IMF yatoa orodha ya nchi 15 zenye uchumi mkubwa Afrika. Tanzania yashika namba 9 ikiwa na uchumi wa Dola Bilioni 80

Nchi 4 kati ya hizo 10 ndio sielewe uchumi wao unapandishwa na kitu gani.
Nchi hizo ni Kenya,Ghana,Ivory Coast na Morocco
 
Ghana:
GDP $76.7bil. GDP per Capita $2,300
Tanzania:
GDP $85bil. GDP per Capita $1,400
Sasa tumewapita kwa kigezo kipi?
Sisi tulitakiwa kuwa na GDP mara mbili ya hii 85$ billion kwa watu hawa hawa millioni 60 ili angalau tuwe kwenye Per Capita ya 2800$.
Tupo nyuma sanaaaaaa
 
Ghana:
GDP $76.7bil. GDP per Capita $2,300
Tanzania:
GDP $85bil. GDP per Capita $1,400
Sasa tumewapita kwa kigezo kipi?
Babuuu, hapo huoni? Au hesabu zinakusumbua?

Uchumi unapimwa kwa GDP total siyo utajiri wa mtu mmoja mmoja.

Ukichukua Tanzania hiyo Billioni 85 gawanya kwa 1400 midomo millioni zaidi ya 60. Obviously Midomo hiyo ni mingi zaidi ya Ghana.

Fanya hesabu hiyo hiyo utaona midomo Yao michache. Sisi midomo mingi.
 
Nchi 4 kati ya hizo 10 ndio sielewe uchumi wao unapandishwa na kitu gani.
Nchi hizo ni Kenya,Ghana,Ivory Coast na Morocco
Kenya

-FDI,Kenya.inachukuliwa kama gate way to EAC so biashara huanzia hapo na kupanuka kwingine
-Utalii
-Transport and Logistics
-Bussiness,Ina watu aggressive na skilled

Ghana
-Ina Dhahabu,Mafuta ,Kakao na FDI

Ivory Coast
-Cacao ndio wazalishaji Wakuu Duniani na miaka ya karibuni bei ya Kakao haikamayikii
-Biashara

Morocco
-Utalii,Second to Egypt
-Manufacturing
-Biashara
-Transport and Logistics,Wana Bandari kubwa kabisa Zenye viwango vya Kimataifa
 
Ghana:
GDP $76.7bil. GDP per Capita $2,300
Tanzania:
GDP $85bil. GDP per Capita $1,400
Sasa tumewapita kwa kigezo kipi?
Kwa hiyo wewe unaelewa kuliko IMF? Unaijua GDP lakini? Hicho ulichoweka wewe ndio Kipimo.cha Ukubwa wa Uchumi?
 
Yaani cacao peke yake ndiyo imeipandisha daraja Ivory Coast na kuipiku Tanzania yenye kila aina ya rasilimali.Lazima kuna kitu cha ziada.
Kwa Morocco watalii wanafuata nini mpaka waishinde Tanzania yenye mbuga zaidi ya 20
 
Unaijua Cacao lakini? Unajua kiwango Chao Cha uzalishaji? Pili kabla ya uhuru kwani Nchi nyingi za Afrika na Duniani zilikiwa zinategemea Madini au mazao ya shamba? Tena aina Moja.
 
Unaijua Cacao lakini? Unajua kiwango Chao Cha uzalishaji? Pili kabla ya uhuru kwani Nchi nyingi za Afrika na Duniani zilikiwa zinategemea Madini au mazao ya shamba? Tena aina Moja.
Cacao ina sifa gani.Na kwanini imedumu muda mrefu kwa Ivory Coast
 
Cacao ina sifa gani.Na kwanini imedumu muda mrefu kwa Ivory Coast
Ukiacha Kakao kama Moja ya mazao yenye bei kubwa Duniani ila Ivory Coast Ina Uongozi mzuri kwenye uchumi yaani hakuna Ufisadi wa kipuuzi na watu wanapiga kazi.
 
Mbona unasema ya 9 wakati list inaonyesha ya 10
 
Kenya pekee ndio haipo kwenye LDC. Tanzania bado tupo kwenye LDC kaangalie UN statistics za 2024
 
Ukiacha Kakao kama Moja ya mazao yenye bei kubwa Duniani ila Ivory Coast Ina Uongozi mzuri kwenye uchumi yaani hakuna Ufisadi wa kipuuzi na watu wanapiga kazi.
View attachment 2973717
Kuna kitu nimekifahamu kuhusu kupanda kwa Morocco kiuchumi.Ni kama vile Kenya inavyonyonya utalii wa Tanzania kwa kuutangaza mlima Kilimanjaro.
Morocco ni soko kubwa la dhahabu za Afrika Magharibi.Hii ni kutokana na nchi za Afrika Magharibi kufuata watalii wanaoingia Morocco kwa wingi sijui kufuata nini.
 
Kenya pekee ndio haipo kwenye LDC. Tanzania bado tupo kwenye LDC kaangalie UN statistics za 2024
Kuna vitu vinachanganya sana katika kulinganisha uchumi wa nchi na maisha ya watu.
Nashangaa sana kati ya Tanzania na Kenya.Ukienda Kenya utagundua wanaishi maisha duni sana kulinganisha na watanzania na hata miji yao haina ubora kuliko Dar es salaam.Lakini bado tu wametuzidi sana katika GDP.
 
Ogopa sana takwimu za IMF na World Bank siyo watu wazuri kwa maendeleo ya nchi masikini.
 
Reactions: Ame
Kuna mashirika makubwa mangapi na viwanda vingapi Kenya? Ila wananchi wa kawaida hawana Chao...Nchi ya kibepati ile
 
Kuna mashirika makubwa mangapi na viwanda vingapi Kenya? Ila wananchi wa kawaida hawana Chao...Nchi ya kibepati ile
Hata Tanzania ni nchi ya kibepari, kuna wananchi wengi tu hawana chao.
 
Ndio maana nikassma, Africa ni very poor, sana yani!!
Sehemu yoyote aliyepo ngozi nyeusi, ukuaji wa uchumi unakuwa uko chini; mfano mzuri tu, kuna nchi inaitwa Haiti, Guyana zipo karibu na USA lakini ni masikini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…