Ina maana gani kuota unatembea uchi mbele ya watu?

Ina maana gani kuota unatembea uchi mbele ya watu?

Kuna aibu itakukumba. Mwombe Mungu akuepushie mbali aibu inayokunyemelea
Mimi niliota Kuna watu walikuwa wameniibia viatu nikawa nawasaka nilifika sehemu naulizia wanasema hawajawaona,then nikaamua kurudi home,nje walikuwa wamekaa wanaume kadhaa wanapiga story,Wala hawakuniangalia wakaendelea na story zao .Nikaingia uani,nikakuta binti mmoja anauza duka na baadhi ya ndugu,mama yangu alikuwa amesimama pembeni,(ni marehemu sasa)nikawa nalalamika kuhusu kuibiwa viatu vyangu,wale ndugu wakanishangaa wakanambia mbona uko uchi,nikastuka nikajifunika sehemu za Siri na viganja,mama akawaambia wanipe shuka,wakanipatia shuka jekundu nikajitanda,akachukua maji kwenye kikombe akamwaga kwenye maji yalokuwa yamesimama yakionekana na uchafu,alipomwagia Yale maji toka kwenye kikombe ule uchafu kwenye maji Yale yalotuama ukatoweka/kuyayuka,mie nikatazamana na yule dada alokuwa auza duka tukatabasamu,hapo ndo fahamu zikanijia,kuona mama yangu yupo hapo,nikataka kumsalimia na kumjulia hali then nikazinduka toka usingizini,toka sikuile nawaza tafrsir ya hii ndoto,ila Sina majibu,naomba nifafanulie mkuu Kama una weza.
 
Kwanza kabisa nilikuwa juu ya jengo la ghorofa 4 nikiwa uchi kama nilivozaliwa, sasa wakati nashuka zile ngazi zilikuwa ni zile zinakaaga nje kwa pembeni, cha ajabu hizo ngazi hazikuwa za kawaida yaani ni nyembamba mno kiasi ya kwamba ili uzishuke lazima uwe umegeuzia tumbo ukutani na ushikilie ukuta.

Kwakweli nilijaribu tu kutembea ngazi moja nikashindwa sababu ya kuangalia macho chini, ila cha ajabu nilijikuta namalizia ngazi ya mwisho chini kushuka na nikashuka nikiwa hivo hivo uchi na kuanza kutembea kwenda jengo lingine lililokuwa pembeni yake.

Watu walikuwa tu wengi ila nilijipa ujasiri nikachukua mashine yangu na kuibana kwenye mapaja na kuanza kutembea, nikaenda bafuni na kuoga ila sikumbuki kabisa kama niliweza kuvaa nguo.
Inaamanisha maandalizi ya marinda kutatuliwa kutokana labda kwa dhulma na wizi
 
Angalia maisha yako, angalia ulipokosea omba sana Maana aibu yako ipo wazi kwa watu. Hiyo ni Allert tu ila kuna mambo unayofanya yatageuka kuwa aibu kubwa sana na hutakuwa na ya sehemu ya kujificha. kitendo cha kushuka ghorofani ni kwamba utashushwa chini kabisa

N.B OMBA SANA ISIJE KUWA AIBU KAMA YA AFANDE WA ZANZIBAR
 
Kuota ukiwa mtupu humaanisha kudhalilika, kuumbuka ama siri zako kufichuka. Sio ndoto nzuri sana.

Kuota ukishuka chini humaanisha kushuka kwako aidha kiuchumi, kiafya ama mabadiliko yeyote katika maisha yako kulekea kupungua kutoka hali iliyopo sasa. Nayo si ndoto nzuri sana.

Jaribu kumuomba Mungu sana kwa imani yako. Pia toa sadaka kwa wingi.

Mungu akuepushe na kila baya.
 
Kwanza kabisa nilikuwa juu ya jengo la ghorofa 4 nikiwa uchi kama nilivozaliwa, sasa wakati nashuka zile ngazi zilikuwa ni zile zinakaaga nje kwa pembeni, cha ajabu hizo ngazi hazikuwa za kawaida yaani ni nyembamba mno kiasi ya kwamba ili uzishuke lazima uwe umegeuzia tumbo ukutani na ushikilie ukuta.

Kwakweli nilijaribu tu kutembea ngazi moja nikashindwa sababu ya kuangalia macho chini, ila cha ajabu nilijikuta namalizia ngazi ya mwisho chini kushuka na nikashuka nikiwa hivo hivo uchi na kuanza kutembea kwenda jengo lingine lililokuwa pembeni yake.

Watu walikuwa tu wengi ila nilijipa ujasiri nikachukua mashine yangu na kuibana kwenye mapaja na kuanza kutembea, nikaenda bafuni na kuoga ila sikumbuki kabisa kama niliweza kuvaa nguo.
Ndo Basi tena maskini..... Ushaharibikiwa.....
 
Acha Cuca,,, fedheha inafuata shauri yako!!!
 
Kuota unatembea uchi huku ukihangaika kujiziba ina maana ya kupoteza fedha na kuangukia katika umaskini

Pia inaweza kuwa na maana ya SKENDO.

Inaweza pia kumaanisha kutenda jambo ambalo litakupelekea kupata aibu/majuto/kufanya biashara ambayo itakupelea kujuta.

Kujiona upo uchi mbele ya mjumuiko wa watu pia kuna maana ya kuwa siri zako ulizozificha zitafichuka na kukupelekea kufadhaika.

na ALLAH ndie mjuzi zaidi
 
Jiandae kuaibika ila sio kwa jambo kubwa sana nakwambia hivi haita pita miezi miwili kabla hujakubwa na aibu, hayo ni maono sio ndoto so lazima yatimie hata ufanyaje lazima yatimie katika ulimwengu wa mwili.
 
Nyoka ni kiashiria cha uadui, vita, mikosi. Kuna kitu ambacho kinakuzuia usiende mbele, umefanya majaribio na jitihada mbalimbali, lakini mwisho wa siku uko palepale. Kuna roho ya kupambana nayo, ndiyo hiyo inayokuzuia.

Kuna vitu vya kufanya. Wakati mwingine adui yetu anakuwepo ndani yetu. Huenda ni tabia fulani, nataka niiache lakini najikuta nairudia.
Aache kamari,ulevi na uzinzi
 
Kwanza kabisa nilikuwa juu ya jengo la ghorofa 4 nikiwa uchi kama nilivozaliwa, sasa wakati nashuka zile ngazi zilikuwa ni zile zinakaaga nje kwa pembeni, cha ajabu hizo ngazi hazikuwa za kawaida yaani ni nyembamba mno kiasi ya kwamba ili uzishuke lazima uwe umegeuzia tumbo ukutani na ushikilie ukuta.

Kwakweli nilijaribu tu kutembea ngazi moja nikashindwa sababu ya kuangalia macho chini, ila cha ajabu nilijikuta namalizia ngazi ya mwisho chini kushuka na nikashuka nikiwa hivo hivo uchi na kuanza kutembea kwenda jengo lingine lililokuwa pembeni yake.

Watu walikuwa tu wengi ila nilijipa ujasiri nikachukua mashine yangu na kuibana kwenye mapaja na kuanza kutembea, nikaenda bafuni na kuoga ila sikumbuki kabisa kama niliweza kuvaa nguo.

Utashushwa cheo kwa kashfa mbaya, kushuka kutoka ghorofani maana yake ni kushushwa cheo, mamlaka, ukuu nk, na kuwa uchi ni kufedheka katika kadhia hiyo.

Fanya maombi haraka na utoe sadaka ikiwezana sadaka ya kuchinja mbuzi nk, na uwape maskini.
 
Jiandae kuaibika ila sio kwa jambo kubwa sana nakwambia hivi haita pita miezi miwili kabla hujakubwa na aibu, hayo ni maono sio ndoto so lazima yatimie hata ufanyaje lazima yatimie katika ulimwengu wa mwili.

Sio kweli lazima yatimie, Mungu kamuonyesha kitu kinachoweza kutokea hapo baadaye hivyo anatakiwa achukue hatua hivi sasa ili jambo hilo lisitokee.
 
Sio kweli lazima yatimie, Mungu kamuonyesha kitu kinachoweza kutokea hapo baadaye hivyo anatakiwa achukue hatua hivi sasa ili jambo hilo lisitokee.
Hayo ni maono lazima yatimie sikatai kuchukua hatua lakini hiyo lazima itimie tushaota ndoto sana mkuu navyomwambia ni sababu ya uzoefu.
 
[emoji1666][emoji1666]
Nyoka ni kiashiria cha uadui, vita, mikosi. Kuna kitu ambacho kinakuzuia usiende mbele, umefanya majaribio na jitihada mbalimbali, lakini mwisho wa siku uko palepale. Kuna roho ya kupambana nayo, ndiyo hiyo inayokuzuia.

Kuna vitu vya kufanya. Wakati mwingine adui yetu anakuwepo ndani yetu. Huenda ni tabia fulani, nataka niiache lakini najikuta nairudia.
 
Hayo ni maono lazima yatimie sikatai kuchukua hatua lakini hiyo lazima itimie tushaota ndoto sana mkuu navyomwambia ni sababu ya uzoefu.

Sio lazima, Yawezekana Mungu anamuonyesha kitu kitakachokuja tokea ili kumfanya achukue tahdhari mapema.
 
Ila ndoto nyingine bwana!!
Mimi naitafsiri ndoto yako kuwa usiporekebisha mienendo yako ipo siku utaaibika
 
wameniibia viatu nikawa nawasaka nilifika sehemu naulizia wanasema hawajawaona,then nikaamua kurudi home,nje walikuwa wamekaa wanaume kadhaa wanapiga story,Wala hawakuniangalia wakaendelea na story zao .
Viatu ni nini? Viatu vinaubeba mwili wako wote. Viatu ni heshima, ndio maana watu wanakuangalia kuanzia chini (viatu). Viatu vinaonyesha hali yako, kama ulitembea kwa miguu mtu akikutazama viatu atajua huyu kapuyanga. Viatu vinaonyesha hali yako ya kipato. Hivyo basi ukiota viatu unakuwa unaota hatma yako (your destiny).

Mtu akichukua nyayo za miguu yako, dhamira yake ni kuharibu hatma yako, au ubaadaye wako au destiny yako.

Kwa ndoto hii ndoto ni kwamba hatma yako imeibiwa. Pia umesema walikuwepo wanaume kadhaa, wala hawakukujali. Hii ina maana upande wa baba yako hawana msaada, wala hawajihusishi na matatizo yako, hivyo ukipatwa na jambo lolote watakaa kimya kama hawakuoni.
Nikaingia uani,nikakuta binti mmoja anauza duka na baadhi ya ndugu,mama yangu alikuwa amesimama pembeni,(ni marehemu sasa)nikawa nalalamika kuhusu kuibiwa viatu vyangu,wale ndugu wakanishangaa wakanambia mbona uko uchi,nikastuka nikajifunika sehemu za Siri na viganja,
Mama ni Mungu mdogo. Mama akakusitiri aibu yako, akakuvalisha shuka jekundu. Msaada wako utatoka kwa Mungu tu, kuvalishwa vazi jekundu ni kupewa mamlaka makubwa, ndio maana rais anapita kwenye red carpet na rais ndio huvaa tai nyekundu na rais ndio husain kwa wino mwekundu.

Kwa hiyo kifupi ni kwamba usiposali kwa juhudi na kumwomba Mungu uwe na kesho nzuri, utaishia kuabika (kuwa uchi) ila ukisali Mungu atashuka kukusitiri na ubaadaye wako utakuwa mkuu.
 
Kuota uko uchi ni ishara ya Fedheha.... Utapata fedheha kutokana na Mambo yako!

Kushuka Ngazi ni kushuka kwa NYOTA...
 
Back
Top Bottom