Tetesi: Inadaiwa Wakili Peter Madeleka amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa Serena Hotel

Kama sijakosea nadhani huyu mtu atakuwa anakamatwa hii mara ya pili, watamsumbua kama kawaida yao halafu wamuachie.
 
Mleta mada ungeweka sababu za kukamatwa ungeonekana akili zako kichwani zimo kwa uandishi ulioandika unaonyesha kichwa chako nusu kaputi na umo jamiiforums kwa bahati mbaya sio kama great thinker
Sasa mleta mada azitoe wapi sababu kama polisi waliomkamata hawajasema?

Au mleta mada ni mpiga ramli?
 
Siku chache zilizopita alisema kuna njama za kumuua zikiratibiwa na maafisa uhamiaji.Na akatoa screenshot ya mjadala.Inawezekana likawa hilo.Hata hivyo huyu ni ex Police officer na mwanasheria,ni uji unaunguzana na bakuli.
 
Ficha ujinga wako
 
Mnasotesha watu miezi na miezi rumande halafu mnawaachia kwa kukosa ushahidi. Mnakuwa mmekwishawatesa na kuwapotezea muda wao bila hatia (Ref: Mbowe na ugaidi wa kubumba).
SASA KAMA ANAKOSA ASIKAMATWE YEYE NI NANI? ACHENI UHUNI WENU ITAJULKIKANA ALIKOSEA WAPI AU TAYARI MMESHAJUWA KAKAMATWA KWAKOSA GANI?
 
Unataka kuficha utekaji kwa sababu tu wanaccm hawatekwi ?
 
Kwahiyo mtu akikamatwa unataka watu wasitoe taarifa acheni u much know.
 
Wewe una Akili kuliko Moderators wa Jamiiforums? Acha Kujipendekeza, Kuwafundisha Kazi na kuwa na Kiherehere sawa? Haya Uzi ndiyo huo uko Kurasa ( Page ) ya Tatu ( 3 ) sasa je, unasemaje?
 
Askari wa uhamiaji na polisi ni walewale wanufaika wa mfumo kandamizi wa Magufuli. Wote walipiga sana pesa Kipindi cha mwendazake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…