#COVID19 IMF: Tanzania lazima iweke wazi takwimu za COVID-19 ili ipate msaada wa dharura

#COVID19 IMF: Tanzania lazima iweke wazi takwimu za COVID-19 ili ipate msaada wa dharura

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Tanzania inahitaji kuweka wazi data ya ueneaji kwa Covid-19 kabla ya kupata idhini ya mkopo wa dharura wa Dola 574 milioni kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa. Maamuzi hayo yanatokana hali ya kutojulikana kwa takwimu halisi za ugonjwa huo tangu Serikali ilipoacha kuziweka wazi Mei mwaka 2020 wakati utawala wa Rais John Magufuli.

Tangu kifo chake mnamo tarehe 17 Machi, kiongozi mpya Samia Hassan ameashiria mabadiliko ya sera kwa kuteua timu ya ushauri juu ya jinsi ya kukabiliana na janga hilo na kuanza mchakato wa kupata chanjo. Serikali bado haijatoa takwimu halisi za ugonjwa huo.

"Uchapishaji wa data hizo zitakuwa ni sharti la kusonga mbele," alisema Jens Reinke, mwakilishi wa IMF nchini Tanzania. "Ili kuhalalisha ufadhili wa dharura katika muktadha wa janga hilo, unahitaji kuchapisha data muhimu za afya ya umma."

===

Zaidi Soma:
Tanzania needs to publish data on the spread of Covid-19 before getting approval for a $574 million emergency loan from the International Monetary Fund, the Washington-based lender said.

Reporting numbers on coronavirus infections and deaths would be an about turn for the government that hasn’t done so since May last year when then-President John Magufuli’s administration played down the threat from the disease. Since his death in March, new leader Samia Hassan has signaled a shift in policy by appointing an advisory team on how to tackle the pandemic and started a process to procure vaccines. The government hasn’t yet given numbers on the disease, though.

“Publication of such data would be a precondition of moving ahead,” said Jens Reinke, the IMF’s resident representative in Tanzania. “In order to justify emergency financing in the context of the pandemic, you need to publish relevant public-health data.”

The government first asked the IMF for a loan under its Rapid Credit Facility in March last year, he said by phone. Negotiations never progressed, and the government said last month it had revived the request.

Tanzania could access as much as $574 million given its current IMF quota, or double that if the lender’s board approves a proposed new general allocation of special drawing rights to further help countries deal with the consequences of the pandemic.

The government will make a statement on its coronavirus response once it has considered the advice from its Covid-19 technical committee, chief spokesman Gerson Msigwa said by phone.

Vulnerable Sectors​

The nation doesn’t face an immediate balance of payments crisis, so Hassan’s administration would seek to justify the request on the basis of needing to finance its response to the impact of Covid-19. Early talks have started, said Reinke.

“We are exploring ways for the financing to go toward the government response to the public-health crisis, and maybe also to support vulnerable sectors like tourism,” he said, adding that the previous government had neglected investment in other sectors like health, education, and sanitation. “The government is reaching out to not only just us to kick-start investment in that.”

Source: Bloomberg
 
Ile Report ifanyiwe KAZI kusita sita kunaturudisha KULE KULE.

MPUNGA UINGIE hizo fedha zilipe madeni ya Wastaafu na Mifuko ya Jamii

Mmekomba kule NSSF zakwetu bila huruma
 
Tumefinywa kidogo ngoja tuone tutakavyorukaa😂😂😂😂😂

Na pesa tunaitaka! Elimu yetu haipo sawa Na mfumo dume wa Mkoloni wa ulimwengu.

Hatufundishwi jinsi ya kumjibu Mzungu na kuachana Na ujinga wake.

Leo hii China hawataki kutoa ushirikiano kwa W.H.O lkn hatusikii lawama nyingi kama tunavyolalamikiwa sisi.
 
Tumefinywa kidogo ngoja tuone tutakavyorukaa😂😂😂😂😂

Na pesa tunaitaka! Elimu yetu haipo sawa Na mfumo dume wa Mkoloni wa ulimwengu...
Kwanini takwimu hizi zinafanywa siri?

Kwamba zinafanywa siri ni kutotutendea haki sisi wenyewe kama waathirika nambari 1 wala hata si kwa sababu ya incentive yoyote.
 
Ukikubali kuolewa sharti ulale bila chupi!!!!!!. Sisi tuna Elimu lkn hatuna akili. Madini, gesi maziwa utalii lkn bado sisi ni omba omba. W.H.O hawawezi kumvimbia kifua china kwa sababu china hatembezi bakuli.
Extremely good! Umenielewa sana mkuu
 
Kwanini takwimu hizi zinafanywa siri?

Kwamba zinafanywa siri ni kutotutendea haki sisi wenyewe kama waathirika nambari 1 wala hata si kwa sababu ya incentive yoyote.
Hakuna Siri tena . Ripoti ianikwe au ndiyo tulikopi takwimu za Kenya kweli watu walivyobashiri?
 
Emergency loan!

Kwani inatolewa tolewa tu. Yaombwa tena hata kwa magoti hupati. Kuipata hadi kukidhi vigezo. Vigezo vilivyomo ni pamoja na kuwatendea haki raia wako kwa kutoa takwimu.

Wajameni - ugumu uko wapi hapo? Nani anayezuia hizi takwimu kutoka? Mwendazake sasa hivi si hayupo?

Mzuia takwimu muda wake wa kutumbuliwa ni sasa.
 
Mimi naona tuwape takwimu ya bupiji ngapi na fukiza plus ngapi na malimau, tangawizi,pilipili kichaa na vitunguu vilivyotumika mpaka sasa na gharama za kujenga mashine ya nyungu ndio watupatie kama msaada, ni vihela vichache tu hamna haja ya kukopeshana, au nasema uongo ndugu zangu ? 🐒🤸‍♂️🤣
 
Mama tuvushe watanzania kwani hatupo kisiwa,Tumelia sana kwa maamuzi ya utawala wa masikini Jeuri. Usiturudishe Misri, enough is enough tuunganishe na ulimwengu. mama our trust is in you...Regards.
 
Ukikubali kuolewa sharti ulale bila chupi!!!!!!. Sisi tuna Elimu lkn hatuna akili. Madini, gesi maziwa utalii lkn bado sisi ni omba omba. W.H.O hawawezi kumvimbia kifua china kwa sababu china hatembezi bakuli.
Nimekuwa nikiongea siku zote ukombozi wa kweli ni kuwa na uchumi imara , hiyo ndio heshima ya nchi , yanayobaki yote ni kelele tu, tuna zaidi ya miaka 60 ya uhuru bado akili zetu zote zinawaza misaada, yaani viongozi wetu na wachumi wetu ni kama bongo zilisha bunguliwa.
 
Nimekuwa nikiongea siku zote ukombozi wa kweli ni kuwa na uchumi imara , hiyo ndio heshima ya nchi , yanayobaki yote ni kelele tu, tuna zaidi ya miaka 60 ya uhuru bado akili zetu zote zinawaza misaada, yaani viongozi wetu na wachumi wetu ni kama bongo zilisha bunguliwa.
Nafasi yako ni ipi katika miaka 60 ya uhuru kiuchumi? Umeitendea haki?
 
Back
Top Bottom