IMF yaisamehe Tanzania deni la Tsh. Bilioni 33 kwa ajili ya Corona

Hongereni mabeberu,
Ndio najua leo kuwa uchumi wetu sio imara mpaka tumefikia hatua ya kukopa kwa mabeberu ili kuuimarisha
 
Kama sijakosea, uganda walipewa zaidi ya dola mil. 400, kenya walipewa zaidi ya dola mil. 700, sisi tumeishia kupata pesa ya nyanya..
 
Za Corona ipi? Tanzania hakuna Corona
Ukisoma vizuri utaelewa kuwa sio mkopo ila ni nafuu ya deni ili tuweze kutumia nafuu hiyo kutibu majeraha ya corona. Ni sawa na mtu aliyekuwa anakudai 1,000,000 kwa makubaliano uwe unalipa 100,000 kila mwezi, lakini baada ya kupata majanga anaamua kukupa nafuu umlipe 80,000 ili 20,000 inayobaki uweze kutibu majeraha ya majanga.

Ukumbuke hili ndilo rais alisema na sio kuturundikia madeni mengine eti kisa corona.

Na hii nafuu imetolewa kutibu majeraha yaliyoachwa na corona kwa maana corona imeondoka.
 
Wamesamehe au wameahirisha kulipa?
 
Kama sijakosea, uganda walipewa zaidi ya dola mil. 400, kenya walipewa zaidi ya dola mil. 700, sisi tumeishia kupata pesa ya nyanya..
Elewa kwanza maana ya credit relief. Uganda na Kenya walikopeshwa. Sisi hatujakopeshwa bali tumepewa nafuu ya mkopo uliopo IMF ambao tunalipa kila mwezi. Tofautisha kati ya kukopeshwa na kupunguziwa mkopo.
 
Ni furaha kwa Nchi sasa,baada ya Tanzania kupambana na Ugonjwa wa COVID-19 yenyewe bila kuomba msaada wowote kwenye Bank ya Dunia, Neema hii ni muhimu kwetu,wamesema wanataka Uchumi uimarike baada ya Corona kupungua kwa Kiwango kikubwa hapa Nchini.

TANZANIA OYEEEEEEEEEEEE,VIVA RAIS MAGUFULI
View attachment 1474784
 
Hahaha..rekebisha mkuu.
 
Mkiwa na shida ya dola zao mnawaita wahisani au wabia wa maendeleo, wakiwakemea kwa ujuba wenu mnawaita mabeberu.
 
Sasa kwa akili yako ulifikiri kwa vile umeona barua kwa kigogo basi hawatapata mikopo?
Tz hakuna korona, izo pesa za nini?
Maambukizi hakuna mkopo wa nini au mnatafuta hela ya kampeni?
Si wanasema corona imeisha sasa wapewe nyingi ili iweje?Wacha wapewe wanachostahili ndio watajifunza kuwa wakweli.
Mkuu ikiwa hata kama nchi haina corona kama north Korea tambua kuwa kuna athari za moja kwa moja katika uchumi wa nchi husika,hebu fikiria kuwa kwa sasa korona haipo nchini mwetu lakini kwa wenzetu ipo hivyo athari zake lazima na sisi tuzihisi,hebu fuatilia trend ya ujaji wa watalii,hapa utajua kuwa tumeathirika na huu ugonjwa na tunahitaji pesa ya kuboost uchumi wetu.

Lakini pia hata wee unayehoji kuwa korona imesha sasa hizo pesa za nini,naimani kwa namna moja korona itakuwa umekuathiri mfano mzunguko wa biashara umedumaa ikilinganishwa na hapo kabla ya ugonjwa,vile vile hii pesa itasaidia hata wewe unayeonekana kuhoji kwa kutanguliza upinzani mbele kuliko masrahi ya nchi

Bianfsi nawapongeza IMF kwa hii huduma yao maana hizi pesa zitasaidia kuboost secta zilizokuwa zimeathiriwa moja kuwa moja na corona.

Mungu ni mwema simu zote.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Mtu akiwa anakudai laki tatu then siku ya siku kutokana na uhohe hahe wako akaona huruma na kukuambia kuwa badala ya kunilipa laki tatu nilipe laki moja tu hiyo nyingine tumia ikusaidie kwenye matatizo yako,unaenda ukipiga kifua kuwa wewe ni mshindi?
 
Akiiona yule bwana mwenye domo kubwa anayependa kubwabwaja mitandaon lazima ajikijolee,yule sijui yuko ubeligiji sio Poland .Mimi sijui,labda waumini wake

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Huu siyo mkopo, ni kusamehe Deni na kupunguziwa makali ya kulipa Deni ndugu! Tangu mwanzo rais wetu aliwaambia Kama kweli wanna Nia nzuri, kipindi Cha corona ni Cha kusamehe madeni na sio kutuongezea kwa kutukopesha! IMF imeelewa na kutii!
Kweli rais wetu ni kiongozi wa malaika yaani hata IMF wanatii amri zake??? Hahahaha
 
Mtu akiwa anakudai laki tatu then siku ya siku kutokana na uhohe hahe wako akaona huruma na kukuambia kuwa badala ya kunilipa laki tatu nilipe laki moja tu hiyo nyingine tumia ikusaidie kwenye matatizo yako,unaenda ukipiga kifua kuwa wewe ni mshindi?
Nani kataja mshindi hapa? Nikuulize pia, ukiwa unanidai alafu tena unataka kutumia mwanya wa matatizo kunishawishi niongeze mkopo ili mwisho wa siku uchukue shamba langu, nikakataa kukopa tena kwako nakuwa sio mjanja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…