Inafikirisha: Miujiza ya Mchungaji Mwamposa


Mkuu najua mantic yako ya huu uzi (sarcasm ) ,ila inafikirisha inakuwaje Mwamposa amzidi yesu kwa miujiza 😀 ? Yaani ni kweli amebakiza kulisha watu elfu 5 tu kwa kugeuza mikate mitano na kuwa elfu 5 ila cha kushangaza yeye ndiyo anawauzia mikate(Keki,Biscuit) na maji kwa bei ya juu badala ya kugawa bure.
 
Mwamposa ni retailer mkubwa wa maji hapa Dar tena kwa bei anayopanga yeye. Bila control baada ya miaka 10 kila nyumba itakua na nabii.

Kweli kabisa baada ya uboda boda, unabii unaweza kufuata. Maana kila kijana anataka aitwe nabii au mtume na aogopwe na kutetemekewa.
 
Acheni propaganda. Maelfu gani unaongelea?. Yule akija Dodoma watoa ushuhuda wanakuwa watu wa shinyanga na akienda Tabora watoa ushuhuda wa musoma na kahama. Sio wa hapo hapo. Tuache kutumika na shetani hukumu yake ni mbaya Sana.
Ikifika zamu ya kwenda Shakahola 😂 watakwenda wote🚶🚶
 
Niko Morogoro sijawahi kwenda Kawe ili kupitia maombi ya usiku na mafuta nimepona vidonda vya tumbo,nimeiokoa familia yangu hasa uzazi kwa mama watoto,amini utaona
Nguvu za Mungu zinafanya kazi

Kwa hivyo mafuta ndio yamekuponya?.
 

Halafu Kuna shuhuda zingine kwa Hali ya kawaida ni uongo. Kwa mfano mtu anasema alikuwa anadaiwa milioni tano lakini tangu ananunue maji na kuyamwaga kwenye eneo lake la biashara ameweza kurejesha milioni tano na kunenga nyumba kubwa ya vyumba kumi ndani ya mwaka mmoja.
 
Hata mimi nilikuwa siamini lakini naamini kwa sababu tatizo lililokuwa linanisumbua miaka mingi limeisha
 
Acheni propaganda. Maelfu gani unaongelea?. Yule akija Dodoma watoa ushuhuda wanakuwa watu wa shinyanga na akienda Tabora watoa ushuhuda wa musoma na kahama. Sio wa hapo hapo. Tuache kutumika na shetani hukumu yake ni mbaya Sana.

Hawa manabii hawajawahi hata siku moja kumponya mlemavu ambaye anafahamika tangia utoto mlemavu...wao wanawaponya waigizaji wao tu (Set Up).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…