Inafikirisha: Miujiza ya Mchungaji Mwamposa

Inafikirisha: Miujiza ya Mchungaji Mwamposa

Nimebahatika kuona vipindi kadhaa vya mchungaji Mwamposa.

Yawezekana ukimtoa Yesu (Kwenye ukristo) kiumbe mwenye kufanya miujiza mingi hapa duniani anaweza kuwa huyu Mchungaji.

Sitaki kuhukumu kama ni mkweli au Lah, ila kwa wanaoshuhudia kwenye vipindi vyake anaweza vunja rekodi.

Nadhani ile miujiza ya Yesu ya uponyaji huyu mchungaji ataivunja rekodi zake, isipokuwa Kulisha watu 5000 ambao walikula na kusaza na kufufuka kwa yesu.

Kuna yoyote amepatwa na muujiza wa Mwamposa haswa uponyaji humu?

Mkuu najua mantic yako ya huu uzi (sarcasm ) ,ila inafikirisha inakuwaje Mwamposa amzidi yesu kwa miujiza 😀 ? Yaani ni kweli amebakiza kulisha watu elfu 5 tu kwa kugeuza mikate mitano na kuwa elfu 5 ila cha kushangaza yeye ndiyo anawauzia mikate(Keki,Biscuit) na maji kwa bei ya juu badala ya kugawa bure.
 
Mwamposa ni retailer mkubwa wa maji hapa Dar tena kwa bei anayopanga yeye. Bila control baada ya miaka 10 kila nyumba itakua na nabii.

Kweli kabisa baada ya uboda boda, unabii unaweza kufuata. Maana kila kijana anataka aitwe nabii au mtume na aogopwe na kutetemekewa.
 
Acheni propaganda. Maelfu gani unaongelea?. Yule akija Dodoma watoa ushuhuda wanakuwa watu wa shinyanga na akienda Tabora watoa ushuhuda wa musoma na kahama. Sio wa hapo hapo. Tuache kutumika na shetani hukumu yake ni mbaya Sana.
Ikifika zamu ya kwenda Shakahola 😂 watakwenda wote🚶🚶
 
Niko Morogoro sijawahi kwenda Kawe ili kupitia maombi ya usiku na mafuta nimepona vidonda vya tumbo,nimeiokoa familia yangu hasa uzazi kwa mama watoto,amini utaona
Nguvu za Mungu zinafanya kazi

Kwa hivyo mafuta ndio yamekuponya?.
 
Miujiza ya kutema viwembe sijui kutema uzi ndio miujiza, hujawahi hudhuria show za mazingaombwe mtu anatemeshwa hivyo vitu live live live kwenye mazingaombwe, miujiza km kweli yeye anayo akawaponye wagonjwa mahospitalini wapone wote watembee wakiwa na afya tele sio kujifanya anatemesha watu matutu kisha anapata pesa za ubwete, wenye akili hawawezi kukubariana nae ile sio miujiza ita maluweluwe au mazingaombwe

Halafu Kuna shuhuda zingine kwa Hali ya kawaida ni uongo. Kwa mfano mtu anasema alikuwa anadaiwa milioni tano lakini tangu ananunue maji na kuyamwaga kwenye eneo lake la biashara ameweza kurejesha milioni tano na kunenga nyumba kubwa ya vyumba kumi ndani ya mwaka mmoja.
 
Hata mimi nilikuwa siamini lakini naamini kwa sababu tatizo lililokuwa linanisumbua miaka mingi limeisha
 
Acheni propaganda. Maelfu gani unaongelea?. Yule akija Dodoma watoa ushuhuda wanakuwa watu wa shinyanga na akienda Tabora watoa ushuhuda wa musoma na kahama. Sio wa hapo hapo. Tuache kutumika na shetani hukumu yake ni mbaya Sana.

Hawa manabii hawajawahi hata siku moja kumponya mlemavu ambaye anafahamika tangia utoto mlemavu...wao wanawaponya waigizaji wao tu (Set Up).
 
Back
Top Bottom