Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Tume ya Warioba imebeza na kupuuzia kurudisha mfumo wa Majimbo ikidai itajenga ukanda na ubaguzi. Halafu "magenius wetu" hawa wakaamua kupendekeza kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar in fact wameunda majimbo mawili - moja kubwa sana litaitwa Tanganyika na jingine litaitwa Zanzibar. Je hakutakuwa na hisia ya ukanda (Sisi Watanganyika, na sisi Wazanzibari) au ubaguzi "Hawa siyo wenzetu"?
Hivyo madai kuwa wamekataa majimbo kiuhalisia si ya kweli kwani kwa kuunda nchi inayoundwa na "States" mbili kimsingi wametengeneza kile walichokikataa. Tatizo ni kuwa - kama nilivyosema hapo juu - Jimbo moja litakuwa kubwa sana kuliko jingine na matokeo yake litaendelea kujiona kuwa lina nguvu zaidi. Ni sawasawa na kuwa na California na Texas halafu ukazipair na Rhode Island!
Vinginevyo tusipoangalia miaka hamsini ya majaribio ya serikali tatu tutajikuta tunavutwa kurudi kwenye serikali moja!
Njia pekee kama wameamua kuja na majimbo ni kuigawa Tanganyika katika majimbo mengine ili angalau kutengeneza equilibrium ya utawala vinginevyo kama nilivyosema kwenye ile posti nyingine Tanganyika itakuwa na nguvu mno kiasi kwamba hakutakuwa na jinsi isipokuwa Zanzibar kujiondoa.
Upande mwingine kuunda serikali moja ya kitaifa - na siyo tatu au mbili ndio njia pekee ya kuimarisha Muungano.