In Fact: Kwa Kupendekeza Tanganyika Tume ya Warioba Imependekeza Majimbo!

In Fact: Kwa Kupendekeza Tanganyika Tume ya Warioba Imependekeza Majimbo!

si tunaitwa Tanzania Bara, tatizo liko wapi? Shida yako hasa ni nini? ni jina Tanganyika tu? au ni lazima tuitwe Tanganyika ndio uridhike? tatizo liko hapo? au ni mimi labda sikuelewi? embu nisaidie kwa mara ya mwisho kukuelewa kama ukiweza!

Tanzania bara manake nini?
 
aise we jamaa wa ajabu sana, nimekuuliza neno zima "Tanzania bara " sijaligawa

Pouwa basi tuishie hapo labda mimi ndio mgumu kuelewa! kwa maana nijuavyo mimi kama mtu anafamu Kiswahili Tanzania Bara linajieleza!
 
Pouwa basi tuishie hapo labda mimi ndio mgumu kuelewa! kwa maana nijuavyo mimi kama mtu anafamu Kiswahili Tanzania Bara linajieleza!

yaonekana hujajitambua bado,na kama hujitambui ina maana hujakomboka bado. na waswas hata jina lako huelewi maana yake nini
 
Una maanisha nini? maana ya neno Bara au vipi, fafanua kama ukiweza!
Tanzania bara imetokana na muungano.......Tanzania visiwani umeisikia mara ngapi katka maisha yako..........hata rasimu inatamka wazi kwenye ibara ya kwanza

''1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.''

baada yapo mwendo wa Tanzania bara kwenda lakini upande wa pili Zanibar na wala sio Tanzania Visiwani

sasa kinachowafanya waogope kuitaja Tanganyika nini.....
 
Tanzania yenye serikali moja ndiyo itakuwa suluhisho la kudumuisha umoja wetu, utaifa wetu na maendeleo ambayo tunayataka

Hili ndilo wasilotaka wazanzibari.......nchi yao kumezwa katika kivuli cha serikali moja!
 
Mifano iko Mingi ya Muungano wa nchi ambyao imeua jina moja wa wanachama kwa mfano,

Kwa nini jina liwe Ishu? Jina linabadilisha nini? tungekuwa tunaongelea faida na hasara

Sijaona mifano yako. Umesema iko mingi?

Na miungano hiyo iliposambaratika Nchi hizo zilirudi kutumia majina yao ya zamani au walibuni majina mepya?

Unayo mifano ya hii pia?
 
Hili ndilo wasilotaka wazanzibari.......nchi yao kumezwa katika kivuli cha serikali moja!

Hakuna cha wazanzibar kumezwa na serikali moja maana wote tutakuwa ni watanzania wenye taifa lenye umoja, upendo, ushirikiano, na mshikamano katika kulinda na kutetea maliasili zetu.Hatutakuwa tena na kulilia kuitwa mimi mzanzibar au mpemba au mtanganyika.

Tutakuwa na uhuru wa kuishi mahali popote Tanzania bara au visiwani bila kukiuka sheria za nchi.Wapemba,Wazanzibar, Wanamtwara, Wanatabora, Wanadodoma etc wote tutakuwa kitu kimoja na kile tunachopata katika taifa letu tutaweza kushare kwa equity
 
Jamani mimi nilianza kubishana na huyu jamaa Kijakazi, niklaona kweli ipo kazi na si Kijikazi kumwelewesha. Mgumu kweli kama chuma cha pua. Eti mara Tanganyika jina la kikoloni, mara Tanzania Bara ndo jina letu mara jina siyo issue. Bora mmemuona alivyo mgumu. Tanganyika ndo tunataka kama nao wanataka Zanzibar
 
NINAFURAHISHWA:hata CCM ambao sera ya chama chao ni serikali mbili wameifurahia Katiba hii.NAPATA HOFU PIA:ISIJE IKAWA RASIMU NI NJEMA KULIKO KATIBA YENYEWE MAANA WAKATI MABARAZA YAKIIJADILI Babu wa SAMUNGE ataibuka na mpya,freemasons watazidi kutangazwa wakati hawajitangazi,waandishi mahiri kukobolewa, njaa kubwa sehemu Fulani,ufufuo wa misukule na habari tete kama hizo ukiamka washaichakachua kabrasha lote na kilichopo ni KATIBA MBAYA KULIKO RASIMU YAKE NA KULIKO KATIBA YA 1977!kwa hiyo?Mzalendo kaa macho!
 
Hakuna cha wazanzibar kumezwa na serikali moja maana wote tutakuwa ni watanzania wenye taifa lenye umoja, upendo, ushirikiano, na mshikamano katika kulinda na kutetea maliasili zetu.Hatutakuwa tena na kulilia kuitwa mimi mzanzibar au mpemba au mtanganyika.

Tutakuwa na uhuru wa kuishi mahali popote Tanzania bara au visiwani bila kukiuka sheria za nchi.Wapemba,Wazanzibar, Wanamtwara, Wanatabora, Wanadodoma etc wote tutakuwa kitu kimoja na kile tunachopata katika taifa letu tutaweza kushare kwa equity

Hicho kitu hakiwezekani!
Unashindwa kuelewa kitu kimoja Zanzibar ni Nchi ya zamani sana kuliko Tanzania Bara, tayari wana Utamaduni wao ambao ni tofauti na wetu, wana namna yao ya kuishi na kufanya mambo na imekuwa hivyo kwa miaka mingi sana, hivyo hawawezi kukubali kusalimisha yote hayo kwa ajili ya Muungano, hilo linapaswa kueleweka, na nafikiri akina Mlm Nyerere walilielewa hilo, hivyo basi njia pekee ya Tanzania Bara kuungana na Zanzibar ni kwaZanzibar kubakiza baadhi ya uhuru wao kwa kiingereza wanaiita semi autonomous nafikiri, kama ulivyo Muungano wa England, Scotland, Ireland!

Wao pia walishindwa kuungana moja kwa moja kwa sababu kila nchi ilikuwa na utamaduni wake na hawakuwa tayari kusalimisha kila kitu chao kwa ajili ya Muungano, sasa England ambaye yeye ndiye mkubwa akaamua kujitolea kila kitu chake kwa ajili ya Wadogo akina Scotland na Ireland, na ndio maana Scotland wana mawaziri wao, wana Bunge lao lkn England hawana, Bali Engalnd kuna Serikali kuu tu yaani ya Muungano, lkn hakuna Serikali ya England, yaani hakuna tofauti na sisi, ukichukua sisi ni wakubwa sana (TZb) ukilinganisha Zanzibar hivyo tunaweza kusalimisha kila kitu chetu kwa ajili ya Muungano na Zanzibar kwa kuwa ni wadogo (2,600 km2) basi inabidi tuwakubalia kama walivyo kwa maana hatuna cha kupoteza, angalia huu uwiano;

Tanzania Bara eneo kilometa za Mraba zaidi ya Laki tisa na arobaini elfu (945, 000)
Watu; zaidi ya 40 milioni.

Zanzibar; Eneo kilometa za Mraba elfu mbili na mia tano (2,500)
Watu; Chini ya milioni moja!

Hivyo sisi tuna nini cha kudai hapo? hivi kweli tunaweza kusema tunadhulumiwa na Zanzibar? Nafikiri ndio iliyokuwa hoja ya waliotuunganisha hapo mwanzo (sina uhakika)
, hivyo ni aidha hivyo au Muungano uvunjwe lkn Wazanzibari hawawezi kukubali kusalimisha kila kitu chao kwa ajili ya Muungano, ila sisi tunaweza na mpaka sasa hivi tumeweza hakuna tulichopungukiwa!
 
JAMHURI YA TANGANYIKA. Kijakazi waacheni waunguja na wapemba...
" WAPUMUWE ".
 
Hicho kitu hakiwezekani!
Unashindwa kuelewa kitu kimoja Zanzibar ni Nchi ya zamani sana kuliko Tanzania Bara,

Hapo ndipo mnapojidanganya; nani kakuambia Zanzibar ni nchi ya zamani sana kuliko Tanzania bara? uzamani wa vipi? Watu wameishi Tanzania bara kabla ya kuishi Zanzibar; wakiishi na mifumo yao ya utawala tangu enzi na enzi...
 
Hapa ndipo ninapo kushangaa mwanakijiji kwa akili zako,hivi unaweza kunambia tanzania bara ilipata uhuru wake lini?
 
Hapo ndipo mnapojidanganya; nani kakuambia Zanzibar ni nchi ya zamani sana kuliko Tanzania bara? uzamani wa vipi? Watu wameishi Tanzania bara kabla ya kuishi Zanzibar; wakiishi na mifumo yao ya utawala tangu enzi na enzi...
Mkuu umekusudia tanganyika au tanzania bara?
 
Hapo ndipo mnapojidanganya; nani kakuambia Zanzibar ni nchi ya zamani sana kuliko Tanzania bara? uzamani wa vipi? Watu wameishi Tanzania bara kabla ya kuishi Zanzibar; wakiishi na mifumo yao ya utawala tangu enzi na enzi...

Kuna mwana Falsafa mmoja alisema hivi. Kizazi cha kwanza kinajenga, cha pili kinashikilia na kuendeleza na Cha Tatu kinabomoa!

Sasa sisi karibu tunafika huko, na bado tulianza na Shule zilizotaifishwa za dini tukazirudisha na sasa kila dhehebu linaruhusiwa kuwa na shule yake na kufundisha watoto wetu wanachotaka, tukaja Reli na viwanda tukaua vyote, Nyumba za Serikali tukauza zote, sasa tumehamia kwenye Muungano tutauvunja kwa maana hatuutaki, baada ya hapo tutahamia kwenye Kiswahili ndiyo last frontier Wazungu wanasema tutakiondoa na kuleta Kiingereza au Mandarin, ili kukamilisha msemo wa huyo Mwanafalsafa, hivyo mimi kwangu hii ni trailer tu ya kinachokuja mbele ya safari, lkn mwisho wa siku hatutabakiza kitu, kuna Film inaitwa when a country dies na ndio tunakoelekea, NA BADO!

Kimsingi Wazanzibar wamesema na wanasema wao hawakushirikishwa na Rais wao wa kwanza namna ya kuingia katika muungano! Ndo maana walitaka kuwepo kura ya kuamua either waendelee kuwapo ndani ya muungano or hapana! kwa kuwa kura hiyo haikuwepo basi kiu hii nayo haijawatoka zaidi ya kuja na serikali tatu! maanake ni kuwa muungano huu unapendwa na wabara ila wao ni mpaka tungepata majibu ya kura ya kuutaka au kuukataa muungano. Warioba na tume yake wamefanya shortcut badala ya kuanza na kura kwa wazanzibar.
Muafaka ilikuwa ni kuanza kukubaliana muungano au la na kisha kama ni muungano ni wa jinsi gani. Kwa hiyo kura ya maoni isingekuwa ya Zanzibar tu bali hat sisi wa bara.
 
Back
Top Bottom