Inadaiwa hizi video ni za wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020

La muhimu mkuu 'Erythro', ni kuzitumia hizi kama fundisho.

Kosa ni kukubali kushiriki tena kwenye uchaguzi ambao mnajuwa wazi kwamba ni "uchafuzi".

Na msidhani kwamba kwa kuwa Magufuli hayupo, hao watu wataacha tabia zao chafu. La muhimu ni kukataa upuuzi wa aina hiyo usifanyike tena.
 
Baada ya huu wizi wakaenda kuapishwa wameshika Biblia na Quran. Haya mashetani ni hatari sana.
LOoooh!

Hii inatisha sana! Majambazi yanashika vitabu vya dini na kuapa; kama nilivyomsikia Kingai akiapa pale mahakamani?

Mungu atusaidie!

Lakini leo inabidi niulize hili swali: hivi kwa nini iwe ni lazima kuapa? Mtu asiye amini hizi dini hufanyaje?
Naomba tuondoe huu unafiki miongoni mwa jamii.
 
Too low hii unaweza hata ukapozi kijijini kwenu na wanakijiji ukatengeneza video ya kwamba unajaza karatasi ya kura kwenye ndoo....,
njoo na kitu kungine substantial hii ni uchafu tu
 
Hapana, mimi sitakutukana, ila kuna mambo umeyasema kama lawama kwa CHADEMA bila kuangalia uhalisia.

Ndiyo, CHADEMA wanastahili lawama katika mambo kadhaa ambayo hawayafanyi vizuri, na kubwa zaidi ya yote ni hilo ulilogusia kiaina..., la kuwaendea wananchi ambao ndio wenye uwezo wa kubadili mwelekeo wa nchi hii.

CHADEMA mara nyingi sana wameshauriwa wawashirikishe wananchi, kwa kuwa elimisha na kuwapa uongozi wa nini kifanywe. Juhudi zao huko ni hafifu sana, na ndiyo maana CCM huwachezea kama watoto wadogo kwa kujuwa hawana wananchi walio nyuma yao wanaoweza kuzuia michezo hiyo.

CHADEMA hawahitaji kuwa na mamilioni ya wafuasi wanaoweza kusimamia na kushinikiza mabadiliko yawepo nchini. Wakiwa na wafuasi laki tano hadi milioni moja nchi nzima waliotayari kujitoa mbele, mara moja utaona wengi wa wananchi ambao wako kimya wanaingia kwenye mstari nyuma ya hao, na mabadiliko yanakuwepo.

Kwa hiyo, lawama pekee ninayoweza kukubaliana nawe juu ya udhaifu wa CHADEMA ni huo, wa kuwa wazembe katika kuwashirikisha wananchi.

Hayo ya viongozi mamluki, kama akina Slaa, Ngoyai Lowasa, akina Nyalandu na wengine hayo ni mambo madogo sana. Chama chochote huingiza watu wenye ushawishi ili wapate madaraka.

Mwisho, ngoja nikukumbushe kama kumbukumbu zako zimefutika, au kama si ulaghai tu unaoonyesha hapa kulaumu:

CHADEMA wamewahi kuwa na wabunge wengi katika mabunge yaliyopita. Unadhani hao wabunge walipatikana kwa kufanya lelemama mbele ya uchaguzi?
Tazama mara zote walipopatikana wabunge wengi, utaona kuwa maeneo walipotokea wabunge hao watu walikuwa ngangari kulinda haki zao kuwachagua wabunge hao. Walipojaribu kufanya upuuzi wananchi walikuwa tayari kupambana.
 
Haya ni mawazo potofu. Unataka wafanyeje, wapindue nchi?. Huyo Slaa aligombea mlimchagua?. Mbona uchaguzi uliopita waliungwa mkono. Wakiandamana mnalamika wanafanya vurugu . Wakitulia mnasema wamepoa. Kwangu Mimi CHADEMA ndio watakao amua siasa za nchi hii. Ndio maana wanapigwa Vita.
 
Reactions: PNC
Duh...Huo ni wizi.Madaraka ni matamu.

Je hiyo siyo sababu ya maisha ya mlala hoi kuendelea kuwa magumu??
 
Ni kweli mkuu na upo sahihi kabisa, lakini suala la kukaribisha mtu, si mtu yeyote tu, lazima kuwe na utaratibu maalumu,vigezo na pia kusimamia msimamo wenu no matter what.., kumkaribisha mtu mliyemuita fisadi no 1, then baadae mnamkaribisha tena agombee uraisi kupitia tiketi ya chama chenu hio imekaaje?

hapo totally walivuruga kila kitu, huwezi shirikisha wananchi kwenye upuuzi kama huo wakuelewe, ujue katika kila jambo lenye manufaa na ili lizae matunda ni lazima ujue kuna taratibu za kufuata na miiko yake, kwa hio usi base tu kufuata taratibu lazima pia ujue miiko, kama utafuata vyote hautofanikiwa... hata kama unashirikisha wananchi bado haitoshi kama unashindwa kusimamia misimamo yako na kufuata taratibu na miiko kisa tamaa...
 
Stop this nonsense, siyo Tanzania, watu tunaogopa sana, watu tu waoga sana tena sana wa KUFA. Hakuna aliyetayari kufa. Mpaka hapo woga utakapo tutoka ndipo tutaona mabadiliko makubwa. Kenya WANANCHI "walimwapisha' Raila pamoja na vitisho ya Uhuru kuwa he will kill them kama watakuja uwanja wa Kamkuji "kumwapisha" Raila. Watu walipuuza kifo wakaja kwa malaki "kuuawa". Siyo Tanzania, Nyerere alitumaliza kabisa. Nenda Tanga, utamwambia Mdigo aandamane? Msambaa? Mbondei?
 
Siku za kuishi hawa wadhalimu ni chache sana.Mungu anawaona
 
Tumeshazoea hizo habari ajabu kila chaguzi mnashiriki baadae maneno hayo hayo hivyo hivyo kila mwaka hii ni kama ile hadithi ya sungura sizitaki mbichi hizi
Kwetu Zambia raisi wa sasa aligombea mara nyingi bila mafanikio ila hatimae ameshinda.
 
Wakati wa Uchaguzi watu walikuwa hawavai barakoa! Wameanza kuzivaa baada ya JPM kufariki, kwa hiyo hii siyo video ya uchaguzi bali ni "movie" tu. Huyo jamaa anayechomekea makaratasi hayo amevaa "Magwanda' na barakoa, halafu huyo mwingine aliyesimama amevaa sweta ya CHADEMA na barakoa.
 
Fake video
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…