Kinyungu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 19,484
- 38,416
Wewe mnyalu na biashara wapi na wapi? Wewe unajua tu kugema ulasi na kuuza mia 5 kwa kilita kwenye kilabu. Ndiyo maana hata miti hapo Mafinga wametawala Wakinga na Wachagga.Ninavyofahamu hata mzee Mgaya na lile duka lake la Hardware ana mhasibu na mshauri wa kodi ambaye husimama kama wakili wa maswala yake ya kiuhasibu na kodi.
Ninavyojua ukiwa na kampuni ni lazima uwe na mhasibu na external auditor kwa mujibu wa kanuni na taratibu za TRA.
Freeman Mbowe kuwa jela haimaanishi kwamba biashara zake na maswala yake ya kodi yamesimama.
Na siamini kama Freeman Mbowe huwa anakwenda yeye binafsi TRA kushughulikia maswala ya kodi kama Individual taxpayer kwa sababu biashara zake zimeshavuka level hiyo.
Sisemi kwamba Mbowe hajaonewa bali siyo sawa kulitumia jambo hili kujinufaisha kisiasa, anapaswa aongee kama mfanyabiashara mkubwa.
Nawatakia Dominica yenye baraka!
Hayo.mambo ya kodi na TRA kubambika kodi yamekuzidi sana akili. We leta zile nyuzi zako nyepesi nyepesi za kumhusu Ndugai na covid 19