Ndo utwambie ww sababu za kumfukuza ni zipi km anapotosha tupe mwanga ww
Ila kwa weng kufukwazwa kwa gamondu ni km kukurupuka tu kwa viongozi na mashabiki wanaotaka furaha toka kwenye mpira wakat furaha inapatikana tkt vtu vingi tu
Kwani mpira unachezwa chumbani? Mpira ni mchezo wa wazi kila mtu anaona.
1) mambo ya nje ya uwanja.
Hapa kuna mambo ya starehe, kocha ni mtu wa starehe sana na ikapelekea wachezaji nao kuwa watu wa starehe. Azizi Ki na wenzie starehe ya kwenda klabu kwa sana. Kama tu kocha mtu wa bata ni nani atasimamia nidhamu?
Ukiachana na starehe, Gamondi ana asili ya ujeuri na ubinafsi. Haangalii maslahi ya timu bali ni misimamo yake yeye ndio kila kitu. Kuna mtu professional kaachwa kisa Gamondi.
Sifa zilizidi mno jambo ambalo liliua hali ya upambanaji kwa wachezaji wa Yanga. Ukiangalia msimu uliopita uchezaji wa Yanga ulibebwa na morali kubwa ya wachezaji kuwa na kiu ya kupata magoli mengi. Ukifungwa goli la mapema aisee umeisha, hesabia goli 3+ ila angalia msimu huu hata timu ipate goli kipindi cha kwanza unaweza kukuta mpira ukaisha kwa goli hilo hilo moja. Timu iko pungufu lakini vigoli ndio hivyo hivyo hiyo yote ni kutokana na wachezaji kuridhika.
Ukisikiliza press ya Gamondi yeye ni kujisifia na kusifia timu yake pamoja na wachezaji wake kuwa ni bora, hapa anaua morali ya timu na wachezaji wanakuwa ni watu wa ku relax.
2) mambo ya ndani ya uwanja.
Hapa kuna ishu ya upangaji wa kikosi na mbinu zake za mpira.
Tuanze na upangaji wa timu, Yanga ina utitiri mkubwa sana wa wachezaji wenye kufanana ubora japo hawalingani ila sio timu ya kushindwa kuifanyia rotation na ukapata matokeo mazuri kwa timu zilizo daraja la kati na daraja ya chini.
Gamondi kikosi ni hiko hiko, yeye na Aziz Ki, Azizi Ki na yeye wakati ana watu wengi tu kwenye kikosi.
Angalia Mkude yule aliyekiwasha dhidi ya Mamelodi, je Mkude yule yuko wapi? Mtasema haingii kwenye mfumo wa Gamondi, lakini je mbona anapopewa nafasi ya kucheza huwa anauwasha ipasavyo?
Msimu huu kaletewa bonge la kiraka, Abuya aisee huyu jamaa ni mali haswa lakini Gamondi anashindwa kumpa nafasi. Mechi ya Tabora kaona hana mabeki na Kibwana yupo benchi ila kaona bora Aucho akawe beki kuliko Kibwana kucheza.
Tunaona sura ni zile zile kila mechi halafu sura zenyewe zingine zinaonesha kuchoka zingine zinaonesha kushuka viwango lakini yeye kakomaa nao. Kushinda goli moja moja ilikuwa ni dalili ya kushuka kwa timu wala sio kukamiwa. Msimu uliopita timu zilikuwa zinakuja kwa kukamia na kupaki basi lakini walikuwa wanalazimishwa kufanya makosa kwa kupelekewa moto mwanzo mwisho kwa kasi na ukiruhusu goli umekwisha.