In Fact: Kwa Kupendekeza Tanganyika Tume ya Warioba Imependekeza Majimbo!

Mwanakijiji stretch your brain a bit more! Majimbo tunayoyataka ni zaidi ya Tanganyika na Zanzibar
 
Tume ya Warioba imebeza na kupuuzia kurudisha mfumo wa Majimbo ikidai itajenga ukanda na ubaguzi. Halafu "magenius wetu" hawa wakaamua kupendekeza kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar in fact wameunda majimbo mawili - moja kubwa sana litaitwa Tanganyika na jingine litaitwa Zanzibar. Je hakutakuwa na hisia ya ukanda (Sisi Watanganyika, na sisi Wazanzibari) au ubaguzi "Hawa siyo wenzetu"?

Hivyo madai kuwa wamekataa majimbo kiuhalisia si ya kweli kwani kwa kuunda nchi inayoundwa na "States" mbili kimsingi wametengeneza kile walichokikataa. Tatizo ni kuwa - kama nilivyosema hapo juu - Jimbo moja litakuwa kubwa sana kuliko jingine na matokeo yake litaendelea kujiona kuwa lina nguvu zaidi. Ni sawasawa na kuwa na California na Texas halafu ukazipair na Rhode Island!

Vinginevyo tusipoangalia miaka hamsini ya majaribio ya serikali tatu tutajikuta tunavutwa kurudi kwenye serikali moja!

Njia pekee kama wameamua kuja na majimbo ni kuigawa Tanganyika katika majimbo mengine ili angalau kutengeneza equilibrium ya utawala vinginevyo kama nilivyosema kwenye ile posti nyingine Tanganyika itakuwa na nguvu mno kiasi kwamba hakutakuwa na jinsi isipokuwa Zanzibar kujiondoa.

Upande mwingine kuunda serikali moja ya kitaifa - na siyo tatu au mbili ndio njia pekee ya kuimarisha Muungano.

Vilaza mko wengi sana kwenye RASIMU HII YA KATIBA na Watanzania tusipokuwa makini na watu kama wewe nchi itaangamia. Nadhani hata maana ya serikali za amjimbo.
 
Tume ya Warioba imebeza na kupuuzia kurudisha mfumo wa Majimbo ikidai itajenga ukanda na ubaguzi. Halafu "magenius wetu" hawa wakaamua kupendekeza kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar in fact wameunda majimbo mawili - moja kubwa sana litaitwa Tanganyika na jingine litaitwa Zanzibar. Je hakutakuwa na hisia ya ukanda (Sisi Watanganyika, na sisi Wazanzibari) au ubaguzi "Hawa siyo wenzetu"?

Hivyo madai kuwa wamekataa majimbo kiuhalisia si ya kweli kwani kwa kuunda nchi inayoundwa na "States" mbili kimsingi wametengeneza kile walichokikataa. Tatizo ni kuwa - kama nilivyosema hapo juu - Jimbo moja litakuwa kubwa sana kuliko jingine na matokeo yake litaendelea kujiona kuwa lina nguvu zaidi. Ni sawasawa na kuwa na California na Texas halafu ukazipair na Rhode Island!

Vinginevyo tusipoangalia miaka hamsini ya majaribio ya serikali tatu tutajikuta tunavutwa kurudi kwenye serikali moja!

Njia pekee kama wameamua kuja na majimbo ni kuigawa Tanganyika katika majimbo mengine ili angalau kutengeneza equilibrium ya utawala vinginevyo kama nilivyosema kwenye ile posti nyingine Tanganyika itakuwa na nguvu mno kiasi kwamba hakutakuwa na jinsi isipokuwa Zanzibar kujiondoa.

Upande mwingine kuunda serikali moja ya kitaifa - na siyo tatu au mbili ndio njia pekee ya kuimarisha Muungano.

hii ni kweli kwani kiongozi mkuu wa tanganyika na zanzibar watakuwa ni MAGAVANA. Gavana huwa anaongoza jimbo period
 
Despite the fact kwamba CCM kwa muda sasa wamejigamba kutekeleza sera ya Decentralization by Devolution(D by D) kwa kupeleka madaraka kwenye halmshauri na kuakisi sera ya majimbo UKWELI ni kwamba halmashauri hizi zinafanya kazi chini ya directives za wizara ya tamisemi na hazina mamlaka ya kupanga na kuamua juu ya mgawanyo wa rasilimali katika ngazi husika.

The only big difference kati ya mfumo wa majimbo na halmashauri ni juu ya mamlaka ya umiliki na uendeshaji wa rasilimali, maamuzi na utoaji wa huduma ndani ya maeneo husika.There is a big delay katika utoaji wa huduma coz mambo mengi yako centralized na hata Wakurugenzi katika mamlaka hizi wako dependent kifikra.

Unachotakiwa kuelewa ni kwamba D by D haitakiwi kufanyika kwa mwaka mmoja, unachotakiwa ni kuangalia kwamba year by year je... madaraka na mamlaka kweli yanapelekwa kwenye halimashauri? Mimi naelewa wanafanya hivyo...
 
Tume ya Warioba imebeza na kupuuzia kurudisha mfumo wa Majimbo ikidai itajenga ukanda na ubaguzi. Halafu "magenius wetu" hawa wakaamua kupendekeza kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar in fact wameunda majimbo mawili - moja kubwa sana litaitwa Tanganyika na jingine litaitwa Zanzibar. Je hakutakuwa na hisia ya ukanda (Sisi Watanganyika, na sisi Wazanzibari) au ubaguzi "Hawa siyo wenzetu"?

Hivyo madai kuwa wamekataa majimbo kiuhalisia si ya kweli kwani kwa kuunda nchi inayoundwa na "States" mbili kimsingi wametengeneza kile walichokikataa. Tatizo ni kuwa - kama nilivyosema hapo juu - Jimbo moja litakuwa kubwa sana kuliko jingine na matokeo yake litaendelea kujiona kuwa lina nguvu zaidi. Ni sawasawa na kuwa na California na Texas halafu ukazipair na Rhode Island!

Vinginevyo tusipoangalia miaka hamsini ya majaribio ya serikali tatu tutajikuta tunavutwa kurudi kwenye serikali moja!

Njia pekee kama wameamua kuja na majimbo ni kuigawa Tanganyika katika majimbo mengine ili angalau kutengeneza equilibrium ya utawala vinginevyo kama nilivyosema kwenye ile posti nyingine Tanganyika itakuwa na nguvu mno kiasi kwamba hakutakuwa na jinsi isipokuwa Zanzibar kujiondoa.

Upande mwingine kuunda serikali moja ya kitaifa - na siyo tatu au mbili ndio njia pekee ya kuimarisha Muungano.

Nafikiri utakuwa ni msomaji mzuri wa historia za nchi mbali mbali Duniani, mara nyingi Mfumo wa Majimbo hauanzishwi tu kwa sababu fulani anapenda uanzishwe bali unaanzishwa kwa sababu ya Mazingira ambayo hayazuiliki, kwa Mfano Marekani wana majimbo sio kwa sababu eti walikaa wakafikiri kwamba Majimbo yatawaletea maendeleo hivyo wakayaanzisha, HAPANA!

Marekani kuna Majimbo kwa sababu, hayo Majimbo yote yalikuwa ni nchi zilizojitegemea na Sheria zao na mfumo wao wa kisiasa, sasa walivyotaka kuungana hizo nchi zikatoa masharti kwamba kama mnataka tuingie kwenye muungano na nyinyi ni lazima tubakize autonomy fulani, kwamba hatuko tayari kusalimisha kila kitu kwa ajili ya Muungano, sasa ili kuweza kukubaliana ndio wakaja na hayo Majimbo, na ndio maana unaona kila Jimbo lina Sheria zake!

Na nchi nyingi Duniani zenye huo mfumo ukiangalia utaona hiyo sababu, ni kama Sisi tuamue kuungana na Uganda na Burundi, kila nchi tayari ina mfumo wake hivyo kila nchi itasema sawa tunaungana lkn tunabakiza uhuru wetu wa kufanya mambo yetu kwa kiasi fulani, sasa hapo hakuna jinsi bali kutengeneza Majimbo!

Sasa kwa Upande wetu wa TZ bara hakuna hiyo haja ya kufanya Majimbo, kwa nini?
Na Zanzibar inaeleweka kwa sababu tayari walikuwa na Nchi yao na mfumo wao wa maisha hawawezi kukubali kusalimisha Uhuru wao wote na mfumo wao wa Maisha kwa ajili ya Muungano, na ndio maana nafikiri hilo waliliangalia na kuona umuhimu wake!

Hivyo TZ Bara kuanzishwa kwa Majimbo ni hoja ambayo haina Msingi hata kidogo, na kusema kwamba italeta sijui maendeleo au Uwajibikaji ni kujidanganya kulikopindukia, kama tumeshindwa kujenga Uwajibikaji kwa Mfumo huu hata kwa Majimbo au Mfumo wowote ule tutashindwa pia!

Kuna Nchi nyingi sana Duniani zina Mfumo kama wetu na zimeendelea mf. Uchina, Singapore, Korea Kusini(hapo mwanzo), Vietnam, Namibia, Botswana, n.k na kuna Nchi nyingi pia zinafwata Mfumo wa Majimbo na sasa ni chaos tupu kama India, Nigeria, Msumbiji, Ethiopia, Kongo (DRC), Angola na Angola ni mfano mzuri pamoja na kuwa na Majimbo lkn bado kila kitu kinapekwa Mji Mkuu Luanda na wananchi wanaoishi kwenye Majimbo yenye Rasilimali hawana chao, hivyo hiyo hoja haina mshiko!

Mzee Mwanakijiji, nisngependa kukubaliana na Nonda juu ya observation yako.
Naelewa kuwa CHADEMA na CUF are in total dis array baada ya kutolewa rasimu ya Katiba mpya.
Hivyo basi sioni analogy ya Tanganyika na Zanzibar kuwa "majimbo" kwa maana ya majimbo ya uchaguzi kwa jinsi tunavyoyajua.
They are more than that, halafu Zanzibar ni nchi atii!!!!
siyo majimbo ya ucaguzi ni States za kiutawala kama za USA zinazounda shirikisho
 
Tatizo ccm wana asili ya ubishi. Kisa wazo la majimbo halikuanzia kwao wakaamua kulitosa. Mbona kuna kanda katika nyanja za michezo umiss n.k? Nani aliwahi kubaguliwa huko? Hamjawahi kusikia mchaga kawa miss kanda ya ziwa.?
 
Mzee Mwanakijiji,
Niliandika mahali fulani humu kuwa wameikubali sera ya majimbo ya Chadema kwa kuunda mawili badala ya yale mengi yaliyokuwa yatakiwe na CDM.
 
Mwana Kijiji nadhani ujawaelewa vizuri hawa Tume ya Katiba, hakuna mahali wanatamka Tanganyika, badala yake kinachotamkwa ni Tanzania Bara, lakini cha ajabu wanashindwa kutamka Tanzania Visiwani. Maoni yangu ni kwamba wameamua kuizika Tanganyika kabisa. Kama ni serikali tatu basi kuwepo Seriakali ya Mapinduzi ya Zanzibar, serikali ya Tanganyika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Au waseme Tanzania Visiwani, Tanzania Bara na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Hakuna Tanzania bila kuwepo Tanganyika na Zanzibar maana neno TAN(Tanganyika)ZA(Zanzibar) NIA kama kuleta jina linalotamkwa. Kwa hiyo lazima kama wameamua kuwepo serikali tatu Tanganyika lazima itamkwe na wala si Tanzania Bara
 
Tanganyika haitamkwi kwa sababu ni neo la Kikoloni, kwa maana nyingine Mlm Nyerere alilifuta kabisa na hakuliita kwa sababu lilianzishwa na Wakoloni na ndio maana haulisikii, kushabikia jina la Tanganyika ni sawa tu na kushabikia au kuuliza kwa nini tusiitwe German East Afrika? nikikuuliza kwa nini tusiitwe hivyo? kwa maana ndio jina asilia kabisa la Nchi yetu, kwa maana nyingine German East Afrika ndio hasa tunapaswa kulipigania kama hoja ni tu jina asili la nchi yetu!
Ndio maana wanaoelewa vizuri historia ya nchi mpamoja na hiyo tume ya Katiba wanapendelea kutumia Tanzania Bara!

masopakyindi,

..kwanini unafikiri CUF na CCM r in total disarray baada ya rasimu hii kutoka?

..kubwa lililofanyika ni tume kukubali mapendekezo ya CDM na CUF kuwepo kwa mfumo wa serikali 3.

..hata tume huru ya uchaguzi ilikuwa ni moja ya mapendekezo ya CDM.
Tume imeridhia serikali 3 baada ya wananchi walio wengi kupendekeza utaratibu huo, n si CDM na CUF tu.
Kuna wana CCM wengi wasiopendezwa na misimamo isiyoeleweka toka jamaa zet wa visiwani.
Kimsingi ni rahisi kumwelewa mwana CDM kuliko hawa jamaa zetu wa visiwani.

Hata hivyo usijesahau kuwa CDM walidiriki hata kutishia kujitoa katika mchakato utayarishaji wa rasimu ya katiba.
Hatujasahau Dr Slaa kutaka Prof Baregu ajitoe katika tume ya utayarishaji wa katiba mpya!
Ni busara ya Prof Baregu kumjibu DrSlaa kuwa moyoni mwake nchi iko mbele kuliko vyama-that was patriotic.
Today we are reaping the proceeds of patriotism.
 
Tanganyika haitamkwi kwa sababu ni neo la Kikoloni, kwa maana nyingine Mlm Nyerere alilifuta kabisa na hakuliita kwa sababu lilianzishwa na Wakoloni na ndio maana haulisikii, kushabikia jina la Tanganyika ni sawa tu na kushabikia au kuuliza kwa nini tusiitwe German East Afrika? nikikuuliza kwa nini tusiitwe hivyo? kwa maana ndio jina asilia kabisa la Nchi yetu, kwa maana nyingine German East Afrika ndio hasa tunapaswa kulipigania kama hoja ni tu jina asili la nchi yetu!
Ndio maana wanaoelewa vizuri historia ya nchi mpamoja na hiyo tume ya Katiba wanapendelea kutumia Tanzania Bara!

tatizo sio nani aliyeanzisha jina la Taganyika bali maana pia ni muhimu kujiuliza ,we jiulize Tan-zan-ia (Tanganyika na zanzibar wakitumia kiunganishi cha nia)mana yake nini na Tanga-nyika(pwani ya kuingia ardhi isiyojulikana) mana yake nini?halaf tujiulize kwanini tuendelee kuwajumuisha wazanzibar ndani ya bara wakati wao tayari wanajitambua wapo tofaut na Tanganyika na ndani ya shirikisho wakiwa wanajiwakilisha wao kama wao wazanzibar?
tuache kukumbatia tusivyovielewa kisa tu alisema mtu fulani
 
Kwani kuna Ubaya gani tukiitwa Tanzania Bara? Mbona ni jina zuri tu, tayari linajulikana, sasa unataka tuingiie tena gharama za kubadilisha jina? ili nini? Unajua kubadilisha jina kuna gharama?
Waulize Afrika Kusini kwa nini wameamua kuendelea na majina yao yale yale, si nao walitaka kubadilisha yote kuanzia Capetown, J'burg, Pretoria n.k gharama ikawashinda, wakaamua kuyabakiza, yaani ktk mambo yoote tunayoweza kubadilisha kweli Jina tu liwe tabu?

Hata kama tukibakiza Tanzania ambalo linajumisha Zanzibar sisi tutapoteza nini? Kumbuka unaongelea nchi yenye kilometa za Mraba 2000 na watu wasiofika milioni 1, dhidi ya nchi yenye km za Mraba 945 000 na watu zaidi ya milioni 40, huoni hapo kuna walakini kudai haki kutoka kwa kwenye namba ndogo kama hiyo? Kama unakumbuka Hesabu za uwiano unaweza kufanya hiyo namba, yaani ni kichekesho Watu Bara kudai kudhulimiwa na Wazanzibari!

Kuna mambo lazima uyapime kwanza, hata baada ya kupata Uhuru viongozi wengi wa Kiafrika walifikiria kubadilisha mipaka ya kikoloni lkn wakaaona gharama ya kubadilisha kubwa kuliko ya kuiacha kama ilivyo, hata hili la Zanzibar, ni Nchi ndogo sana kuweza kutunyima usingizi yaani ni karibu sawa na Mkoa wa Dar tu!

Nadhani Kijakazi una tatizo la kuijua historia na kueleza kitu hisichokijua ni kama kupapasa gizani kwa hiyo waache wanaojua historia ya Tanganyika wachangie japo unao uhuru wa kuchangia. Tanganyika ni nchi ambayo ilipata uhuru wake 9 Disemba 1961. Tanzania ni nchi imekuja baada ya muungano wa nchi mbili Zanzibar na Tanganyika. Ukiondoa Zanzibar hakuna Tanzania, umeelezwa maneno yanayounda Tanzania yanatokana na nini. Labda kama una tatizo la kutamka Tanganyika utuelezee na si swala la ukoloni sijui wa kijerumani. Nadhani umezaliwa kabla ya Tanganyika nalo linaweza kuwa tatizo lako.
Hapajawahi kuwepo nchi inaitwa Tanzania Bara, ilo litakuwa ni jina jipya la nchi hiyo tangu tupate uhuru. Au tukubali iwe Tanganyika na wao Zanzibar au Tanzania Bara na wao Tanzania Visiwani
 
Hivi nisaidieni... halmashauri zetu na hiyo sera ya majimbo what is the differences and similarities...

Mfumo wetu wa Halmashauri japo unaitwa ni "Local Government" lakini kwa kweli bado uko very centralized na unategemea serikali "kuu". Halmashauri haziko uhuru - imagine Mkurugenzi wa Halmashauri anateuliwa na Waziri Mkuu! Hakuna halmashauri ambayo iko huru from the reach of the central government as a matter of fact sidhani kama kuna halmashauri inayofanya kazi bila kutegemea TAMISEMI.
 
yani me nishachoka na hii habari

hivi kwa nn tusitengane tu

kila mmoja aende na shida zake.
 
Tanganyika haitamkwi kwa sababu ni neo la Kikoloni, kwa maana nyingine Mlm Nyerere alilifuta kabisa na hakuliita kwa sababu lilianzishwa na Wakoloni na ndio maana haulisikii, kushabikia jina la Tanganyika ni sawa tu na kushabikia au kuuliza kwa nini tusiitwe German East Afrika? nikikuuliza kwa nini tusiitwe hivyo? kwa maana ndio jina asilia kabisa la Nchi yetu, kwa maana nyingine German East Afrika ndio hasa tunapaswa kulipigania kama hoja ni tu jina asili la nchi yetu!
Ndio maana wanaoelewa vizuri historia ya nchi mpamoja na hiyo tume ya Katiba wanapendelea kutumia Tanzania Bara!

Umesema vyema kabisa; Tanganyika siyo zao la Watanganyika - hata wakiligombania. Tanganyika lilikuwa ni zao la siasa za wakoloni (kuanzia Ujerumani na baadaye Uingereza). Watu wa Tanganyika hawakuwa na ushauri wala hiari ya kuwemo ndani ya Tanganyika. Kuidai Tanganyika na watu kuona ati ni 'fahari' kuirudisha ni sawasawa na kukubali kuwa Mkoloni alikuwa sahihi na sisi tunashukuru!

Nchi ya Tanzania ndio zao pekee katika Afrika la watu wa Tanzania. Ni nchi yetu wenyewe tuliyoiunda wenyewe ndio maana hata Zanzibar wakiitoa ni bora kuendelea kujiita Tanzania kuliko Tanganyika na tunaweza kujipendelea tu kubadilisha sababu ya kwanini tutaendelea kuitwa Tanzania - remember Azania?

Hata ikirudi Tanganyika (kwa jina lolote lile) na Zanzibar ikatoka bado hoja ya kuigawa katika majimbo ya kiutawala inasimama kuliko ilivyo sasa. Tungerudisha madaraka mikononi mwa mahali vizuri zaidi kuchochea utawala bora, demokrasia na maendeleo. Nchi yetu ya watu milioni karibu hamsini haiwezi kuendelea kutawaliwa kutoka Makao Makuu fulani hivi.. tunahitaji kutoa nafasi kwa maeneo kujijenga..
 
Nadhani Kijakazi una tatizo la kuijua historia na kueleza kitu hisichokijua ni kama kupapasa gizani kwa hiyo waache wanaojua historia ya Tanganyika wachangie japo unao uhuru wa kuchangia. Tanganyika ni nchi ambayo ilipata uhuru wake 9 Disemba 1961. Tanzania ni nchi imekuja baada ya muungano wa nchi mbili Zanzibar na Tanganyika. Ukiondoa Zanzibar hakuna Tanzania, umeelezwa maneno yanayounda Tanzania yanatokana na nini. Labda kama una tatizo la kutamka Tanganyika utuelezee na si swala la ukoloni sijui wa kijerumani. Nadhani umezaliwa kabla ya Tanganyika nalo linaweza kuwa tatizo lako.
Hapajawahi kuwepo nchi inaitwa Tanzania Bara, ilo litakuwa ni jina jipya la nchi hiyo tangu tupate uhuru. Au tukubali iwe Tanganyika na wao Zanzibar au Tanzania Bara na wao Tanzania Visiwani

Ngoja nikuulize swali dogo sana hivi unajua kati ya Majina ambayo yalipendekezwa kuitwa nchi yetu na Waingereza baada ya kushinda vita yalikuwa New Maryland, Windsorland na Victoria? Je yule Waziri wa mambo ya ukoloni wa Uingereza angeamua kuiita nchi yetu hivyo pia mngekuwa leo hii mnapigania hayo majina badala ya Tanzania? Kwa maana pia badala ya Tanganyika tungekuwa tunaitwa New Maryland, Windsorland, au Victoria, Je pia ungepigania hayo Majina?

tusipoteza muda kujadili mambo ambayo hayana maana Mlm Nyerere alipoamua kuiita Nchi Tanzania badala yaTanganyika hakuwa mjinga alijua yote haya.
unaweza hata ukaiita nchi yetu X ukitaka, kwani jina linatunyima nini sisi? Na ndio maana nikakupa mfano wa Afrika Kusini hata wao walitaka kubadilisha majina kwa ajili ya mambo ya kihistoria, kwani hata kama Zanzibar wakijitenga kesho na tukabaki kuitwa Tanzania kuna tatizo gani?

Shida yangu mimi ni kwa nini Jina liwe ishu? Na ndio maana nika kwambia kama swala ni Jina lenye asili ya Nchi yetu basi ni German East Africa na sio Tanganyika, kwa maana Tanganyika nalo liliwekwa tu kama vile Tanzania, lkn jina asilia la Nchi yetu ni German East Africa!

Back
Top Bottom