Inadaiwa hizi video ni za wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020

Inadaiwa hizi video ni za wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020

Unafikiri basi hizo ni siri, huo ni ubabe makusudi kwamba tunafanya hivi na hamtufanyi lolote wala kushtaki popote...
yaani CCM waiogope CHADEMA kabisa? wazee wa kupiga domo mitandaoni huku upo nyuma ya keyboard ume activate premiun vpn...
Kama Zanzibar Seif alifanyiwa kiini macho mpaka US ikaingilia na haikusaidia kitu, ndugu zangu siasa hazitowasaidia chochote, mmekwisha kwenda kushtaki hadi kwa mabeberu lakini hakuna matokeo yeyote... huwa naamini kwamba hii nchi wananchi ndio wataamua nchi iende kulia ama kushoto, hii nchi nyie CHADEMA hamtofanya lolote, zaidi bungeni mmetolewa almost wote, mmebaki kulia tu twitter na mitandaoni...
Hili taifa ni wananchi ndio watakuwa na mustakabali taifa liende wapi, tamaa zenu za fisi kumkaribisha Lowassa, wananchi wakaona hamueleweki kama sigara nyota...
CHADEMA mmekwisha, Mbowe mungu amsaidie ashinde hio kesi, yaani mmekwisha ndugu zangu hamna jipya..., mwenzenu mzee Slaa anakula huko mema ya nchi..., yule dada enu Mdee kawageuka chap..
uzuri mie sipo CCM wala CHADEMA, mie nawapa tu ukweli mchungu...
Kampeni zenu zenyewe watu walikuwa wana stream youtube na hamkufanya lolote, hakuna hata TV moja ilikuwa inaonyesha kampeni zenu, lakini wadau mmekomaa tu,katibaaaa!!!! katibaaaa!!!, tunaibiwaaa, tunaibiwaaaa, tunaibiwaaa, kila siku nyimbo ni zile zile...

Nyie komaeni tu muendelee kufukuzia hizo ruzuku, mpate hata pesa za kuweka mafuta kwenye gari... niipofika hapa niendelee tu mishe zangu hizi siasa wengine wanafanya kama hobby lakini sio userious wa kuleta mabadiliko ya kweli...

nakaribisha matusi...
Stress zitakuua. Tafuta hela ndugu usipate presha bure.

Ukitarajia Chadema ikishinda utamaliza matatizo yako ya nyumbani?

Chadema tunatafuta haki, uhuru na amani. Maendeleo ni wajibu wa mtu mmoja mmoja.
 
Nyie komaeni tu muendelee kufukuzia hizo ruzuku, mpate hata pesa za kuweka mafuta kwenye gari... niipofika hapa niendelee tu mishe zangu hizi siasa wengine wanafanya kama hobby lakini sio userious wa kuleta mabadiliko ya kweli...
Hivi nyie UVCCM kwa nini akili zenu hazinaga akili?! Wenyewe mnawaza TEUZI na RUZUKU tu .
 
Wazalendo wameanza kuachia hadharani mambo machafu yaliyotendwa kwenye kile kilichoitwa uchaguzi mkuu wa 2020 .

Toleo la sasa ni video inayoonyesha wizi wa kishamba sana wa kura ulivyofanyika , tena chini ya watu walioaminiwa kulinda usalama .

Hebu jionee mwenyewe .View attachment 1964679

Majina ya Wahusika wote yamepatikana , ila yanahifadhiwa kwa muda kwa sababu za kibinadamu
.
 
Wazalendo wameanza kuachia hadharani mambo machafu yaliyotendwa kwenye kile kilichoitwa uchaguzi mkuu wa 2020 .

Toleo la sasa ni video inayoonyesha wizi wa kishamba sana wa kura ulivyofanyika , tena chini ya watu walioaminiwa kulinda usalama .

Hebu jionee mwenyewe.

View attachment 1964679

Majina ya Wahusika wote yamepatikana , ila yanahifadhiwa kwa muda kwa sababu za kibinadamu
Halafu watu wanasema wamekula kiapo, Mungu hadhihakiwi
 
Stop this nonsense, siyo Tanzania, watu tunaogopa sana, watu tu waoga sana tena sana wa KUFA. Hakuna aliyetayari kufa. Mpaka hapo woga utakapo tutoka ndipo tutaona mabadiliko makubwa. Kenya WANANCHI "walimwapisha' Raila pamoja na vitisho ya Uhuru kuwa he will kill them kama watakuja uwanja wa Kamkuji "kumwapisha" Raila. Watu walipuuza kifo wakaja kwa malaki "kuuawa". Siyo Tanzania, Nyerere alitumaliza kabisa. Nenda Tanga, utamwambia Mdigo aandamane? Msambaa? Mbondei?
Mkuu "Retired', umeanza vibaya kwa hayo maneno "Stop this nonsense". I never indulge in nonnsense, and you should drill that into your head before you respond to me.

Kuhusu hayo mengine uliyoandika hapo chini, siyo kwewli.

Kinachokosekana ndani ya wananchi ni moto wa kuamsha mori wao, kukataa ukandamizi na unyanyasaji wanaofanyiwa.

Ninapoandika kuhusu watu laki tano, hawa ni watu ambao wameelimishwa na kutambua heshima ya HAKI zao.
Hakuna ujasiri au woga kwenye kujitoa maisha, na siyo kila jambo lazima liishie kwenye kifo.

Watu wanaogopa hata kuwekwa mahabusu kwa sababu ya kutafuta haki zao? Huo ni woga? Hapana, ni kukosa uongozi wa kuamsha hisia za watu wasimamie haki wanazoporwa.
Kuna mahabusu ya kuwaweka watu milioni moja kwa wakati mmoja ndani ya nchi hii na ikabaki bado tunajiamini kwamba tuko sawa?

CCM wamechukuwa udhaifu wa CHADEMA kutoweza kuwaongoza watu waliotayari kudai haki zao, na kuutumia udhaifu huo kuendeleza vitisho kwa raia wote ambao hawana msisimko wowote wa kukataa vitisho hivyo. Huu siyo woga.
 
Ni kweli mkuu na upo sahihi kabisa, lakini suala la kukaribisha mtu, si mtu yeyote tu, lazima kuwe na utaratibu maalumu,vigezo na pia kusimamia msimamo wenu no matter what.., kumkaribisha mtu mliyemuita fisadi no 1, then baadae mnamkaribisha tena agombee uraisi kupitia tiketi ya chama chenu hio imekaaje?
hapo totally walivuruga kila kitu, huwezi shirikisha wananchi kwenye upuuzi kama huo wakuelewe, ujue katika kila jambo lenye manufaa na ili lizae matunda ni lazima ujue kuna taratibu za kufuata na miiko yake, kwa hio usi base tu kufuata taratibu lazima pia ujue miiko, kama utafuata vyote hautofanikiwa... hata kama unashirikisha wananchi bado haitoshi kama unashindwa kusimamia misimamo yako na kufuata taratibu na miiko kisa tamaa...
Mkuu, bado hatuelewani hata kidogo.

Kumpokea Lowassa haiwezi kamwe kuwa sababu kwa nini CHADEMA haikufanya vizuri katika uchaguzi. Kutumia haoja hiyo kuwa ndiyo imeifanya CHADEMA kukosa ufanisi ni kurahisisha uwezo wa kuchambua hoja.

Na usije hapa na kunilaumu kwamba sijui maana na umuhimu wa sera wanazotakiwa kuzisimamia CHADEMA kama chama; kiasi kwamba wanazisahau wanapoingiza watu kama hao uliowataja.

Lengo hapa ni kupata kura nyingi katika uchaguzi na ikiwezekana kushinda uchaguzi kabisa. Kuna chama chochote cha siasa kisichotaka kufanya hivyo?
 
Wazalendo wameanza kuachia hadharani mambo machafu yaliyotendwa kwenye kile kilichoitwa uchaguzi mkuu wa 2020 .

Toleo la sasa ni video inayoonyesha wizi wa kishamba sana wa kura ulivyofanyika , tena chini ya watu walioaminiwa kulinda usalama .

Hebu jionee mwenyewe.

View attachment 1964679

Majina ya Wahusika wote yamepatikana , ila yanahifadhiwa kwa muda kwa sababu za kibinadamu
mbaya zaidi wanaotumika kufanya huo wizi ni walewale watuhumiwa wa siku zote, jeshi la polisi.
 
Hata wakisusa haitawasaidia....rejea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.
"Hata wakisusa...*. Kususia uchaguzi ni UPUMBAVU. Werevu ni KUZUIA kwa njia zozote ziwezekanazo 'uchafuzi' usifanyike. Hii ndiyo njia pekee iliyobakia CHADEMA waifanye kama haiwezekani kuwepo Tume Huru ya Uchaguzi.
 
Kama muda wa kuandaa wagombea haupo wanaishia kukodishwa muda wa kufuatilia vitu vya msingi kama kura unatoka wapi

Kufeli kwa upinzani ni kwa kujitakia

Huwezi toa jibu hilo kila mtihani nanukafeli na bado likawa ndio jibu lako
Anayejua mazingira ya chaguzi za Tanzania hili halimuumizi kichwa.
 
Umeelewa vyema, ila mimi ninavyoona kwa kipindi cha awamu zilizopita hata sasa, naona hilo tatizo bado lipo, wakati wa mwenda zake, vyama vya upinzani hata kuongea na wananchi ilikuwa ngumu sana, huwezi kuongea na wananchi wakati umeambiwa usifanye mkutano. Ili uwafikie wananchi ni lazima ufanye mikutano, vyama vya upinzani wapigwa pini huku Chama tawala kikiendelea kuongea na wananchi, wapinzani kesi kibao kila siku ni kushinda mahakamani tu hadi hii leo, Tume yenyewe ndiyo hiyo inataeuliwa na Rais (Nakulipa mshahara, nakupatia usafiri halafu uje unitangazie mpinzani, hii kauli ilitolewa hadharani kila mtanzania a naye futilitilia siasa za hii nchi alisikia). Wale wote wanahusika na kusimamia UCHAGUZI ni watumishi wa umma unataka wakose mshahara watatangaza tu, ili maisha yaenelee, Unakuja kujua hapo hakuna haki, utasikia Watanzania muniombee. Sasa wewe hutendi haki tutakuombea kweli na maombi yatapokelewa kweli?
Mimi naona vyama vya upinzani wako vizuri, haki zitendekee kweli na siyo maigizo, kumbuka "AMANI NI TUNDA LA HAKI"
Mkuu 'SOSDANNY', sikatai wala sikusahau mazuio wanayowekewa vyama vya upinzani kuwafikia wananchi, hasa kupitia kwenye mikutano.

Mikutano ya hadhara ni njia moja tu ya kuwafikia wananchi, na kwa hakika ni kama njia ya mwisho kabisa ya kujumuisha, baada ya kuwa na wananchi mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo huko mitaani na kwenye mashina.

Hii ndiyo kazi ngumu, lakini muhimu sana wanayotakiwa kuifanya CHADEMA.

CCM na ubovu wao wote, bado wanavuna matunda kutokana na juhudi zilizofanywa huko miaka ya nyuma, iliyokiwezesha hicho chama kujitanua hadi huko chini kwa wananchi mitaani.

Kwa hiyo, swala la mikutano ya hadhara, pamoja na umuhimu wake katika kuwasiliana na wananchi, si njia pekee, na wala siyo njia muhimu zaidi ya kueneza mambo ya chama kwa wananchi na wanachama wao.
 
Mkuu "Retired', umeanza vibaya kwa hayo maneno "Stop this nonsense". I never indulge in nonnsense, and you should drill that into your head before you respond to me.

Kuhusu hayo mengine uliyoandika hapo chini, siyo kwewli.

Kinachokosekana ndani ya wananchi ni moto wa kuamsha mori wao, kukataa ukandamizi na unyanyasaji wanaofanyiwa.

Ninapoandika kuhusu watu laki tano, hawa ni watu ambao wameelimishwa na kutambua heshima ya HAKI zao.
Hakuna ujasiri au woga kwenye kujitoa maisha, na siyo kila jambo lazima liishie kwenye kifo.

Watu wanaogopa hata kuwekwa mahabusu kwa sababu ya kutafuta haki zao? Huo ni woga? Hapana, ni kukosa uongozi wa kuamsha hisia za watu wasimamie haki wanazoporwa.
Kuna mahabusu ya kuwaweka watu milioni moja kwa wakati mmoja ndani ya nchi hii na ikabaki bado tunajiamini kwamba tuko sawa?

CCM wamechukuwa udhaifu wa CHADEMA kutoweza kuwaongoza watu waliotayari kudai haki zao, na kuutumia udhaifu huo kuendeleza vitisho kwa raia wote ambao hawana msisimko wowote wa kukataa vitisho hivyo. Huu siyo woga.
1. I am sorry for the inconveniences so caused to you by the unfriendly salute used. Sorry! apology
2. All what you have narrated above boil to one conclusion: if people are not ready to face the wrath of brutal police expect nothing from them in terms of liberation struggle! Nimetoa mfano wa Kenya, wamekufa wengi ndiyo Katiba na adabu vikawa realised from dictators in Kenya!
3. Chadema is not weak, had it been that CDM is weak as you brand it, it would have long ago been erased from the political parties register book!
4. Can you suggest some modalities to be put in place by CDM to lead or let me put it in a harsh language, INCITE those ready to demand their political rights from our rulers?
 
To be honest, tangu 2010 CCM hawajashinda uchaguzi. Tanzania mshindi anaamuliwa na Mwenyekiti wa Tume na akina Mahela wale....!!
 
Unafikiri basi hizo ni siri, huo ni ubabe makusudi kwamba tunafanya hivi na hamtufanyi lolote wala kushtaki popote...
yaani CCM waiogope CHADEMA kabisa? wazee wa kupiga domo mitandaoni huku upo nyuma ya keyboard ume activate premiun vpn...
Kama Zanzibar Seif alifanyiwa kiini macho mpaka US ikaingilia na haikusaidia kitu, ndugu zangu siasa hazitowasaidia chochote, mmekwisha kwenda kushtaki hadi kwa mabeberu lakini hakuna matokeo yeyote... huwa naamini kwamba hii nchi wananchi ndio wataamua nchi iende kulia ama kushoto, hii nchi nyie CHADEMA hamtofanya lolote, zaidi bungeni mmetolewa almost wote, mmebaki kulia tu twitter na mitandaoni...
Hili taifa ni wananchi ndio watakuwa na mustakabali taifa liende wapi, tamaa zenu za fisi kumkaribisha Lowassa, wananchi wakaona hamueleweki kama sigara nyota...
CHADEMA mmekwisha, Mbowe mungu amsaidie ashinde hio kesi, yaani mmekwisha ndugu zangu hamna jipya..., mwenzenu mzee Slaa anakula huko mema ya nchi..., yule dada enu Mdee kawageuka chap..
uzuri mie sipo CCM wala CHADEMA, mie nawapa tu ukweli mchungu...
Kampeni zenu zenyewe watu walikuwa wana stream youtube na hamkufanya lolote, hakuna hata TV moja ilikuwa inaonyesha kampeni zenu, lakini wadau mmekomaa tu,katibaaaa!!!! katibaaaa!!!, tunaibiwaaa, tunaibiwaaaa, tunaibiwaaa, kila siku nyimbo ni zile zile...

Nyie komaeni tu muendelee kufukuzia hizo ruzuku, mpate hata pesa za kuweka mafuta kwenye gari... niipofika hapa niendelee tu mishe zangu hizi siasa wengine wanafanya kama hobby lakini sio userious wa kuleta mabadiliko ya kweli...

nakaribisha matusi...
Wenye hasara si CHADEMA. Wao maisha yao yanapeta tu. Ndio njia waliyochagua. Akina Mbowe, Lissu, Sugu, Heche ... maisha yao yanaendelea with clear conscience.

Wananchi ndio wanapewa message mubashara: KURA ZENU HAZINA MAANA YOYOTE; simameni juani siku nzima kusubiri kupiga kura lakini machaguo yenu ni ujinga mtupu, sisi CCM tunaunda serikali jinsi tunavyotaka. Kushiriki kwenu zoezi la uchaguzi ni kielelezo cha jinsi mlivyokuwa mazuzu.

Usihangaike na CHADEMA. Hata Kristo aliwaambia msinililie mimi bali ... Luka 23:28. Kama Watanzania hawaoni tabu kusherehekea dharau hiyo dhidi yao, hatuna haja ya kujisumbua na mambo ya CHADEMA. Wale ni watu binafsi waliochagua njia yao. Hawatuhusu. Kila mtu ajijue mwenyewe.
 
Back
Top Bottom