Mkuu ni kweli hali ya uwezo wa baadhi ya watumishi wa Umma inasikitisha na kukatisha tamaa.
Ingawa siungi mkono google search, Tafsiri ya ulichoandika ni kuwa weledi wa watumishi wa Umma upo chini.
Nakubaliana nawe, kuna viashiria vingi vinavyoonyesha kuwa baadhi ya watumishi wa umma hawana weledi stahili kwenye utendaji, uongozi na nafasi za kisiasa. Udhaifu unaonekana katika maamuzi, ubunifu, na utekelezaji wa sera.
Zamani ilikuwa vigumu kwa mtu anayefanya kazi kufaulu na kupata shahada au stashaha. wengi walikuwa wana discontinue au wanafaulu kwa tabu sana kutokana na utu uzima au uwezo wao kuwa mdogo. Lakini kwa sasa ni rahisi zaidi kwa watumishi kufaulu vyuo vikuu kuliko watoto wanaotoka A'level directly. Hii inatokana na ukweli kuwa sasa kuna njia mbadala nyingi za kufaulu vyuoni kuliko jitihada na uwezo wa mwanafunzi. Ukiwa na ushawishi, ni rahisi kupata B, M hadi PhD wewe tu na mbinu zako. Hivyo undeperomance kwa graduate wa sasa siyo kitu cha kushangaza.
Katika Ofisi fulani kuna mtaalamu ana MBA na CPA lakini anakodi watu wamwandikie riport na majibu ya CAG. Kuna mtu ni wakili aliyesajiriwa lakini hawezi draft mkataba. Kuna mtu ni Katibo Mkuuu lakini hawezi kutafsiri ripoti ya andiko la mradi. Unakuta watu wamevaa suti zimewakaa wanakula uapisho, unajua yes sasa taasisi itafufuka, akifika ofisini utatamani aliyetumbuliwa arudishwe!
Yaani huwa inashangaza kumkuta Katibo mkuuu, wakurugenzi na wasomi wanapambana ili kupiga pesa za posho za safari au ku overestamate bajeti kwa dhumuni ya kuiibia serikali. Watu kama utani wanakutana baa kujadili namna ya kuandaa dokezo la kupiga pesa, na kweli mchongo unafanikiwa, lakini haohao hawawezi kuandaa dokezo la maana la mradi. Mbaya zaidi, ikitokea kuna mtu ana upeo mkubwa na uwezo wa kutoa solutions za changamoto, atachukiwa na kupigwa vita kuanzia waziri, katibu, mkuu wa taasisi na benefiries wa udhaifu, mwishowe utengenezewa zengwe ili aonekane hajui kitu. watu wanapenda ku maintain status Quo ili waendele kupiga fedha za umma.
Ili kuishi katika mazingira ya sasa baadhi ya wasomi wameamua kujifyatua tu ili mambo yaende na wattoto wapate mlo.
Mungu atusaidie