IMF yazipa msaada nchi 6 zilizotingwa na madeni, Tanzania imo

IMF yazipa msaada nchi 6 zilizotingwa na madeni, Tanzania imo

Baada ya kukopa ni kulipa na tunakopa Ili tu boost maendeleo na Tija ya uzalishaji
Maendeleo yapi hayo sasa kama uchumi unatupiga chenga miundombinu ndio vile tena imagine na hela za uviko ila mpaka sasa kuna shule watoto wanakaa chini kwenye vumbi maendeleo yapi hasa unayosemea na tuendako mfumoko wa bei na nchi kukosa nguvu ya uwekezaji ni jini linalotutafuna mpaka litumalize
 
Sishangai watu wakitetea ujinga wa Serikali, najua magumu wanayopitia kutafuta teuzi ila kwenye hako kamchakato jitahidi ewe chawa uwe na kipato unaweza sahulika kwenye teuzi halafu ukaishia kuwa maskini usiethaminika na uliipamba sana Serikali.
 
'Give back to society'..' Thanks giving'..
Sema tunapewa kama mkopo ili tusibweteke..
 
Nachukia neno msaada kwenye Fedha za IMF na World Bank kwa sababu fedha zao hazishushi deni la Taifa bali Impact yake ni kuliongeza deni!!!
 
Maendeleo yapi hayo sasa kama uchumi unatupiga chenga miundombinu ndio vile tena imagine na hela za uviko ila mpaka sasa kuna shule watoto wanakaa chini kwenye vumbi maendeleo yapi hasa unayosemea na tuendako mfumoko wa bei na nchi kukosa nguvu ya uwekezaji ni jini linalotutafuna mpaka litumalize
Serikali haigawi pesa
 
Hivi sisi Tanzania na Congo pamoja na madini yote tuliyonayo bado ni masikini hoehae?! Kuna kipindi tulikuwa dona kantri!!
Kwani hujawahi kuona nyumba inagraduate wa shahada za chuo ila ni masikini hatari.
Jitihada haizi kudraa!
 
Serikali haigawi pesa
Hatukatai lakini hebu sema maendeleo yapi hayo kama hatuwezi kulipa madeni mpaka tuhurumiwe na mabeberu kama hatutumii mali zetu za asili kujinufaisha kama hatuwezi kuifanya Tanzania sehemu salama na sahihi ya kuishi.

Kama hatuwezi kuondoa tabaka kati ya walio nacho na wasio nacho sasa hizi Serikali zetu zina kipi cha maana na tunakopa kama nchi zingine na huenda tumewazidi mikopo ila wao wana maendeleo sisi hatuna kinachofanyika cha maana.
 
Hatukatai lakini hebu sema maendeleo yapi hayo kama hatuwezi kulipa madeni mpka tuhurumiwe na mabeberu kama hatutumii mali zetu za asili kujinufaisha kama hatuwezi kuifanya tanzania sehemu salama na sahihi ya kuishi kama hatuwezi kuondoa tabaka kati ya walio nacho na wasio nacho sasa hizi serikali zetu zinakipi cha maana na tunakopa kama nchi zingine na huenda tumewazidi mikopo ila wao wanamaendeleo sisi hatuna kinachofanyika cha maana
Kila mwaka Serikali inalipa Madeni kati ya sh Trilioni 8-10. Sasa kuhurumiwa ni kipi huko? Kukopesha Ili ulipe Madeni wakati unadunduliza makusanyo ni jambo la kawaida.

Kwa hiyo Tanzania ya mwaka 2021 ndio iliyopo Sasa? Kazi inaendelea 👇

View: https://twitter.com/yose_hoza/status/1739910318715756705?t=90d08coqOjwtJ6ReSE7cpA&s=19
 
Kumbe na sisi bado tumo kwenye kundi la nchi maskini zaidi kwenye ukanda huu, sasa tuache mbwebwe ati uchumi wetu unakua kwa kasi sana.

Sasa huo uchumi unakuaje huku kila kukicha kiguu na njia kutembeza bakuli, au mimi ndiyo sielewi mambo ya Uchumi.
 
Back
Top Bottom