Imetimia mwezi mmoja sasa tokea nimeanza kukaa na Mwanamke, natamani nimtimue

Wewe una moyo mgumu sana, mwezi mmoja? Unakaa na malaika? Mimi siku 3 tu nishamchoka.
 
Mademu wanavyopenda tamthilia na internet yeye muda huo anautowa wapi? Au huna TV na hulipii subscription? Umemnunulia smartphone? Unamuwekea bando?

Siamini mwanamke mwenye access hizi kama ana muda wa gossiping za waswahili.
 
Jumamosi mnatakiwa ushinde naye ndani siku nzima jioni unatoka ukirudi unakesha naye mpaka Jumapili jioni, sawa.
 
Mi alijichanganya eti anaenda kwao, kesho yake asubuhi nikampeleka Ubungo!

Hizi stress zisikie tu, wanawake wanaojielewa sijui wanapatikana wapi!
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Mi niliamka kwenda kwenye mazoezi asubuhi kurudi nikakuta mtu keshamaliza kupaki na mabegi tayari tayari. Nauliza kulikoni mwenzangu mbona ghafla au kuna msiba home? Kimyaaa!

Wala sikuuliza ila niliita bajaji chap ili imuwahishe Mbezi kwa Magufuli. Wiki ya tatu sasa hata sijui kama alifika salama alikokuwa anakwenda ama la! [emoji706][emoji706][emoji706]
 
Jamaa ameshakula sasa amemkinai mapema hapa anatafuta tu sababu ya kuingia mitini.

Ila nawatahadharisha tu mtindo wa kuchezea mabinti za watu na kuwakimbia mkumbuke kuna kurogwa, ni vitu nimeshuhudia kwa macho yangu sikuhadithiwa.
Hapana ndugu yangu, Kuna siku nimemzingua sana akampigia simu mama yake, nikamwambia Mama yake jinsi ilivyo, tatizo ni jambo moja tu ambalo linaleta mgogoro, Mazoea Mazoea na watu ndio chanzo. Na Mimi tokea nimezaliwa kwa mzee wangu Familia yetu mzee wangu alikuwa anapinga sana mazoea ya hovyo na watu watu, ndio principle niliyokuwa nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…