Imetimia mwezi mmoja sasa tokea nimeanza kukaa na Mwanamke, natamani nimtimue

Imetimia mwezi mmoja sasa tokea nimeanza kukaa na Mwanamke, natamani nimtimue

Dah wazee, kutokuoa ni Bora kuliko kuoa, nimekaa Miaka mingi ya u-bachelor mpaka age ilipoanza kusonga hivi, maisha yangu yote yalikua ya furaha isiyo na kifani, Sina stress za hovyo hovyo naweza kujiamulia kwenda sehemu yoyote bila stress, mipango yangu Ilikua inaenda sawa kidogo nachokipata najibana nikajikita kununua mashamba, kiufupi maisha yalikua mazuri though nilikua na mchumba mmoja wa muda mrefu kidogo, nikasema nivute niiweke sawa nikatoe mahali baadae kidogo.

Ni mwezi mmoja tu Lakini stress nilizonazo ni kama nimekaa Miaka 70 kwenye ndoa, ogopa Mwanamke mjuaji , kiburi Cha chini chini asiefata maelekezo kichwa changu kinawaka moto vibaya mno Sina furaha tena nimemtimua aondoke amegoma naona hapa Mimi ndio nitimke kimya kimya nimuachie vitu nisepe.

Ninapokaa hapa Nina miaka 5 Sina mazoea na watu kabisa sipendi kuzoeana na siruhusu mtu anizoee zaidi ya salamu (haswa Majirani) Wananiona mkorofi sana kwa sababu ya kutopenda mazoea, alipofika hapa nilimwambia principle yangu huwa sipendi mazoea na watu zaidi ya salamu na vitu vingine vidogo vya ku-socialize Lakini mazoea lazima yawe na mipaka. Ooh ndani ya mwezi ameshajuana na watu mbalimbali Majirani woote wanamfahamu.

Ndani ya Mwezi mmoja tu Majirani wote wanajua identity yake tokea alipozaliwa na mikoa aliyoishi Hapo kabla, kiukweli Sielewi but moyo wangu una hasira sana. Kiukweli sipendi kufungua password ya maisha yangu kabisa tena kwa stranger Lakini huyu yeye akitekenywa tu anafunguka vibaya mno japo tokea amekuja nimeshamwambia Zaidi ya mara 1000 never trust anybody Kila unaemuona mbele yako muone kama threat kwenye maisha yako, Lakini aelewi.


Kwa sehemu mbalimbali nilipopita Kwa nature ya mabinti kama huyu nilienae Ilikua rahisi sana kusex nae bila hata ya kumtongoza kwa sababu unachokifanya ni kutengeneza mazoea tu na trust kwa sababu wamejengwa kuamini watu mapema huwa wanaliwa kizembe tu.
Mmewezaje kukaa na Mwanamke mjuaji? Unalomwambia hafanyi? Wala maelekezo hafati?

Nimeona kwamba katika Maisha watu tupo na character tofauti tofauti, tumezaliwa katika mazingira tofauti tunapokutana ukubwani kimbembe Cha kubadilishana tabia ndio kinaanza unakua mwana saikolojia, sosholojia na filosofia bila kupenda.

Navyoona huko mbeleni kama naenda kupiga mtu vibaya mno.
Wewe una moyo mgumu sana, mwezi mmoja? Unakaa na malaika? Mimi siku 3 tu nishamchoka.
 
Nikitoka job namkuta yupo na Majirani huko nje, story zake tukiwa tunaongea. pia weekend huwa nashinda ndani asubuhi mpaka jioni akitoka nje akiwa anafanya shughuli zake, utamsikia Mimi Dodoma hivi na vile....eeeh Nina ndugu yangu pale....nimekaa sana pale.....nimesoma Hapo.....hata Mama yangu alishaugua huo ugonjwa.....chuma hayo majani yanatobu UTI. Nadhani umenielewa kaka, Sasa hiyo situation ya kuongea ongea sana sijisikii vizuri kabisa.
Mademu wanavyopenda tamthilia na internet yeye muda huo anautowa wapi? Au huna TV na hulipii subscription? Umemnunulia smartphone? Unamuwekea bando?

Siamini mwanamke mwenye access hizi kama ana muda wa gossiping za waswahili.
 
Nikitoka job namkuta yupo na Majirani huko nje, story zake tukiwa tunaongea. pia weekend huwa nashinda ndani asubuhi mpaka jioni akitoka nje akiwa anafanya shughuli zake, utamsikia Mimi Dodoma hivi na vile....eeeh Nina ndugu yangu pale....nimekaa sana pale.....nimesoma Hapo.....hata Mama yangu alishaugua huo ugonjwa.....chuma hayo majani yanatobu UTI. Nadhani umenielewa kaka, Sasa hiyo situation ya kuongea ongea sana sijisikii vizuri kabisa.
Jumamosi mnatakiwa ushinde naye ndani siku nzima jioni unatoka ukirudi unakesha naye mpaka Jumapili jioni, sawa.
 
Mi alijichanganya eti anaenda kwao, kesho yake asubuhi nikampeleka Ubungo!

Hizi stress zisikie tu, wanawake wanaojielewa sijui wanapatikana wapi!
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Mi niliamka kwenda kwenye mazoezi asubuhi kurudi nikakuta mtu keshamaliza kupaki na mabegi tayari tayari. Nauliza kulikoni mwenzangu mbona ghafla au kuna msiba home? Kimyaaa!

Wala sikuuliza ila niliita bajaji chap ili imuwahishe Mbezi kwa Magufuli. Wiki ya tatu sasa hata sijui kama alifika salama alikokuwa anakwenda ama la! [emoji706][emoji706][emoji706]
 
Jamaa ameshakula sasa amemkinai mapema hapa anatafuta tu sababu ya kuingia mitini.

Ila nawatahadharisha tu mtindo wa kuchezea mabinti za watu na kuwakimbia mkumbuke kuna kurogwa, ni vitu nimeshuhudia kwa macho yangu sikuhadithiwa.
Hapana ndugu yangu, Kuna siku nimemzingua sana akampigia simu mama yake, nikamwambia Mama yake jinsi ilivyo, tatizo ni jambo moja tu ambalo linaleta mgogoro, Mazoea Mazoea na watu ndio chanzo. Na Mimi tokea nimezaliwa kwa mzee wangu Familia yetu mzee wangu alikuwa anapinga sana mazoea ya hovyo na watu watu, ndio principle niliyokuwa nayo.
 
Back
Top Bottom