In Fact: Kwa Kupendekeza Tanganyika Tume ya Warioba Imependekeza Majimbo!

Unabisha bila mantiki bola nikuache maaana hujui unataka kuongelea nini. Mwl hakuacha kuiita Tanganyika kwa sababu ya ukoloni unaoongelea na Tanzania haikuja ili kufuta Tanganyika ya mkoloni. Narudia kukuelewesha tena. Tanzania imekuja kwa sababu ya muungano na ni muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar. Sasa ukianza kuongelea mambo ya mkoloni basi Zanzibar hisiwepo kwa sababu ni kukumbuka Usultani wa Kiarabu bari tuiite Unguja na Pemba. Inaonekana wewe ni mgumu wa kuelewa. Jamani watu nisaidie kumwelewesha huyu mtu Kijakazi maana mimi sijawahi kufundisha watu wenye vichwa vigumu
 

poa poa tuachie hapo!

 

hivi unajua hata sababu ya kubadili jina kutoka Tanganyika kwenda Tanzania?
nakuomba usiniambie kwamba Nyerere hakua mjinga kubadili jina bila kunipa sababu ya msingi itakayotufanya tuendelee kushikilia hili jina?
halaf kwa kumbukumbu nilizonazo Nyerere hakulibadilisha jina la Tanganyika, ni katika uongozi wa Mwinyi ndio jina lilibadilika,
na hivi unadhani wazanzibar ni wajinga kukomaa na jina lao toka nchi hizi zimeungana Tanganyika na Zanzibar na kuitwa Tanzania?na kama sio wao kukomaa wangepoteza identity yao .
kwa hili suala ni sawasawa na leo ujarib kubadili jina la Israel na kuiita shetan halaf uone kama hakuna umuhimu wa jina kwenye jamii.
kwa kifupi tunataka Jina letu Tanganyika
 

Mimi nadhani tunahitaji Evolution sio Revolution... angalieni na uelewa wa Wananchi wetu... Hivi tangu Serikali za Mitaa zianze ni miaka mingapi? Kwa nini wananchi hawajachangamkia hayo madaraka yao... Leo hii Bungeni wabunge wengi wanaongea mambo ya kwenye mabaraza ya madiwani... as if wao sio wajumbe wa hizo halmashauri... kama wabunge wenyewe bado.... is it realistic real to go to Majimbo... meaning fully independent halmashauri... real let think critically jamani.
 
Bila definitions za federation na cnfederation hapa tutakesha bure, maana inaoekana kama kwamba yote yana maana moja kwa kiswahili. Halafu tujue tume ilimaanisha ipi kati ya hizo mbili.
 

..kama wananchi wengi wamependekeza serikali 3, basi CUF na CDM, wako upande wa walio wengi.

..walichokipinga CDM ni mchakato wa kupata wajumbe wa mabaraza ya katiba. wanadai waliwasilisha malalamiko yao kwa tume ya Warioba, lakini hawakusikilizwa.

..hayo majibu ya Prof.Baregu yanaweza kutolewa na mtu yeyote yule. hata mimi naweza kusema CDM walipokuwa wanapinga mfumo mbovu wa kuchagua mabaraza ya katiba waliweka maslahi ya taifa mbele.

..kwa upande wangu, naona kwa kiasi kikubwa CDM na CUF ndiyo washindi ktk hatua hii ya kwanza kuelekea katiba mpya.
 

Hapa tunazungumzia majimbo (provinces) na sio majimbo ya uchaguzi (constituencies)
 
sijui ni kwa nini watawala wetu wanashinikiza kuwepo kwa muungano bila kuuliza kama wenye nchi wanautaka au la!!

Kuvunjika muungano ndio mwisho wa CCM. Nnje ya muungano hamna CCM.Nnje ya muungano ni TANU na ASP.
 

Kutoshirikishwa Kwao kilitokana na ukweli kwamba uhuru wao haukua kamili .... nchi ya Zanzibar iliipindua serikali ya ukoloni bila ya kuwa na jeshi wala polisi wa kuulinda Uhuru huo.... Njia pekee ilikua ni kuungana na Tanganyika ili kuwepo na jeshi na Polisi wa kulinda Uhuru kutoka bara..... leo wanasema hawakushirikishwa tena kwa ushauri unaoyolewa na wale wale waliowatala safari hii wanajiita wa harakati wa kiislam ili kuficha dhamira yao ya kweli....!
 

bado mwanakijiji anatokwa na kipovu than nimegundua mtoa mada hupenda kukurupuka bila kutafuta taarifa za kweli.warioba hakusema serikali ya tanganyika amesema serikali ya tanzania bara
 
bado mwanakijiji anatokwa na kipovu than nimegundua mtoa mada hupenda kukurupuka bila kutafuta taarifa za kweli.warioba hakusema serikali ya tanganyika amesema serikali ya tanzania bara

Wengine wanasema "Potato" na wengine wanasema "Poteto"...
 

Kijakazi
Mwaka 1964 nchi zilizoungana ziliitwa kwa majina yepi?

Zanzibar iliungana na nchi ipi?

Katika dunia hii wapi umesikia,umesoma au umeota ndoto kuwa muungano unaua jina la nchi wanachama wake?

Jina Tanzania lilianza kutumika lini? Jina la asili la muungano unalifahamu?

Nani alifanya "mazingombwe" ya Tanzania kuwa na "bara" mbele yake.

Mafia,Juani, Jibonde, Ukerewe ni Tanzania bara,Tanzania visiwani au Tanganyika visiwani?

Unajua vipi lilitengenezwa,lilibuniwa jina Tanzania?

Nchi zipi zilisaini mkataba wa Muungano?

Kwa nini hatukubadilisha jina Tanganyika baada ya kupata uhuru 1961?
 

Maisha nenda rudi ccm kamwe hawatakubali kura kupigwa kwani wanajua kura itaamua kile wasichokitaka
 

Mifano iko Mingi ya Muungano wa nchi ambyao imeua jina moja wa wanachama kwa mfano,


Kwa nini jina liwe Ishu? Jina linabadilisha nini? tungekuwa tunaongelea faida na hasara tunazopita kiuchumi kutokana na yaliyomo kwenye Mkataba wa Muungano sawa lkn SIYO jina! Sijawahi kusikia mimi sehemu yoyote watu wanabishania jina!

Waafrika kusini baada ya Apartheid kuisha pia walitaka kubadilisha jina Afrika Kusini (South Africa) kwa kuwa halikuwa lao bali ni la wazungu, lkn mwisho wa siku wakaja kugundua kwamba kubadilisha JINA hakutawafaidisha chochote, cha muhimu ni kuangalia Sera za kuwakomboa watu wao kiuchumi, hata sisi tunaweza kufanya hivyo, tuna mambo mengi ya kufanya ili kuboresha maisha yetu badala tu ya kubishania Jina!

 
Mkuu umejitahidi sana kumuelewesha huyo Kijakazi, ila naona ni mgumu sana kuelewa. Kama alifika darasani, waalimu wake walikuwa na kazi ya ziada!
 

Nakubaliana na wewe Mkuu, kuna watu huwa wanajitoa akili ama wana akili za kushikiwa kwa sababu fulani alisema. Niwaulize wale wanaoionea aibu Tanganyika, Nyerere na wenzake wakati wa harakati zao za kutafuta uhuru, walikuwa wanatafuta uhuru wa nchi gani kati ya hizi; Germany East Afrika, Tanganyika, Tanzania Bara? Na baada ya kupata uhuru ule walishangilia na kubebana kwa fahari ya uhuru wa nchi gani? Kipindi kile hawakuona aibu ya kuitwa jina hilo?
 

hukujibu swali langu umebaki kuuliza swali lilelile la jina lina umuhimu gani?naomba nikuulize kama una mtoto? huyo mtoto umempa jina gani? au ulitoa tu jina bila sababu?

halaf usiwe na mawazo finyu eti tujadili sera za kiuchumi tu.kuna mwanafalsafa mmoja Yesu kristo alisema binadamu hutaishi kwa mkate tu.alimaanisha watu hawataishi kwajili ya mambo ya kiuchumi tu,usiwe kama mnyama anayeangalaia atakula nini tu leo wewe ni binadamu una mambo mengi ya kuangalia zaidi ya uchumi

kuna mambo mengi ya kuangalia katika katiba na sio sera za uchumi tu,bali pia na sera za kisiasa,na kijamiii na kiutamaduni ambazo zinahitaji mjadala, la sivyo kungekua hakuna umuhimu wa kua na fani tofauti bali wote tungesomea uchumi tu.

Lazima tuitengeneze Tanzania tunayoitaka na Tanganyika ni muhimu iwepo.

kama wasauzi waliridhika na hilo jina ni maamuzi yao na wanalia na kusaga meno mpaka leo kwa kutokua makini wakati walipopewa nchi kwani njia kuu zote za kiuchumi zimeshikwa na tabaka la wazungu na waafrika wengi ni maskini wa kutupwa na wasio na kazi, na yote hii ni inatokana na kudharau mambo madogomadogo ambayo ni kama tone la maji lakini linapasua mwamba baada ya muda mrefu
 

si tunaitwa Tanzania Bara, tatizo liko wapi? Shida yako hasa ni nini? ni jina Tanganyika tu? au ni lazima tuitwe Tanganyika ndio uridhike? tatizo liko hapo? au ni mimi labda sikuelewi? embu nisaidie kwa mara ya mwisho kukuelewa kama ukiweza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…