IMF yaidhinisha ufadhili wa Dola Milioni 900 kwa Tanzania kwa ajili ya Bajeti na kukabiliana na Mabadiliko ya hali ya Hewa

IMF yaidhinisha ufadhili wa Dola Milioni 900 kwa Tanzania kwa ajili ya Bajeti na kukabiliana na Mabadiliko ya hali ya Hewa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Bodi ya Wakurugenzi ya IMF imeidhinisha Mkopo kiasi Cha $900 Milioni sawa na karibu Shilingi Trilioni 2.4 Kwa Tanzania Ili kuisaidia kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Hali ya hewa kwenye uchumi.

Aidha ieleweke kwamba Serikali inakopo kile ambacho kimeidhinishwa kwenye Bajeti,haifangi kiholela.

Aidha ieleweke kwamba Nchi inakopeshwa Kwa sababu Ina uwezo wa kulipa kulingana na uimara wa Uchumi wake. Sio Kila Nchi inapewa Mkopo.

My Take: Katika kipindi hiki Nchi inatekeleza miradi mikubwa ya Maendeleo, Tuendelee kukopa kwani mikopo inaharakisha maendeleo hususani Miradi ya kimkakati

==============

IMF Pic.jpg

Shirika la kimataifa la fedha (IMF) Alhamisi limesema bodi yake ya utendaji imeidhinisha ufadhili wa dola milioni 786.2 kwa Tanzania kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Shirika hilo la kifedha linakamilisha pia tathmini tofauti ya kuruhusu malipo ya dola milioni 149.4 kwa ajili ya msaada wa bajeti.

Mamlaka za Tanzania zina dhamira ya kuendelea kutekeleza mageuzi ya kudhibiti uthabiti wa kifedha, kuimarisha ufufuaji wa uchumi, kukuza ukuaji endelevu na shirikishi, IMF ilisema katika taarifa.

Katika miaka mitatu iliyopita, utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan ulifanya mageuzi mbalimbali ya kiuchumi kwa lengo la kurudisha ukuaji wa uchumi katika kiwango cha ukuaji wa pato la taifa la kabla ya janga la Covid wa asilimia 6 hadi asilimia 7.

Mpango wa mageuzi ya uchumi wa Tanzania bado umeendelea kuwa imara, IMF imesema, na kuongeza kuwa ukuaji wa uchumi uliongezeka mwaka 2023 baada ya kupungua mwaka 2022.

Uchumi wa Tanzania ambao unategemea utali, madini, kilimo na viwanda, umeendelea kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa yanayochochewa na kuongezeka kwa sekta ya huduma, kulingana na Benki ya Dunia.

Uchumi wa Tanzania unakadiriwa kukua kwa asilimia 5.4 mwaka huu, kutoka asilimia 5.1, waziri wa mipango na uwekezaji katika Ofisi ya Rais, Kitila Mkumbo alisema wiki iliyopita.

DW Kiswahili

PIA, SOMA:
 
Vizazi vitakuja kumkumbuka Ndugai.

Ndugai ulitimiza wajibu wako wa kupeleka neno, wajinga wakakuona kwamba wewe ndio mjinga. Damu yetu haiko tena mikononi mwako.

Samia anachotaka ni kutuweka rehani, akimaliza muda wake arudi kwao Zanzibar atuachie zigo la mavi la madeni kwa sababu hizo hela wanazokopa hakuna kinachofanyika, wanajipigia tu. Jana Shabiby amesema upigaji serikali umekua mkubwa sana, wapigaji wanerudi kwa kasi.

View: https://www.instagram.com/reel/C8ciOsbtDUH/?igsh=MTZjMDJneTh1aHhwbQ==

Lakini pia vizazi vitakuja kuwakumbuka sana wale jamaa waliotaka katiba isifuatwe mwaka 2021.
 
Kwa nini?
 
Bodi ya Wakurugenzi ya IMF imeidhinisha Mkopo kiasi Cha $900 Milioni sawa na karibu Shilingi Trilioni 2.4 Kwa Tanzania Ili kuisaidia kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Hali ya hewa kwenye uchumi.

View: https://twitter.com/VOASwahili/status/1803984456912699644?t=Jfoj2_ImnW7OmqY-6gYGOA&s=09

My Take
Tuendelee kukopa ila Kwa Ajili ya Miradi ya kimkakati

Mikopo hiyo sio poa kuishadadia hela zinatumbukia kwenye mifuko ya mwigulu akivimbiwa ananua ihefu sasa tunasikia amenunua pamba jiji!
 
Unazungumzia vizazi vya 2100 huko kipindi hicho Chura kashajipumzikia zake zamani sana labda watakulaumu Wewe Babu yao
Hata Sasa Nchi inalipa mikopo ya kina Nyerere,ndio utaratibu maana maisha ya kesho huandaliwa Sasa hivi
 
Kwa nini?
Ndugai alionya hii nchi ipo siku itapigwa mnada kwa kukopa kopa hovyo hovyo. Tukamuona Ndugai hafai, tukamnanga hadi kumlazimisha ajiuzulu, akajiuzulu mwaka 2022, deni lilikua trilioni 72, leo miaka 2 mbele deni liko trilioni 92.

Wale jamaa wa katiba ipindishwe walijua kwamba hapa tutaingiza hii nchi matatizoni, watu wakawaona ni wajinga, sasa ukweli uko wazi, ukweli umejidhihirisha mapema sana.
 
Serikali yetu inakopa sisi wanachi pia moto uwe chini woga wa nini - wapi kausha damu ijumaa ishafika - deni halijawahi kufunga mtu.
 
Ndugai alionya hii nchi ipo siku itapigwa mnada kwa kukopa kopa hovyo hovyo. Tukamuona Ndugai hafai, tukamnanga hadi kumlazimisha ajiuzulu, akajiuzulu mwaka 2022, deni lilikua trilioni 72, leo miaka 2 mbele deni liko trilioni 92.

Wale jamaa wa katiba ipindishwe walijua kwamba hapa tutaingiza hii nchi matatizoni, watu wakawaona ni wajinga, sasa ukweli uko wazi, ukweli umejidhihirisha mapema sana.
Nchi gani imewahi pigwa Mnada kisa mikopo? Alikutajia?
 
VoA wameandika Ufadhili, wewe umeandika mkopo, know the difference.
Ila mwanzo waliposema ishu za kuuza bahari kwenye mkopo wa korea walipingwa. Ila mkuu hakuna cha bure siamini kuhusu ufadhili maana hata wao wanayo matatizo
 
Back
Top Bottom