Imihigo: Mfumo wa Kuwawajibisha Viongozi wa Tanzania

Imihigo: Mfumo wa Kuwawajibisha Viongozi wa Tanzania

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Umewahi kujiuliza kwanini miradi mingi mtaani kwetukama barabara, ujenzi wa madarasa, au usambazaji wa umeme na maji inachelewa sana, alafu kiongozi aliyefeli anahamishwa tu kituo cha kazi badala ya kuwajibishwa? Kule jirani zetu Rwanda kuna mfumo wa kijasusi wa utendaji kazi unaitwa Imihigo. Huu sio mfumo wa kizamani wa makaratasi; ni mkataba wa wazi unaomfanya kiongozi asilale usiku kwa sababu kibarua chake kinakuwa kipo rehani!
Huu hapa ni mchanganuo
1. Mikataba ya Vipimo Mbele ya Kamera: Chini ya Imihigo, Wakuu wa Wilaya (DCs) au Wakurugenzi (DEDs) hawaahidi vitu vya hewa kama "tutaboresha miundombinu." Wanasaini mkataba mbele ya Rais na wananchi unaosema: "Nitajenga kilomita 12 za lami Ilala, nitaunganisha umeme nyumba 4,000, na kupunguza vifo vya uzazi kwa 15% kabla ya Juni 30." Ukifeli, unatumbuliwa hadharani, hakuna dharura ya kuhamishwa kituo kingine.

2. Kunyoosha TARURA na TANROADS Wetu: Tukiingiza mfumo huu Tanzania, kusingizia wakandarasi au kuchelewa kwa fedha za wizarani itakuwa mwisho. Kama mkataba wa mkurugenzi unasema mifereji ya dharura ya kuzuia mafuriko imalizike kabla ya masika, atalazimika kulala site kuhakikisha kazi inafanyika, la sivyo anafungasha virago vyake asubuhi.

3. Kuziba Mianya ya Mapato ya Ndani: Mara nyingi tunasikia mashine za POS za halmashauri zimeharibika au zimeingiliwa na "virusi" ili watu wapige pesa za ndani. Chini ya Imihigo, wakuu wa wilaya, mikoa n.k na wakurugenzi mkataba wao unawapima kwa asilimia ya makusanyo. Ili kulinda ugali wao, watapambana wenyewe usiku na mchana kudhibiti mafisadi wanaovujisha mapato ya serikali.

4. Uhaba wa Madawati na Dawa: Hospitali kukosa dawa za msingi au wanafunzi kukaa chini kwenye vumbi itakuwa ni historia. Kiongozi wa wilaya atajua kabisa kuwa kamati huru ya ukaguzi itakuja kukagua idadi ya madawati na uwepo wa dawa i. Hii inamfanya kiongozi kuwa mtatuzi wa matatizo (proactive) badala ya kusubiri ziara za viongozi wakuu ndio ashtuke.

Ukweli Mchungu:

Mfumo wetu wa sasa wa kujitathmini kiutendaji (OPRAS) umekuwa wa siri na wa mkataba wa makaratasi ya ndani ya faili yanayojaa vumbi maofisini. Tukihama huko na kuja kwenye mikataba ya wazi yenye vipimo vya namba inayowekwa hadharani mbele ya wananchi, viongozi wetu mtaani wataacha kufanya siasa kwenye miradi na wataanza kuheshimu jasho na kodi za watanzania.
Maendeleo ya nchi hayaji kwa hotuba ndefu zenye maneno matamu; yanakuja kwa kuweka mifumo thabiti inayowajibisha watu kwa matokeo yanayoonekana kwa macho. Imihigo ni mfano hai wa Kiafrika unaothibitisha kuwa nidhamu ya kazi ikisimamiwa kwa namba, mtaani kunanyooka!
 
CCM hawataki wanajua wengi wataachishwa kazi na kukosa ulaji.

CCM kumejaa wazembe wezi waongo wababaishaji matapeli na majitu ya hovyo ya kila namna.

Magu alifanya hivyo CCM wenzie ndio wa kwanza kumchukia.

Wale waliokuwa wanatumbuliwa na Magu kwa uzembe wizi na ubadhirifu ni CCM wenzake.

Hii nchi siku CCM ikitoka madarakani ndio mwanzo wa kunyooka kwake.
 
Back
Top Bottom