe babu yao au baba wa babu yao alikwisha mwaga damu isiyo na hatia....ISIPOKULAMBA WEWE ITALAMBA UZAO WAKO....
 
Kuna uzi humu wa jamaa ambaye amezinguana na wazazi wake kwa miaka mitatu.

Mimi yakiwahi kunikuta, ni baada ya kukaa ughaibuni kwa miaka kadhaa na kurudi nchini mikono mitupu.

Dunia ina rangi nyingi sana, hakuna rangi sukuona, ndugu walinitenga sana, upendo wa wazazi sikuuona kabisa.

Mwaka 2013 rafiki yangu akanishauri kutafuta maisha mkoa X, nilienda na shilingi laki moja ila jamaa alikuwa mwenyeji maeneo yale na tulifanikiwa kufanya biashara ya kulangua mazao ya mbogamboga, tunanunua nyanya, hoho, vitunguu au pilipili na kutuma Dar.

Ndani ya mwaka mmoja nilikuwa na akiba ya kutosha bank, kumbuka hapo hakuna ndugu anayejua nilipo.

Niliweza kukodi mashamba na kujikita kwenye kilimo. Ule mkoa ulikuwa na wanawake wazuri sana wanaokuja kuomba vibarua shambani, sikubaki nyuma nilikuwa naingia nao kwenye mahusiano mafupi au marefu.

Kwa kipindi cha miaka kumi nimebahatika kupata watoto kama 30 na wanatumia ubini wangu.

Zoezi la uzalishaji linaendelea, nilinunua shamba kubwa mbali na wanakiji kwa gharama ya milioni tano tu, eneo lilikuwa msitu nilifyeka na Kuanza ufyatuaji wa tofali za kuchoma, kuchimba kisimana ujenzi wa vijumba slopes kumi kwa wake zangu, nimejenga pia bweni dogo kwa ajili ya watoto wa kiume.

Nikiwa kijijini mimi ni mwanakijiji haswaa, nikiwa Dar naishi kwenye single room.

Naweza kusema nina nafsi mbili.
Moja ni ile ya village life na nyingine ni urban life.

Lengo langu ni kutimiza watoto 50, sina ndugu ninayewasiliana nae zaidi ya wana JF nyie ndio ndugu zangu pamoja na watoto wangu na wanawake wanne niliozaa nao,ambao walikubali niishi nao kijijini

Watoto wangu hawawajui shangazi zao wala baba wadogo/wakubwa, bibi wala babu.

Inawezekana kabisa kuanzisha ukoo wako hujachelewa ndugu yangu.

Nikupe moyo ewe kijana uliyekata tamaa mjini bila kujali elimu yako,njoo manyara jikite na kilimo tafuta mke oa anzisha familia,huku kuna wanawake wazuri sana kama ilivyo ardhi yao nzuri

Tofauti ba ujinga ujinga ninaopost humu mimi ni mtu mzima,mwaka 1986 kombe la dunia,nilikuwa na miaka 8 niliangalizia nyumbani kwa Sheikh Yahya,magomeni,aliweka screen kubwa sana pale nje size ya kioo cha mbele cha fuso,pembeni kaoaki limossine yake milango sita
Hapo kwenye ndugu zako na mimi nipo
 
Binafsi naionaga karma kama haina uhalisia, imagine dhulma na mauaji wanayofanya wanasiasa duniani kote bt still wanakula bata na familia zao miaka nenda rudi, je karma ina ubaguzi? Nipe darasa kidogo mkuu.
Kwenye bible kuna mstari unasema,nawapatiliza wana naovu ya baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne.
Maisha yako ya leo huenda ni outcome ya matendo ya babu yako au baba wa babu yako
 
hao wanawake si kikwazo ni fursa adimu, ila kwa upande mwingine brother umetengeneza singo maza wengi
SIkuwa na lengo baya sema ile kujua natoka mjini nijikuta kila mwaka naletewa mimba si chini ya tatu,wambulu ni wazuri mno na hawajui kukataa
 
Upande wa pili kuna vijana wakienda majuu basi dharau kwa wazazi na ndugu,majivuno ,anasa,wanasahau walipotoka, jeuri , wakifilisika wanarudi huku kuleta Story nyingine na kuzipamba waonekane hawana Hatia. HAWAOMBI MSAMAHA
 
Uko sahihi ila bado anastahili upendo
 
Kweli kabisa,ukitaka kuwajua ndugu na rafiki wa kweli firisika
Mie nilichoka kiukweli asubuhi panakucha sijui niende wapi sijui nitakula nini na kipindi hicho mwanangu mdogo bado ananyonya......nilihamia kwenye pagale langu halina mlango....choo ni mifuko ya cement nimeunga unga simu sina...kila jina baya nilipewa...waliniita mpaka mchawi...mpaka kanisani nilikuwa kama kituko...Kuna siku mahubiri yalinihusu mimi kama mfano...wengine wakasema nina laana...wengine wakasema nina roho mbaya ndio maana sifanikiwi.......AISEE
 
Karma...ni kitu halisi...Kuna jamaa anafanya utafiti Marekani...KWA UFUPI
mfano.watoto wasio na hatia wameuawa wakiwa shule...mtafiti kafuatilia kagundua kumbe babu yao au baba wa babu yao alikwisha mwaga damu isiyo na hatia....ISIPOKULAMBA WEWE ITALAMBA UZAO WAKO....
Ilipaswa wahusika ndo wapate masaibu na si wasiohusika direct, na hapa ndo huona kama karma haina uhalisia.
 
Kwenye bible kuna mstari unasema,nawapatiliza wana naovu ya baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne.
Maisha yako ya leo huenda ni outcome ya matendo ya babu yako au baba wa babu yako
Sio kila kilicho kwenye maandiko kina uhalisia, tizama ufalme wa UK wamehusika direct kwenye ukoloni, na vizazi zaidi ya vitatu kwao tayari vimepita bt karma huioni kwao, karma haina uhalisia mkuu.

Kuna nadharia nyingi tunazitumia kujifariji bt ukizichunguza kwa utulivu hazina uhalisia kabisa.
 
Back
Top Bottom