Wakana Mungu wana hila sana huo uzushi siyo kwa Lazaro tu hata Yesu wanadai hakufa na hiyo hata leo wapo wanao amini hivyo.
mfano kuna andiko hili:
Mathayo 27
62 Hata siku ya pili, ndiyo iliyo baada ya Maandalio, wakuu wa makuhani, na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato,
63 wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa akali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka.
64 Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza.
65 Pilato akawaambia, Mna askari; nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo.
66 Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi.
Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.
Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji.
Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu.
BAADA YA YESU KUFUFUKA NA ASKARI WALISHUHUDIA YOTE
11 Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka.
12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi,
13 wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala.
14 Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.
15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo.