In Fact: Kwa Kupendekeza Tanganyika Tume ya Warioba Imependekeza Majimbo!

In Fact: Kwa Kupendekeza Tanganyika Tume ya Warioba Imependekeza Majimbo!

Mzee Mwanakijiji, nisngependa kukubaliana na Nonda juu ya observation yako.
Naelewa kuwa CHADEMA na CUF are in total dis array baada ya kutolewa rasimu ya Katiba mpya.
Hivyo basi sioni analogy ya Tanganyika na Zanzibar kuwa "majimbo" kwa maana ya majimbo ya uchaguzi kwa jinsi tunavyoyajua.
They are more than that, halafu Zanzibar ni nchi atii!!!!
Ndugu yangu chukulia USA inaundwa na kile kwa kiingereza kinaitwa 'States' na sisi hapa kwetu tunayaita majimbo. Kilivhopendekezwa na Rasmu yetu hakina tofauti na hili.
 
Hivi ikitokea Tanganyika ikaongozwa na cdm, zanzibar cuf na muungano ccm hali itakuwaje?
 
Mwana Kijiji nadhani ujawaelewa vizuri hawa Tume ya Katiba, hakuna mahali wanatamka Tanganyika, badala yake kinachotamkwa ni Tanzania Bara, lakini cha ajabu wanashindwa kutamka Tanzania Visiwani. Maoni yangu ni kwamba wameamua kuizika Tanganyika kabisa. Kama ni serikali tatu basi kuwepo Seriakali ya Mapinduzi ya Zanzibar, serikali ya Tanganyika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Au waseme Tanzania Visiwani, Tanzania Bara na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Hakuna Tanzania bila kuwepo Tanganyika na Zanzibar maana neno TAN(Tanganyika)ZA(Zanzibar) NIA kama kuleta jina linalotamkwa. Kwa hiyo lazima kama wameamua kuwepo serikali tatu Tanganyika lazima itamkwe na wala si Tanzania Bara
Si kweli kwamba hawajaitamka Tanganyika. Ebu angalia kwenye Ibara za mwanzoni wanapotafsri Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Kwa maoni yangu Tanzania bara haina tafsiri na haijulikani ni nchi gani na wala mipaka yake haiewezi kupambanuliwa. Magia na Kilwa itakuwa wapi bara au visiwani?
 
Mfumo wetu wa Halmashauri japo unaitwa ni "Local Government" lakini kwa kweli bado uko very centralized na unategemea serikali "kuu". Halmashauri haziko uhuru - imagine Mkurugenzi wa Halmashauri anateuliwa na Waziri Mkuu! Hakuna halmashauri ambayo iko huru from the reach of the central government as a matter of fact sidhani kama kuna halmashauri inayofanya kazi bila kutegemea TAMISEMI.
Maoni yangu ni kuwa baada ya kuwa na majimbno makubwa mawili, Serkali yetu ya Tanganyika tuiweke katika mfumo wa majimbo. Tutoe madaraka kwa serkali za majimbo tutakayoyagawa katika mfumo wetu wa utawala.
 
Maoni yangu ni kuwa baada ya kuwa na majimbno makubwa mawili, Serkali yetu ya Tanganyika tuiweke katika mfumo wa majimbo. Tutoe madaraka kwa serkali za majimbo tutakayoyagawa katika mfumo wetu wa utawala.


Siku zote ninaposoma makala la Mzee Mwanakijiji,huwa naona yafuatayo:

1:Lengo lake Kuu toka moyoni ni kuona serikali inayotawala hivi sasa inatolewa madarakani
2:Ana be troubled kwelikweli toka myoni,kwani anajua sio lelemama hata kidogo kuung'oa current utawala
bila kufanya mabadiliko fulani katika JMT(iwe ni jambo zuri,ama jambo baya,alimradi kuung'oa utawala huu)

Hivyo basi;Topic zake siku zote ninaziona ni kama ndoana iliyovishwa ng'onyo ili kumu attract samaki kwamba kuna msosi mzuri,kumbe kwa kudhania unameza ng'onyo,ndio unakuwa unajiingiza matatizoni kwa faida ya MVUVI;

Huwa simwelewi Mwanakijiji siku zote anavyotoa topic za kuonyesha kwamba anaonyesha moyo wa kuwa support Wazanzibar waweze kujitenga toka JMT.....Hivi ni kweli ana upendo na Wazaznzibar(NA pia ni kweli anaona wAzanzibar wanaonewa katika Muungano?),ama ANA CHUKI NAO na anaona mbona wanachelewa kuondoka toka kwetu?Ama ni kwamba anashadadia hilo kwa sababu tu anajua kwamba Zanzibar ni mojawapo ya sehemu ambayo inachelewesha ndoto zake za kuona current Utawala unatoka madarakani?(Kumbuka kwamba Mwanakijiji yeye ana Chama chake ambacho kwa sasa anakishadadia,na anajua kabisa kwamba Zanzibar haina mchango wowote katika kusaidia Chama hicho kuhukua madaraka ya Nchi).

Majimbo "Tanganyika"(unajua vema sana kwanini umeamua kutumia jina hilo....sio kweli kwamba una uchungu na jina Tanganyika,bali una Uchungu na kwanini watu hawajadili kitu kitakachosababisha wakumbuke kuuvunja Muungano)-Tanzania Bara na "Tanzania Visiwani" ati unataka kuyaweka katika rationale ya Muungano wa Mikoa(kwamba kwanini kukubali Tanzania Bara na Tanzania Visiwani autonomy(semi?) ndani ya Muungano na kukataa Kanda-kundi la mikoa kadhaa yenye autonomy(semi?) ndani ya Muungano.....Hivi kweli Mwanakijiji unataka Mimi nikuamini kwamba huelewi Tanzania Bara na Tanzania Visiwani ni Nchi,wakati hizo Kanda unazozishadadia ni Mkusanyiko wa Mikoa fulani?.....ninadhani siku zote unapenda kujitoa ufahamu ili kupumbaza wengine,kama vile samaki wanavypumbazwa na ng'onyo kwenye ndoana......

Kwanini Tanganyika inakubalika kupoteza jina hilo na zanzibar inalishikilia.....Mmmmmh

Wewe Mwanakijiji ninajua unaelewa kabisa kabisa kwamba katika Nchi/sehemu za Africa ambazo Duniani zinajulikana sana ni pamoja na Zanzibar,Kenya,Madagascar....Nigeria,Somalia,Congo......Hivi hebu niambie,unataka kujifanya hujui ni gharama kiasi gani itakayowa cost Madagascar kubadili jina hilo na kuwa jina jingine?....Unataka kuniambia Watu kama Somalia kubadili jina hakuwezi kukawapa BIG PLUS katika World image?
NItakacho kusema hapa ni kwamba,jina Zanzibar ni kama TRADEMARK....kulibadilisha jina hilo ni kujitakia hasara kubwa sana....ni sawa na kuanza kutaka kubadili jina Mt.Kilimanjaro kutaka kuita Mt.Mangi!....unajua gharama zake(unajua ninajua...lakini unajitoa ufahamu kuwapumbaza wengine!)......UTALII ndio sababu kubwa ya ku preserve jina la ZANZIBAR Kaka.....Jina Tanganyika halina maANA YEYOTE hata leo ukiamua kuita sehemu inayotumia jina hilo kuwa Tanga!.......Siku zote ninapokuwa nje ya Nchi,ninawaambia wenzetu wa nje ninatoka Tanzania wanasema Oooooh,Tasmania?(i know unajua Tasmania iko wapi)....basi inabidi nianze kuwaeleza kwamba ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,hapo wanasema Ooooh,Zanzibar,yeeeeah!.....badaye ukiwaambia chini ya Kenya wanasema yeah Kenya I know.....Sasa wewe unataka ZANZIBAR iitwe Tanzania Visiwani!....Hivi hujui kabisa kwamba Tanzania bara inapata Watalii wengi sana sana wengi wao lengo lao ni kutaka kwenda Zanzibar(as original idea),lakini wanapita Tanzania Bara as "by the way"..........Hata Kenya,ukitaka kuua jina Mombasa,ni Kasheshe kuliko kuua jina "Nyeri"!

WaTanzania siku hizi wamechoka kufikiri....wamechoka....wengi wanasubiri Watu wawafikirie,wao ndio waende kueneza kile kilichofikiriwa na wenzao....
Watu wana discuss rasimu ya Katiba sio kwa sababu wao wameichambua,bali kwa sababu wamesikia Watu fulani wametoa msimamo fulani against ama for certain content ya Rasimu.....

Ninarudia....Majimbo ni "mtego" ambao kama CCM wataukubali....utawaliza...ukatae usikubali majimbo(kama yanayoshadadiwa na Wanasiasa hivi sasa) katika Nchi zetu za Africa ni Chanzo cha Ukabila.....Ukatae usikubali,Africa Watu wanapiga Kura kwa kufuata Kabila,Dini,Rushwa.....

Ninarudia kusema Kenya majuzi kina Ruto na Kenyatta walijua kwamba Odinga ni "Absolute" winner kama wasipofanya "UCHAWI"....Wakaamua kuunganisha Makabila yao(wakatoa wagombea toka Kanda mbalimbali)na kweli wakamshinda Odinga......

Tutadhani kwamba tunaanzisha kitu kwa manufaa yetu,kumbe in the long run tutaja lia na kusaga meno
 
Back
Top Bottom