Tetesi: Inadaiwa Makumi ya Askari jeshi wa SADC watekwa Congo na kupelekwa Kigali

Imekuwaje kuwaje mpaka wakatekwa na kuluna, wakati wao wanapata mafunzo yote, silaa wanazo, na wanalipwa vizuri mishahara na posho?​
... hamna kazi mbovu kama kulinda amani, ... masharti yake yanawanyima kabisa uhuru wa kupigana wanajeshi wetu na muda mwingi wanafanywa 'human shields' na majeshi hasimu!
 
... jeshi ni team work, nidhamu na kutii amri kutoka juu bila shuruti! ... kazi ya kutunza amani ni sawa na kuwa refa wa ngumi, haupigani lakini ukizubaa unadundwa na mahasimu!
 
Hv h
Hv huwa mnafuatulia hz habari ambazo watu wote tunafuatilia ama mna habari zenu binafsi mnazofuatiliaga. Yaani saa zingine mpaka naona aibu jinsi tulivyo na ujinga mwingi
 
Goma kwa sasa ni kama kisiwa. M23 wamezunguka pande zote. Njia pekee ya jeshi kutoroka/kuretreat ni kwenda Rwanda. So majeshi yakienda Rwanda haimaanishi yametekwa na kupelekwa kwa PK. Ni kwamba yanaenda huko kujiokoa.

Hata hivyo wanaopigana Goma mpaka sasa ni wanaume hasa. Waasi wamewazunguka pande zote lakini bado wamo.
 
Kakwambia nani?

Unajua mission ngapi Jwtz inashiriki?

Wabongo mbona mnalodharau sana jeshi lenu?

Au kwa vile mnaona mnazunguka nchini mwenu bila bughudha basi mnaongea vyovyote mnavyojisikia?
Hawawezi kitu mkuu, labda kufanya usafi tu na kuzuia chadema wasiandamane. Basi
 
Mambo yanayo tokea katika uwanja wa Vita ni tofauti kubwa na unayo sikia katika vyombo vya habari.
Ni Ngumu kuamini mamia ya askari wamekufa alafu taarifa zinafichwa wakati miili itarudi makwao kwaajili ya Mazishi.
 
Unaonekana una akili za zamani sana. Wewe ni mzee kiufupi
Unajua kipindi cha vita ya idd Amin, walikufa wanajeshi wangapi wa Tanzania?
Kwenye vita, vifo sio kitu cha ajabu ni kawaida sana.
Kipindi kile ilikuwa bahati tu maana Idd Amin hakuwa kiongozi mwema hata wananchi wake walitaka aondeke (walimchoka). Unafikiri Idd Amin angekuwa kiongozi mzuri unafikiri JWTZ wangeweza kushinda vita?
Kwa nini wasingeweza? Hata hivyo vita sio mashindano kama Simba vs Yanga. Motive behind ndo silaha kubwa.
Hapo Congo unajua wanajeshi wangapi wa Tanzania wamekufa mpaka sasa?
Mwaka juzi kama sikosei kuna wanajeshi wa Tanzania waliletwa kwenye majeneza.
Hiyo ni kawaida sana kwenye vita yoyote ile - usishangae.
Kwahiyo kwa vita ile Nyerere aliwaaminisha kuwa vita ni rahisi? Kule Congo tayari kuna wanajeshi wa Tanzania, wamefanya nn mpaka sasa?
Wanajeshi wa Tz waliopo huko ni kwa ajili ya kulinda Amani na sio kwa ajili ya kupambana.
Vita sio kitu kirahisi kama inavyotamkwa - naelewa hilo. Lakini ikiwepo sababu madhubuti ya kupigana vita e.g. ile ya Kagera, Ushindi unapatikana japokuwa sio kirahisi. Hata ile ya Kagera haikuwa rahisi kivile.
Sioni kama kuna sababu yenye maslahi kwa Tz ya kuingia vitani dhidi ya M23 ndani ya Congo DRC. Mambo ya siasa waachie wanasiasa wanajua zaidi.
 
Basi imetosha sitaki kuongea tena iishe km ilivyoisha ila nimeeleweeka ingawa sijamaanisha ukivyomaanisha sijafikiri km ulivyofikiri tumetofautiana kimtazamo ulichokiona sicho nilichokiona nilichokisema sicho nilichomaanisha, tafakari
Kongole mkuu. Umeonesha ukomaavu wa akili. Ur one among the GTs hapa Jf.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…