Inafikirisha: Miujiza ya Mchungaji Mwamposa

Inafikirisha: Miujiza ya Mchungaji Mwamposa

Nimebahatika kuona vipindi kadhaa vya mchungaji Mwamposa.

Yawezekana ukimtoa Yesu (Kwenye ukristo) kiumbe mwenye kufanya miujiza mingi hapa duniani anaweza kuwa huyu Mchungaji.

Sitaki kuhukumu kama ni mkweli au Lah, ila kwa wanaoshuhudia kwenye vipindi vyake anaweza vunja rekodi.

Nadhani ile miujiza ya Yesu ya uponyaji huyu mchungaji ataivunja rekodi zake, isipokuwa Kulisha watu 5000 ambao walikula na kusaza na kufufuka kwa yesu.

Kuna yoyote amepatwa na muujiza wa Mwamposa haswa uponyaji humu?
Wajinga ndiyo waliwao.

Biblia inasema:

... watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza,...
 
Niko Morogoro sijawahi kwenda Kawe ili kupitia maombi ya usiku na mafuta nimepona vidonda vya tumbo,nimeiokoa familia yangu hasa uzazi kwa mama watoto,amini utaona
Nguvu za Mungu zinafanya kazi
 
Yes ni aina ya utapeli kwa maana wanaifanikiwa ni wachahce.
Na wale wachache inatumika nguvu kubwa kuwatangaza.
Hivyo pia wagalatia yawapasa kuzinduka.
Shetani anaitawala tasnia,amekuwa mtenda miujiza.
Sio kwa wagalatia tu pale wavaa madela ni wengi sana
 
Nimebahatika kuona vipindi kadhaa vya mchungaji Mwamposa.

Yawezekana ukimtoa Yesu (Kwenye ukristo) kiumbe mwenye kufanya miujiza mingi hapa duniani anaweza kuwa huyu Mchungaji.

Sitaki kuhukumu kama ni mkweli au Lah, ila kwa wanaoshuhudia kwenye vipindi vyake anaweza vunja rekodi.

Nadhani ile miujiza ya Yesu ya uponyaji huyu mchungaji ataivunja rekodi zake, isipokuwa Kulisha watu 5000 ambao walikula na kusaza na kufufuka kwa yesu.

Kuna yoyote amepatwa na muujiza wa Mwamposa haswa uponyaji humu?

Pumbavu kabisa hata Biblia huijui
 
Hamna muujiza zaid ya kuombea hadi yanga ishinde nd muujiz pekee nilion ulitimia
1684236229811.jpg
 
Niko Morogoro sijawahi kwenda Kawe ili kupitia maombi ya usiku na mafuta nimepona vidonda vya tumbo,nimeiokoa familia yangu hasa uzazi kwa mama watoto,amini utaona
Nguvu za Mungu zinafanya kazi
Acha kuwachota watu akili wewe una matatizo ya akili, maluweluwe yamekujaa

Jana nilikua kwenye kubadirisha frequency nikaingia hio radio ya Mwamposa kuna wimbo wa dini niliukuta nikastop nisikilize wa Paul Clement, sasa nilipomaliza ndio zikaja shuhuda Wala sikua na lengo nilichostaajabu ni kwamba kuna jamaa alikua anatoa shuhuda alafu yule anaemwambia ashuhudie akawa anacheka vibaya sana maana kwa akili ya kawaida tu alibaini kwamba ule ushuhuda ni UONGO
 
Mimi binafsi imenitokea muujiza wakati naangalia tv yake tena nilitumia maji ya kununua dukani ,cha msingi imani yako itakuponya

hapa ndio shida inapoanzia... usipoponyeka utaambiwa huna imani..
 
Mimi nilitapika wembe na kunya jongoo mzima. Nikapona tezi dume.
Ndio yale yale ya maji kubadirika rangi tofauti tofauti unapoweka miguu yanaitwa maluweluwe hii kitu kuna jamaa walikua wanaonyesha jinsi inavyofanya kazi wale wazee wa mazingaombwe mtu anakunya muhindi wa kuchoma bila kujielewa hio ipo

Kuna kipindi Clouds TV kilionyeshwa Sizi Kitaa jamaa wawili walikua wanaonyesha jinsi wanavyoweza kula ugali kwa misumari inch 2/3 na mwingine akala ugali na viwembe vya kutosha live live on TV kitu ambacho Mwamposa hajawahi kutuonyesha mtu katema kiwembe sijui kanya boga mwingine kanya Muhogo video reality hakuna ni maneno tu ya UONGO UONGO kuwachota watu akili

Kwa hio wewe umepatwa na maluweluwe sio kosa lako ushachezeshwa mazingaombwe unaona maluweluwe tu, km unabisha Mwamposa sio mponyaji mwambie aende Muhimbili au Amana akawanyanyue wale wagonjwa mahututi pale wapone km yeye anatenda miujiza, sio hizo za kutema kokoto, sijui nimetema kokwa, mwingine nimetema uzi, Mara ooh nimetema nywele na kipande Cha mkaa, ujinga mtupu
 
Niko Morogoro sijawahi kwenda Kawe ili kupitia maombi ya usiku na mafuta nimepona vidonda vya tumbo,nimeiokoa familia yangu hasa uzazi kwa mama watoto,amini utaona
Nguvu za Mungu zinafanya kazi
Mkuu mafuta uliyapataje? Na hujawahi kwenda laws?
 
Ni kweli mwamposa anafanya miujiza, ila source ya nguvu zake ni wapi??
Miujiza ya kutema viwembe sijui kutema uzi ndio miujiza, hujawahi hudhuria show za mazingaombwe mtu anatemeshwa hivyo vitu live live live kwenye mazingaombwe, miujiza km kweli yeye anayo akawaponye wagonjwa mahospitalini wapone wote watembee wakiwa na afya tele sio kujifanya anatemesha watu matutu kisha anapata pesa za ubwete, wenye akili hawawezi kukubariana nae ile sio miujiza ita maluweluwe au mazingaombwe
 
Back
Top Bottom