Inakuaje maofisini huku msomi ana Masters ila hajui kuandikia mradi

Inakuaje maofisini huku msomi ana Masters ila hajui kuandikia mradi

Inashangaza unakuta mfanyakazi mwenzako kasoma Sawa ana master ila kuandika kuomba hela za miradi Kwa ma donors wetu hawezi sijui niseme hana idea wakati kila kitu kipo Google ni yeye kusuka tu wazo la hela ya kawaida wazungu Wana hela kibao hakuna PA kuzipeleka ziko hewani.

Mtu kijana under 40 msomi wa level ya master unabaki kugombania hela za per diem za ndani nako ni pesa madafu tu nini tofauti yako na uliowazidi shule?

Wewe ulipaswa uwe unaandika lipitishwe bora likataliwe ila upewe sababu utarekebishwa andika andika andika tena lazima ipo siku litatiki uka coordinate Michongo. Hela za mabadiliko ya tabia ya nchi zipo kama zote mamifuko yanatoa.

Mavyeti kibao unabaki kutumia Google ku watch nonsense everyday.
Ndugu uandishi wa miradi (Project Proposals) ni TAALUMA, sio kila mtu anaweza kujiandikia tu.
 
Huku kwenye ofisi za umma ni kula pesa za bure tu, japo ni kidogo ila hazina kujitesa.
Yaani unataka kunishawishi kwamba mpaka mtu kachukua master hawezi kupata connection hizo za watalaam wakamshauri pa kupita. Hata kama ni kutoa pesa ili uandikiwe kazi hiyo
 
Yaani unataka kunishawishi kwamba mpaka mtu kachukua master hawezi kupata connection hizo za watalaam wakamshauri pa kupita
Wafadhili hapa duniani wapo MAMILIONI katika nyanja tofauti tofauti kama vile elimu, afya, maji, shughuli za kiuchumi na maendeleo, mazingira, mabadiliko ya tabia nchi n.k.
Lakini ukweli unabakia palepale, UANDISHI WA MIRADI NI TAALUMA kama zilivyo taaluma nyingine...
 
Mkuu ni kweli hali ya uwezo wa baadhi ya watumishi wa Umma inasikitisha na kukatisha tamaa.

Ingawa siungi mkono google search, Tafsiri ya ulichoandika ni kuwa weledi wa watumishi wa Umma upo chini.
Nakubaliana nawe, kuna viashiria vingi vinavyoonyesha kuwa baadhi ya watumishi wa umma hawana weledi stahili kwenye utendaji, uongozi na nafasi za kisiasa. Udhaifu unaonekana katika maamuzi, ubunifu, na utekelezaji wa sera.

Zamani ilikuwa vigumu kwa mtu anayefanya kazi kufaulu na kupata shahada au stashaha. wengi walikuwa wana discontinue au wanafaulu kwa tabu sana kutokana na utu uzima au uwezo wao kuwa mdogo. Lakini kwa sasa ni rahisi zaidi kwa watumishi kufaulu vyuo vikuu kuliko watoto wanaotoka A'level directly. Hii inatokana na ukweli kuwa sasa kuna njia mbadala nyingi za kufaulu vyuoni kuliko jitihada na uwezo wa mwanafunzi. Ukiwa na ushawishi, ni rahisi kupata B, M hadi PhD wewe tu na mbinu zako. Hivyo undeperomance kwa graduate wa sasa siyo kitu cha kushangaza.

Katika Ofisi fulani kuna mtaalamu ana MBA na CPA lakini anakodi watu wamwandikie riport na majibu ya CAG. Kuna mtu ni wakili aliyesajiriwa lakini hawezi draft mkataba. Kuna mtu ni Katibo Mkuuu lakini hawezi kutafsiri ripoti ya andiko la mradi. Unakuta watu wamevaa suti zimewakaa wanakula uapisho, unajua yes sasa taasisi itafufuka, akifika ofisini utatamani aliyetumbuliwa arudishwe!

Yaani huwa inashangaza kumkuta Katibo mkuuu, wakurugenzi na wasomi wanapambana ili kupiga pesa za posho za safari au ku overestamate bajeti kwa dhumuni ya kuiibia serikali. Watu kama utani wanakutana baa kujadili namna ya kuandaa dokezo la kupiga pesa, na kweli mchongo unafanikiwa, lakini haohao hawawezi kuandaa dokezo la maana la mradi. Mbaya zaidi, ikitokea kuna mtu ana upeo mkubwa na uwezo wa kutoa solutions za changamoto, atachukiwa na kupigwa vita kuanzia waziri, katibu, mkuu wa taasisi na benefiries wa udhaifu, mwishowe utengenezewa zengwe ili aonekane hajui kitu. watu wanapenda ku maintain status Quo ili waendele kupiga fedha za umma.

Ili kuishi katika mazingira ya sasa baadhi ya wasomi wameamua kujifyatua tu ili mambo yaende na wattoto wapate mlo.

Mungu atusaidie
 
Wakenya na Waganda wametuzidi katika kubuni na kuandika miradi, tukae nao watufundishe.
wakenya elimu yao ipo juu by far kulinganisha na sisi. Ni vigumu kwa mtanzania kushindana na mkenya kiweledi ndio maana kwenye ajira za kimataifa wanatuacha. sisi level zetu ni Malawi, Comoro, Msumbiji, Burundi na somalia
 
Wafadhili hapa duniani wapo MAMILIONI katika nyanja tofauti tofauti kama vile elimu, afya, maji, shughuli za kiuchumi na maendeleo, mazingira, mabadiliko ya tabia nchi n.k.
Lakini ukweli unabakia palepale, UANDISHI WA MIRADI NI TAALUMA kama zilivyo taaluma nyingine...
Mkuu nilipitia uzi wenu ule wa miradi mlikuwa mnabishana sana nikasoma kimyakimya kila hoja. Sikuchangia sababu sijui kitu uko. Sasa huwa najiuliza hivi ni lazima muandishi ajue lugha vizuri sana bila chenga kuandika na kuzungumza, na ni lazima afanye presentation uso kwa uso.
 
Uandishi wa miradi unakwenda zaidi ya kujua lugha mkuu. Ni uwezo wa mtu kutunga, kubuni na kuyaweka mawazo yake katika hali ya utaalamu yaani mtiririko. Lazima uwe na kichwa kizuri, exposure ya nyanja husika na uzoefu na utaalamu.
Chukua hii: watu wengi huandika miradi haipimiki (No performance indicators) na haitekelezeki (Difficult to implement).

Hii ni taaluma na ni kipawa pia, maana kuweka mawazo yako kwenye maandishi ya kitaalam sio jambo dogo.
 
Naona watu wanadanganyana humu, kwamba masters na PHD si kitu.

Mna judge masters na phd kwa sababu ya watu baadhi mliowaona, kuna watu wanazitendea haki masters na phd.

Kingine si kila jambo la kisomi msomi anaweza fanya. Kuandika miradi ni jambo la kawaida tu mtu anaweza kuingia YouTube akasoma akaelewa akaandika.
Kuna kusahau, hata engineers kuna nyakati huwa baadhi ya project inabidi ku review mambo fulani, hata doctors kuna muda wanarudi kusoma vitabu kujikumbusha zaidi.
Programmers n.k, kuwa msomi haimaanishi we ni roboti la tesla lenye AI kwamba utajua kila jambo, unaweza shangaa hata swali la secondary ukakosa lakini haimaanishi ni ujinga.

Acheni wivu usio na maana, mnakaa vijiweni mkidanganyana elimu level ya masters haina msaada, bongo kazi kweli kweli.
 
Inashangaza unakuta mfanyakazi mwenzako kasoma Sawa ana master ila kuandika kuomba hela za miradi Kwa ma donors wetu hawezi sijui niseme hana idea wakati kila kitu kipo Google ni yeye kusuka tu wazo la hela ya kawaida wazungu Wana hela kibao hakuna PA kuzipeleka ziko hewani.

Mtu kijana under 40 msomi wa level ya master unabaki kugombania hela za per diem za ndani nako ni pesa madafu tu nini tofauti yako na uliowazidi shule?

Wewe ulipaswa uwe unaandika lipitishwe bora likataliwe ila upewe sababu utarekebishwa andika andika andika tena lazima ipo siku litatiki uka coordinate Michongo. Hela za mabadiliko ya tabia ya nchi zipo kama zote mamifuko yanatoa.

Mavyeti kibao unabaki kutumia Google ku watch nonsense everyday.
Umeshaghushi miradi mingapi?
 
Mkuu nilipitia uzi wenu ule wa miradi mlikuwa mnabishana sana nikasoma kimyakimya kila hoja. Sikuchangia sababu sijui kitu uko. Sasa huwa najiuliza hivi ni lazima muandishi ajue lugha vizuri sana bila chenga kuandika na kuzungumza, na ni lazima afanye presentation uso kwa uso.
Muandishi wa mradi sio lazima ahusike kwenye hizo process nyingine kama kufanya presentation n.k, anaweza kuishia kwenye kuandika tu na msijuane tena baada ya hapo.
 
Mwaka 2016 nilibahatika kuhudhurua annual technical meeting ya NGO moja hv ambayo ilikuwa imefadhiliwa mradi wake na UNEP kuhusu mambo ya climate change, wale jamaa walikuwa wametengewa bilioni 100 kwa miaka mitatu. Ndani ya mwaka mmoja walikuwa wametumia 38 bilioni. Kwa ufupi mradi ulikuwa uwe wa serikali, ila naona ile NGO ndio ilikuwa inaishirikisha serikali coz fund zilipitia kwao. Jamaa walikuwa wanajiandalia tu study tour mara sijui Moroco sijui Indonesia na per diem za kufa mtu. Ukitumia akili hela za mabeberu zipo hazina matumizi.
 
Hahahaha upate ufadhili wa billion 100 sio mchezo unajua. Ni ishu nzito sana ila mpunga ukitoka ni kujipigia tu.
 
Back
Top Bottom