In Fact: Kwa Kupendekeza Tanganyika Tume ya Warioba Imependekeza Majimbo!

In Fact: Kwa Kupendekeza Tanganyika Tume ya Warioba Imependekeza Majimbo!

Unabisha bila mantiki bola nikuache maaana hujui unataka kuongelea nini. Mwl hakuacha kuiita Tanganyika kwa sababu ya ukoloni unaoongelea na Tanzania haikuja ili kufuta Tanganyika ya mkoloni. Narudia kukuelewesha tena. Tanzania imekuja kwa sababu ya muungano na ni muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar. Sasa ukianza kuongelea mambo ya mkoloni basi Zanzibar hisiwepo kwa sababu ni kukumbuka Usultani wa Kiarabu bari tuiite Unguja na Pemba. Inaonekana wewe ni mgumu wa kuelewa. Jamani watu nisaidie kumwelewesha huyu mtu Kijakazi maana mimi sijawahi kufundisha watu wenye vichwa vigumu
 
poa poa tuachie hapo!

Ngoja nikuulize swali dogo sana hivi unajua kati ya Majina ambayo yalipendekezwa kuitwa nchi yetu na Waingereza baada ya kushinda vita yalikuwa New Maryland, Windsorland na Victoria? Je yule Waziri wa mambo ya ukoloni wa Uingereza angeamua kuiita nchi yetu hivyo pia mngekuwa leo hii mnapigania hayo majina badala ya Tanzania? Kwa maana pia badala ya Tanganyika tungekuwa tunaitwa New Maryland, Windsorland, au Victoria, Je pia ungepigania hayo Majina?

tusipoteza muda kujadili mambo ambayo hayana maana Mlm Nyerere alipoamua kuiita Nchi Tanzania badala yaTanganyika hakuwa mjinga alijua yote haya.
unaweza hata ukaiita nchi yetu X ukitaka, kwani jina linatunyima nini sisi? Na ndio maana nikakupa mfano wa Afrika Kusini hata wao walitaka kubadilisha majina kwa ajili ya mambo ya kihistoria, kwani hata kama Zanzibar wakijitenga kesho na tukabaki kuitwa Tanzania kuna tatizo gani?

Shida yangu mimi ni kwa nini Jina liwe ishu? Na ndio maana nika kwambia kama swala ni Jina lenye asili ya Nchi yetu basi ni German East Africa na sio Tanganyika, kwa maana Tanganyika nalo liliwekwa tu kama vile Tanzania, lkn jina asilia la Nchi yetu ni German East Africa!

hivi unajua hata sababu ya kubadili jina kutoka Tanganyika kwenda Tanzania?
nakuomba usiniambie kwamba Nyerere hakua mjinga kubadili jina bila kunipa sababu ya msingi itakayotufanya tuendelee kushikilia hili jina?
halaf kwa kumbukumbu nilizonazo Nyerere hakulibadilisha jina la Tanganyika, ni katika uongozi wa Mwinyi ndio jina lilibadilika,
na hivi unadhani wazanzibar ni wajinga kukomaa na jina lao toka nchi hizi zimeungana Tanganyika na Zanzibar na kuitwa Tanzania?na kama sio wao kukomaa wangepoteza identity yao .
kwa hili suala ni sawasawa na leo ujarib kubadili jina la Israel na kuiita shetan halaf uone kama hakuna umuhimu wa jina kwenye jamii.
kwa kifupi tunataka Jina letu Tanganyika
 
Mfumo wetu wa Halmashauri japo unaitwa ni "Local Government" lakini kwa kweli bado uko very centralized na unategemea serikali "kuu". Halmashauri haziko uhuru - imagine Mkurugenzi wa Halmashauri anateuliwa na Waziri Mkuu! Hakuna halmashauri ambayo iko huru from the reach of the central government as a matter of fact sidhani kama kuna halmashauri inayofanya kazi bila kutegemea TAMISEMI.

Mimi nadhani tunahitaji Evolution sio Revolution... angalieni na uelewa wa Wananchi wetu... Hivi tangu Serikali za Mitaa zianze ni miaka mingapi? Kwa nini wananchi hawajachangamkia hayo madaraka yao... Leo hii Bungeni wabunge wengi wanaongea mambo ya kwenye mabaraza ya madiwani... as if wao sio wajumbe wa hizo halmashauri... kama wabunge wenyewe bado.... is it realistic real to go to Majimbo... meaning fully independent halmashauri... real let think critically jamani.
 
Bila definitions za federation na cnfederation hapa tutakesha bure, maana inaoekana kama kwamba yote yana maana moja kwa kiswahili. Halafu tujue tume ilimaanisha ipi kati ya hizo mbili.
 
Tume imeridhia serikali 3 baada ya wananchi walio wengi kupendekeza utaratibu huo, n si CDM na CUF tu.
Kuna wana CCM wengi wasiopendezwa na misimamo isiyoeleweka toka jamaa zet wa visiwani.
Kimsingi ni rahisi kumwelewa mwana CDM kuliko hawa jamaa zetu wa visiwani.

Hata hivyo usijesahau kuwa CDM walidiriki hata kutishia kujitoa katika mchakato utayarishaji wa rasimu ya katiba.
Hatujasahau Dr Slaa kutaka Prof Baregu ajitoe katika tume ya utayarishaji wa katiba mpya!
Ni busara ya Prof Baregu kumjibu DrSlaa kuwa moyoni mwake nchi iko mbele kuliko vyama-that was patriotic.
Today we are reaping the proceeds of patriotism.

..kama wananchi wengi wamependekeza serikali 3, basi CUF na CDM, wako upande wa walio wengi.

..walichokipinga CDM ni mchakato wa kupata wajumbe wa mabaraza ya katiba. wanadai waliwasilisha malalamiko yao kwa tume ya Warioba, lakini hawakusikilizwa.

..hayo majibu ya Prof.Baregu yanaweza kutolewa na mtu yeyote yule. hata mimi naweza kusema CDM walipokuwa wanapinga mfumo mbovu wa kuchagua mabaraza ya katiba waliweka maslahi ya taifa mbele.

..kwa upande wangu, naona kwa kiasi kikubwa CDM na CUF ndiyo washindi ktk hatua hii ya kwanza kuelekea katiba mpya.
 
Mzee Mwanakijiji, nisngependa kukubaliana na Nonda juu ya observation yako.
Naelewa kuwa CHADEMA na CUF are in total dis array baada ya kutolewa rasimu ya Katiba mpya.
Hivyo basi sioni analogy ya Tanganyika na Zanzibar kuwa "majimbo" kwa maana ya majimbo ya uchaguzi kwa jinsi tunavyoyajua.
They are more than that, halafu Zanzibar ni nchi atii!!!!

Hapa tunazungumzia majimbo (provinces) na sio majimbo ya uchaguzi (constituencies)
 
sijui ni kwa nini watawala wetu wanashinikiza kuwepo kwa muungano bila kuuliza kama wenye nchi wanautaka au la!!

Kuvunjika muungano ndio mwisho wa CCM. Nnje ya muungano hamna CCM.Nnje ya muungano ni TANU na ASP.
 
Kimsingi Wazanzibar wamesema na wanasema wao hawakushirikishwa na Rais wao wa kwanza namna ya kuingia katika muungano! Ndo maana walitaka kuwepo kura ya kuamua either waendelee kuwapo ndani ya muungano or hapana! kwa kuwa kura hiyo haikuwepo basi kiu hii nayo haijawatoka zaidi ya kuja na serikali tatu! maanake ni kuwa muungano huu unapendwa na wabara ila wao ni mpaka tungepata majibu ya kura ya kuutaka au kuukataa muungano. Warioba na tume yake wamefanya shortcut badala ya kuanza na kura kwa wazanzibar.

Kutoshirikishwa Kwao kilitokana na ukweli kwamba uhuru wao haukua kamili .... nchi ya Zanzibar iliipindua serikali ya ukoloni bila ya kuwa na jeshi wala polisi wa kuulinda Uhuru huo.... Njia pekee ilikua ni kuungana na Tanganyika ili kuwepo na jeshi na Polisi wa kulinda Uhuru kutoka bara..... leo wanasema hawakushirikishwa tena kwa ushauri unaoyolewa na wale wale waliowatala safari hii wanajiita wa harakati wa kiislam ili kuficha dhamira yao ya kweli....!
 
Tume ya Warioba imebeza na kupuuzia kurudisha mfumo wa Majimbo ikidai itajenga ukanda na ubaguzi. Halafu "magenius wetu" hawa wakaamua kupendekeza kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar in fact wameunda majimbo mawili - moja kubwa sana litaitwa Tanganyika na jingine litaitwa Zanzibar. Je hakutakuwa na hisia ya ukanda (Sisi Watanganyika, na sisi Wazanzibari) au ubaguzi "Hawa siyo wenzetu"?

Hivyo madai kuwa wamekataa majimbo kiuhalisia si ya kweli kwani kwa kuunda nchi inayoundwa na "States" mbili kimsingi wametengeneza kile walichokikataa. Tatizo ni kuwa - kama nilivyosema hapo juu - Jimbo moja litakuwa kubwa sana kuliko jingine na matokeo yake litaendelea kujiona kuwa lina nguvu zaidi. Ni sawasawa na kuwa na California na Texas halafu ukazipair na Rhode Island!

Vinginevyo tusipoangalia miaka hamsini ya majaribio ya serikali tatu tutajikuta tunavutwa kurudi kwenye serikali moja!

Njia pekee kama wameamua kuja na majimbo ni kuigawa Tanganyika katika majimbo mengine ili angalau kutengeneza equilibrium ya utawala vinginevyo kama nilivyosema kwenye ile posti nyingine Tanganyika itakuwa na nguvu mno kiasi kwamba hakutakuwa na jinsi isipokuwa Zanzibar kujiondoa.

Upande mwingine kuunda serikali moja ya kitaifa - na siyo tatu au mbili ndio njia pekee ya kuimarisha Muungano.

bado mwanakijiji anatokwa na kipovu than nimegundua mtoa mada hupenda kukurupuka bila kutafuta taarifa za kweli.warioba hakusema serikali ya tanganyika amesema serikali ya tanzania bara
 
bado mwanakijiji anatokwa na kipovu than nimegundua mtoa mada hupenda kukurupuka bila kutafuta taarifa za kweli.warioba hakusema serikali ya tanganyika amesema serikali ya tanzania bara

Wengine wanasema "Potato" na wengine wanasema "Poteto"...
 
Tanganyika haitamkwi kwa sababu ni neo la Kikoloni, kwa maana nyingine Mlm Nyerere alilifuta kabisa na hakuliita kwa sababu lilianzishwa na Wakoloni na ndio maana haulisikii, kushabikia jina la Tanganyika ni sawa tu na kushabikia au kuuliza kwa nini tusiitwe German East Afrika? nikikuuliza kwa nini tusiitwe hivyo? kwa maana ndio jina asilia kabisa la Nchi yetu, kwa maana nyingine German East Afrika ndio hasa tunapaswa kulipigania kama hoja ni tu jina asili la nchi yetu!
Ndio maana wanaoelewa vizuri historia ya nchi mpamoja na hiyo tume ya Katiba wanapendelea kutumia Tanzania Bara!

Kijakazi
Mwaka 1964 nchi zilizoungana ziliitwa kwa majina yepi?

Zanzibar iliungana na nchi ipi?

Katika dunia hii wapi umesikia,umesoma au umeota ndoto kuwa muungano unaua jina la nchi wanachama wake?

Jina Tanzania lilianza kutumika lini? Jina la asili la muungano unalifahamu?

Nani alifanya "mazingombwe" ya Tanzania kuwa na "bara" mbele yake.

Mafia,Juani, Jibonde, Ukerewe ni Tanzania bara,Tanzania visiwani au Tanganyika visiwani?

Unajua vipi lilitengenezwa,lilibuniwa jina Tanzania?

Nchi zipi zilisaini mkataba wa Muungano?

Kwa nini hatukubadilisha jina Tanganyika baada ya kupata uhuru 1961?
 
Kimsingi Wazanzibar wamesema na wanasema wao hawakushirikishwa na Rais wao wa kwanza namna ya kuingia katika muungano! Ndo maana walitaka kuwepo kura ya kuamua either waendelee kuwapo ndani ya muungano or hapana! kwa kuwa kura hiyo haikuwepo basi kiu hii nayo haijawatoka zaidi ya kuja na serikali tatu! maanake ni kuwa muungano huu unapendwa na wabara ila wao ni mpaka tungepata majibu ya kura ya kuutaka au kuukataa muungano. Warioba na tume yake wamefanya shortcut badala ya kuanza na kura kwa wazanzibar.

Maisha nenda rudi ccm kamwe hawatakubali kura kupigwa kwani wanajua kura itaamua kile wasichokitaka
 
Kijakazi
Mwaka 1964 nchi zilizoungana ziliitwa kwa majina yepi?

Zanzibar iliungana na nchi ipi?

Katika dunia hii wapi umesikia,umesoma au umeota ndoto kuwa muungano unaua jina la nchi wanachama wake?

Jina Tanzania lilianza kutumika lini? Jina la asili la muungano unalifahamu?

Nani alifanya "mazingombwe" ya Tanzania kuwa na "bara" mbele yake.

Mafia,Juani, Jibonde, Ukerewe ni Tanzania bara,Tanzania visiwani au Tanganyika visiwani?

Unajua vipi lilitengenezwa,lilibuniwa jina Tanzania?

Nchi zipi zilisaini mkataba wa Muungano?

Kwa nini hatukubadilisha jina Tanganyika baada ya kupata uhuru 1961?

Mifano iko Mingi ya Muungano wa nchi ambyao imeua jina moja wa wanachama kwa mfano,

Kwa nini jina liwe Ishu? Jina linabadilisha nini? tungekuwa tunaongelea faida na hasara tunazopita kiuchumi kutokana na yaliyomo kwenye Mkataba wa Muungano sawa lkn SIYO jina! Sijawahi kusikia mimi sehemu yoyote watu wanabishania jina!

Waafrika kusini baada ya Apartheid kuisha pia walitaka kubadilisha jina Afrika Kusini (South Africa) kwa kuwa halikuwa lao bali ni la wazungu, lkn mwisho wa siku wakaja kugundua kwamba kubadilisha JINA hakutawafaidisha chochote, cha muhimu ni kuangalia Sera za kuwakomboa watu wao kiuchumi, hata sisi tunaweza kufanya hivyo, tuna mambo mengi ya kufanya ili kuboresha maisha yetu badala tu ya kubishania Jina!

Unabisha bila mantiki bola nikuache maaana hujui unataka kuongelea nini. Mwl hakuacha kuiita Tanganyika kwa sababu ya ukoloni unaoongelea na Tanzania haikuja ili kufuta Tanganyika ya mkoloni. Narudia kukuelewesha tena. Tanzania imekuja kwa sababu ya muungano na ni muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar. Sasa ukianza kuongelea mambo ya mkoloni basi Zanzibar hisiwepo kwa sababu ni kukumbuka Usultani wa Kiarabu bari tuiite Unguja na Pemba. Inaonekana wewe ni mgumu wa kuelewa. Jamani watu nisaidie kumwelewesha huyu mtu Kijakazi maana mimi sijawahi kufundisha watu wenye vichwa vigumu
Mkuu umejitahidi sana kumuelewesha huyo Kijakazi, ila naona ni mgumu sana kuelewa. Kama alifika darasani, waalimu wake walikuwa na kazi ya ziada!
 
tatizo sio nani aliyeanzisha jina la Taganyika bali maana pia ni muhimu kujiuliza ,we jiulize Tan-zan-ia (Tanganyika na zanzibar wakitumia kiunganishi cha nia)mana yake nini na Tanga-nyika(pwani ya kuingia ardhi isiyojulikana) mana yake nini?halaf tujiulize kwanini tuendelee kuwajumuisha wazanzibar ndani ya bara wakati wao tayari wanajitambua wapo tofaut na Tanganyika na ndani ya shirikisho wakiwa wanajiwakilisha wao kama wao wazanzibar?
tuache kukumbatia tusivyovielewa kisa tu alisema mtu fulani

Nakubaliana na wewe Mkuu, kuna watu huwa wanajitoa akili ama wana akili za kushikiwa kwa sababu fulani alisema. Niwaulize wale wanaoionea aibu Tanganyika, Nyerere na wenzake wakati wa harakati zao za kutafuta uhuru, walikuwa wanatafuta uhuru wa nchi gani kati ya hizi; Germany East Afrika, Tanganyika, Tanzania Bara? Na baada ya kupata uhuru ule walishangilia na kubebana kwa fahari ya uhuru wa nchi gani? Kipindi kile hawakuona aibu ya kuitwa jina hilo?
 
Mifano iko Mingi ya Muungano wa nchi ambyao imeua jina moja wa wanachama kwa mfano,

Kwa nini jina liwe Ishu? Jina linabadilisha nini? tungekuwa tunaongelea faida na hasara tunazopita kiuchumi kutokana na yaliyomo kwenye Mkataba wa Muungano sawa lkn SIYO jina! Sijawahi kusikia mimi sehemu yoyote watu wanabishania jina!

Waafrika kusini baada ya Apartheid kuisha pia walitaka kubadilisha jina Afrika Kusini (South Africa) kwa kuwa halikuwa lao bali ni la wazungu, lkn mwisho wa siku wakaja kugundua kwamba kubadilisha JINA hakutawafaidisha chochote, cha muhimu ni kuangalia Sera za kuwakomboa watu wao kiuchumi, hata sisi tunaweza kufanya hivyo, tuna mambo mengi ya kufanya ili kuboresha maisha yetu badala tu ya kubishania Jina!

hukujibu swali langu umebaki kuuliza swali lilelile la jina lina umuhimu gani?naomba nikuulize kama una mtoto? huyo mtoto umempa jina gani? au ulitoa tu jina bila sababu?

halaf usiwe na mawazo finyu eti tujadili sera za kiuchumi tu.kuna mwanafalsafa mmoja Yesu kristo alisema binadamu hutaishi kwa mkate tu.alimaanisha watu hawataishi kwajili ya mambo ya kiuchumi tu,usiwe kama mnyama anayeangalaia atakula nini tu leo wewe ni binadamu una mambo mengi ya kuangalia zaidi ya uchumi

kuna mambo mengi ya kuangalia katika katiba na sio sera za uchumi tu,bali pia na sera za kisiasa,na kijamiii na kiutamaduni ambazo zinahitaji mjadala, la sivyo kungekua hakuna umuhimu wa kua na fani tofauti bali wote tungesomea uchumi tu.

Lazima tuitengeneze Tanzania tunayoitaka na Tanganyika ni muhimu iwepo.

kama wasauzi waliridhika na hilo jina ni maamuzi yao na wanalia na kusaga meno mpaka leo kwa kutokua makini wakati walipopewa nchi kwani njia kuu zote za kiuchumi zimeshikwa na tabaka la wazungu na waafrika wengi ni maskini wa kutupwa na wasio na kazi, na yote hii ni inatokana na kudharau mambo madogomadogo ambayo ni kama tone la maji lakini linapasua mwamba baada ya muda mrefu
 
si tunaitwa Tanzania Bara, tatizo liko wapi? Shida yako hasa ni nini? ni jina Tanganyika tu? au ni lazima tuitwe Tanganyika ndio uridhike? tatizo liko hapo? au ni mimi labda sikuelewi? embu nisaidie kwa mara ya mwisho kukuelewa kama ukiweza!
 
Back
Top Bottom