Ina maana gani kuota unatembea uchi mbele ya watu?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Kwanza kabisa nilikuwa juu ya jengo la ghorofa 4 nikiwa uchi kama nilivozaliwa, sasa wakati nashuka zile ngazi zilikuwa ni zile zinakaaga nje kwa pembeni, cha ajabu hizo ngazi hazikuwa za kawaida yaani ni nyembamba mno kiasi ya kwamba ili uzishuke lazima uwe umegeuzia tumbo ukutani na ushikilie ukuta.

Kwakweli nilijaribu tu kutembea ngazi moja nikashindwa sababu ya kuangalia macho chini, ila cha ajabu nilijikuta namalizia ngazi ya mwisho chini kushuka na nikashuka nikiwa hivo hivo uchi na kuanza kutembea kwenda jengo lingine lililokuwa pembeni yake.

Watu walikuwa tu wengi ila nilijipa ujasiri nikachukua mashine yangu na kuibana kwenye mapaja na kuanza kutembea, nikaenda bafuni na kuoga ila sikumbuki kabisa kama niliweza kuvaa nguo.
 
Ndoto ni njia rahisi Mungu kusema na mwanadam yeyote.
Kutembea mbele za watu uchi ni jambo la aibu, maana kuna jambo la aibu litakupata
Kushuka gorofani inaweza kuwa na maana ya kushuka kibiashara, kicheo nk.
Lakini unaweza kumuomba Mungu akuepushe na ayo.
 
Bro umerithishwa uchawi, nenda kaombewe Kimara Temboni
 
Watabiri wasaidizi wa Sh Yahya Husein wamekuwa wengi huku kwenye mtandao.
 
Ndoto ni njia rahisi Mungu kusema na mwanadam yeyote.
Kutembea mbele za watu uchi ni jambo la aibu, maana kuna jambo la aibu litakupata
Kushuka gorofani inaweza kuwa na maana ya kushuka kibiashara, kicheo nk.
Lakini unaweza kumuomba Mungu akuepushe na ayo.
Akiota anaendesha NISSAN patrol je inaashiria nini
 
Kuna aibu itakukumba. Mwombe Mungu akuepushie mbali aibu inayokunyemelea
Sikukuona katika Msiba wa Neurologist wa Jeshi ( JWTZ ) Uncle wangu na Mzanaki Mwenzangu Brigadier Professor Yardon Kohi Mortuary Lugalo na pale Kwake Mbezi Beach.

Naona idadi ya Wanywa Wine Kali za Kirusi mnapungua tu hapo Mbezi Beach akiwemo na yule Gwasu Msuya ( Kaka mkubwa wa aliyekuwa TISS DGIS ) Diwani Athuman Msuya.

Kama hukuwepo Msibani umekosa Bia na Wine za bure kwani kulikuwa na Bia na Pombe nyingi mno za Kumuenzi Mwanachama Mzee Kohi ambaye Leo anatarajiwa Kuzikwa huko Kwao Busegwe Wilayani Butiama Mkoa wa Wanamume na Mashujaa wa Mara ( Musoma )

R.I.P Uncle Kohi.
 
Wengi wanakwambia kuna jambo la aibu linakujia ila inawezekana wewe ni muoga wa kuonekana maumbile yako na kuna nyakati ulishaimagine hivyo. Ndoto mara nyingi(Siyo mara zote) ni reflaction ya uliyowahi kufikiri au kuyaona.
 
Back
Top Bottom