Inadaiwa hizi video ni za wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020

Wazalendo wameanza kuachia hadharani mambo machafu yaliyotendwa kwenye kile kilichoitwa uchaguzi mkuu wa 2020 .

Toleo la sasa ni video inayoonyesha wizi wa kishamba sana wa kura ulivyofanyika , tena chini ya watu walioaminiwa kulinda usalama .

Hebu jionee mwenyewe .View attachment 1964679

Majina ya Wahusika wote yamepatikana , ila yanahifadhiwa kwa muda kwa sababu za kibinadamu
Wezi ndio wanatakiwa wajikamate, je itawezekana? Mungu alikwisha toa adhabu.
 
Tutaaminije sisi kwamba ilikuwa ni uchaguzi 2020 na kwamba wanaofanya hivyo ni kutokea chama cha kijani?

Je kama ni chama cha magwanda nao wakisuka mpango wa kuiaminisha dunia kwamba walihujumiwa? Tutaaminije sisi?
 
Wazalendo wameanza kuachia hadharani mambo machafu yaliyotendwa kwenye kile kilichoitwa uchaguzi mkuu wa 2020 .

Toleo la sasa ni video inayoonyesha wizi wa kishamba sana wa kura ulivyofanyika , tena chini ya watu walioaminiwa kulinda usalama .

Hebu jionee mwenyewe .View attachment 1964679

Majina ya Wahusika wote yamepatikana , ila yanahifadhiwa kwa muda kwa sababu za kibinadamu
Ukeumbuka na barakoa
 
Dhambi ni Mbaya,dhambi ni Mbaya saaana.Unaapa kwa Biblia na Qur'an,,laana Hiyo.
 
Unafikiri basi hizo ni siri, huo ni ubabe makusudi kwamba tunafanya hivi na hamtufanyi lolote wala kushtaki popote...
yaani CCM waiogope CHADEMA kabisa? wazee wa kupiga domo mitandaoni huku upo nyuma ya keyboard ume activate premiun vpn...
Kama Zanzibar Seif alifanyiwa kiini macho mpaka US ikaingilia na haikusaidia kitu, ndugu zangu siasa hazitowasaidia chochote, mmekwisha kwenda kushtaki hadi kwa mabeberu lakini hakuna matokeo yeyote... huwa naamini kwamba hii nchi wananchi ndio wataamua nchi iende kulia ama kushoto, hii nchi nyie CHADEMA hamtofanya lolote, zaidi bungeni mmetolewa almost wote, mmebaki kulia tu twitter na mitandaoni...
Hili taifa ni wananchi ndio watakuwa na mustakabali taifa liende wapi, tamaa zenu za fisi kumkaribisha Lowassa, wananchi wakaona hamueleweki kama sigara nyota...
CHADEMA mmekwisha, Mbowe mungu amsaidie ashinde hio kesi, yaani mmekwisha ndugu zangu hamna jipya..., mwenzenu mzee Slaa anakula huko mema ya nchi..., yule dada enu Mdee kawageuka chap..
uzuri mie sipo CCM wala CHADEMA, mie nawapa tu ukweli mchungu...
Kampeni zenu zenyewe watu walikuwa wana stream youtube na hamkufanya lolote, hakuna hata TV moja ilikuwa inaonyesha kampeni zenu, lakini wadau mmekomaa tu,katibaaaa!!!! katibaaaa!!!, tunaibiwaaa, tunaibiwaaaa, tunaibiwaaa, kila siku nyimbo ni zile zile...

Nyie komaeni tu muendelee kufukuzia hizo ruzuku, mpate hata pesa za kuweka mafuta kwenye gari... niipofika hapa niendelee tu mishe zangu hizi siasa wengine wanafanya kama hobby lakini sio userious wa kuleta mabadiliko ya kweli...

nakaribisha matusi...
Matapishi matupu!
 
La muhimu mkuu 'Erythro', ni kuzitumia hizi kama fundisho.

Kosa ni kukubali kushiriki tena kwenye uchaguzi ambao mnajuwa wazi kwamba ni "uchafuzi".

Na msidhani kwamba kwa kuwa Magufuli hayupo, hao watu wataacha tabia zao chafu. La muhimu ni kukataa upuuzi wa aina hiyo usifanyike tena.
Hata wakisusa haitawasaidia....rejea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.
 
Wazalendo wameanza kuachia hadharani mambo machafu yaliyotendwa kwenye kile kilichoitwa uchaguzi mkuu wa 2020 .

Toleo la sasa ni video inayoonyesha wizi wa kishamba sana wa kura ulivyofanyika , tena chini ya watu walioaminiwa kulinda usalama .

Hebu jionee mwenyewe .View attachment 1964679

Majina ya Wahusika wote yamepatikana , ila yanahifadhiwa kwa muda kwa sababu za kibinadamu

Yana mwisho
 
Hapana, mimi sitakutukana, ila kuna mambo umeyasema kama lawama kwa CHADEMA bila kuangalia uhalisia.

Ndiyo, CHADEMA wanastahili lawama katika mambo kadhaa ambayo hawayafanyi vizuri, na kubwa zaidi ya yote ni hilo ulilogusia kiaina..., la kuwaendea wananchi ambao ndio wenye uwezo wa kubadili mwelekeo wa nchi hii.

CHADEMA mara nyingi sana wameshauriwa wawashirikishe wananchi, kwa kuwa elimisha na kuwapa uongozi wa nini kifanywe. Juhudi zao huko ni hafifu sana, na ndiyo maana CCM huwachezea kama watoto wadogo kwa kujuwa hawana wananchi walio nyuma yao wanaoweza kuzuia michezo hiyo.

CHADEMA hawahitaji kuwa na mamilioni ya wafuasi wanaoweza kusimamia na kushinikiza mabadiliko yawepo nchini. Wakiwa na wafuasi laki tano hadi milioni moja nchi nzima waliotayari kujitoa mbele, mara moja utaona wengi wa wananchi ambao wako kimya wanaingia kwenye mstari nyuma ya hao, na mabadiliko yanakuwepo.

Kwa hiyo, lawama pekee ninayoweza kukubaliana nawe juu ya udhaifu wa CHADEMA ni huo, wa kuwa wazembe katika kuwashirikisha wananchi.

Hayo ya viongozi mamluki, kama akina Slaa, Ngoyai Lowasa, akina Nyalandu na wengine hayo ni mambo madogo sana. Chama chochote huingiza watu wenye ushawishi ili wapate madaraka.

Mwisho, ngoja nikukumbushe kama kumbukumbu zako zimefutika, au kama si ulaghai tu unaoonyesha hapa kulaumu:

CHADEMA wamewahi kuwa na wabunge wengi katika mabunge yaliyopita. Unadhani hao wabunge walipatikana kwa kufanya lelemama mbele ya uchaguzi?
Tazama mara zote walipopatikana wabunge wengi, utaona kuwa maeneo walipotokea wabunge hao watu walikuwa ngangari kulinda haki zao kuwachagua wabunge hao. Walipojaribu kufanya upuuzi wananchi walikuwa tayari kupambana.
Umeelewa vyema, ila mimi ninavyoona kwa kipindi cha awamu zilizopita hata sasa, naona hilo tatizo bado lipo, wakati wa mwenda zake, vyama vya upinzani hata kuongea na wananchi ilikuwa ngumu sana, huwezi kuongea na wananchi wakati umeambiwa usifanye mkutano. Ili uwafikie wananchi ni lazima ufanye mikutano, vyama vya upinzani wapigwa pini huku Chama tawala kikiendelea kuongea na wananchi, wapinzani kesi kibao kila siku ni kushinda mahakamani tu hadi hii leo, Tume yenyewe ndiyo hiyo inataeuliwa na Rais (Nakulipa mshahara, nakupatia usafiri halafu uje unitangazie mpinzani, hii kauli ilitolewa hadharani kila mtanzania a naye futilitilia siasa za hii nchi alisikia). Wale wote wanahusika na kusimamia UCHAGUZI ni watumishi wa umma unataka wakose mshahara watatangaza tu, ili maisha yaenelee, Unakuja kujua hapo hakuna haki, utasikia Watanzania muniombee. Sasa wewe hutendi haki tutakuombea kweli na maombi yatapokelewa kweli?
Mimi naona vyama vya upinzani wako vizuri, haki zitendekee kweli na siyo maigizo, kumbuka "AMANI NI TUNDA LA HAKI"
 
Chademaaa wazee wa kubadilisha gear angani na kuzungusha mikono.
 
Wazalendo wameanza kuachia hadharani mambo machafu yaliyotendwa kwenye kile kilichoitwa uchaguzi mkuu wa 2020 .

Toleo la sasa ni video inayoonyesha wizi wa kishamba sana wa kura ulivyofanyika , tena chini ya watu walioaminiwa kulinda usalama .

Hebu jionee mwenyewe .View attachment 1964679

Majina ya Wahusika wote yamepatikana , ila yanahifadhiwa kwa muda kwa sababu za kibinadamu

9BE6EDF3-E2A0-4F1D-8A4B-97EA3295C908.jpeg
 
Unafikiri basi hizo ni siri, huo ni ubabe makusudi kwamba tunafanya hivi na hamtufanyi lolote wala kushtaki popote...
yaani CCM waiogope CHADEMA kabisa? wazee wa kupiga domo mitandaoni huku upo nyuma ya keyboard ume activate premiun vpn...
Kama Zanzibar Seif alifanyiwa kiini macho mpaka US ikaingilia na haikusaidia kitu, ndugu zangu siasa hazitowasaidia chochote, mmekwisha kwenda kushtaki hadi kwa mabeberu lakini hakuna matokeo yeyote... huwa naamini kwamba hii nchi wananchi ndio wataamua nchi iende kulia ama kushoto, hii nchi nyie CHADEMA hamtofanya lolote, zaidi bungeni mmetolewa almost wote, mmebaki kulia tu twitter na mitandaoni...
Hili taifa ni wananchi ndio watakuwa na mustakabali taifa liende wapi, tamaa zenu za fisi kumkaribisha Lowassa, wananchi wakaona hamueleweki kama sigara nyota...
CHADEMA mmekwisha, Mbowe mungu amsaidie ashinde hio kesi, yaani mmekwisha ndugu zangu hamna jipya..., mwenzenu mzee Slaa anakula huko mema ya nchi..., yule dada enu Mdee kawageuka chap..
uzuri mie sipo CCM wala CHADEMA, mie nawapa tu ukweli mchungu...
Kampeni zenu zenyewe watu walikuwa wana stream youtube na hamkufanya lolote, hakuna hata TV moja ilikuwa inaonyesha kampeni zenu, lakini wadau mmekomaa tu,katibaaaa!!!! katibaaaa!!!, tunaibiwaaa, tunaibiwaaaa, tunaibiwaaa, kila siku nyimbo ni zile zile...

Nyie komaeni tu muendelee kufukuzia hizo ruzuku, mpate hata pesa za kuweka mafuta kwenye gari... niipofika hapa niendelee tu mishe zangu hizi siasa wengine wanafanya kama hobby lakini sio userious wa kuleta mabadiliko ya kweli...

nakaribisha matusi...
I feel you. I share your sentiment. Na mi pia ni neutral Ila kweli chadema sometimes wanazingua. Mfano mwaka unaisha Hilo Baraza kuu linakaa lini kina Mdee wa covid 19 zile appeal zao zishuulikiwe? Makes us believe kuna kamchezo kanachezwa na kutufanya Sisi mapunguawani.
Anyways as you rightly said so wananchi hua ndio waamuzi. Kwani mfano watu siku wakichoka si ni fasta tu nchi nzzima inaigia street aisee Kila mwenye madaraka ata step down bila kuambiwa.
Hapa natoa mfano wa yaliyotokea Arab Spring kule north Africa.
Ila God forbid iyo kitu isitokee kwetu.
 
Wazalendo wameanza kuachia hadharani mambo machafu yaliyotendwa kwenye kile kilichoitwa uchaguzi mkuu wa 2020 .

Toleo la sasa ni video inayoonyesha wizi wa kishamba sana wa kura ulivyofanyika , tena chini ya watu walioaminiwa kulinda usalama .

Hebu jionee mwenyewe .View attachment 1964679

Majina ya Wahusika wote yamepatikana , ila yanahifadhiwa kwa muda kwa sababu za kibinadamu
Hiyo video ilipigwa nchi nyingine siyo hapa Tanzania! Msipotoshe. Angalia vizuri.
 
Tutaaminije sisi kwamba ilikuwa ni uchaguzi 2020 na kwamba wanaofanya hivyo ni kutokea chama cha kijani?

Je kama ni chama cha magwanda nao wakisuka mpango wa kuiaminisha dunia kwamba walihujumiwa? Tutaaminije sisi?
Sisi kina nani???
 
Back
Top Bottom