Inakuaje mtu unajiua sababu ya mpenzi?

Inakuaje mtu unajiua sababu ya mpenzi?

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,047
Reaction score
1,832
Wadau habari zat weekend.Natumaini ni wazima.

Leo naomba kuwekwa sawa kuhusu jambo hili.siku hizi vijana wengi wamekuwa wakijiua sababu ya mapenzi.Je ni sababu ya kupenda sana au ni kufikiri kwamba huwezi kupata tena mpenzi kama yule.

Tujadiliane tupeane uzoefu.
 
Ni kufikiri kua hayupo mwingine kama yule, ,,,mahaba yake ukiyafikiria,ucheshi wake,,duuuu naweza jiua aiseeeee
 
Ni shetani anakuwa amewakalia kooni ni kuwafanya wajione hawana thamani tena ya kuishi kwa kitu walichotendewa. Na pia ni kutokukubali hali iliyokutokea na kubaki kujiuliza kwanini isiyo na jibu.
 
wadau habari zat weekend.
Natumaini ni wazima.
Leo naomba kuwekwa sawa kuhusu jambo hili.siku hizi vijana wengi wamekuwa wakijiua sababu ya mapenzi.Je ni sababu ya kupenda sana au ni kufikiri kwamba huwezi kupata tena mpenzi kama yule.
Hebu tujadiliane tupeane uzoefu.

Mungu aniepushie ibilis mchafu cwz kbs kujiuwa yaan nimuache anafaid mm nimetangulia hy haipo
 
Kuna dada mmoja alipata mpaka magonjwa mapya ambayo hakuwa nayo alipata ulcers,moyo ukawa mkubwa halafu akakonda vibaya mno.Huku kupenda kwingine mtu utakuja kufa kabla ya wakati wako aisee.
 
Kuna mambo ambayo wapendanao wa kweli, hushare ambayo yanamfanya mwanamume amuone mwanamke yupo unique, na mwanamke likewise. Mapenzi si ngono pekee, mapenzi kuwa Connected kupitia feelings zenu. Namaanisha kuwa feelings zenu ndiyo zinunganisha mioyo miwili yenye upendo. Kuna watu hawawezi kuhandle ukweli kuwa wametengana au kusalitiwa na watu waliowapenda toka ndani kabisa ya mioyo yao. Kutokana na kushindwa kuukubali ukweli huo, kifo kinakuwa ni option ya iliyobaki.
 
Kukataliwa kubaya jamani kusikie kwa mwenzio. Mapenzi yanapokolea hakuna alie shujaa. Wengi wetu kama sio wote hugeuka kuwa mazuzu. Usiombe kupenda na yule umpendae akawa kakuchoka.,
 
wadau habari zat weekend.
Natumaini ni wazima.
Leo naomba kuwekwa sawa kuhusu jambo hili.siku hizi vijana wengi wamekuwa wakijiua sababu ya mapenzi.Je ni sababu ya kupenda sana au ni kufikiri kwamba huwezi kupata tena mpenzi kama yule.
Hebu tujadiliane tupeane uzoefu.

sio kwa sikuiz
 
Mkuu kama umewahi kupenda na kupita salama eneo hilo mshukuru Mungu na waombee tu wale wanaopatwa na masahibu hayo. Kwanza kabisa hiyo issue ya kujiua ilikuwepo tangu zamani lbda tuseme taarifa zilikua hazisambai kama ilivyo sasa kwa sababu ya uchache wa vyombo vya habari kipindi hicho.

Refer kwenye usemi huu mapenzi ni upofu tafakari utapata jibu. Usiombee kuachwa na unaempenda kwa dhati isikie tu rafiki. Ni rahisi kuwadharau au kuwadhihaki wanaojiua au kuchanganyikiwa sababu ya kuachwa iwapo tu hujawahi kupenda kweli kweli.
 
Ni shetani anakuwa amewakalia kooni ni kuwafanya wajione hawana thamani tena ya kuishi kwa kitu walichotendewa. Na pia ni kutokukubali hali iliyokutokea na kubaki kujiuliza kwanini isiyo na jibu.

Kheri Ya Mwaka Mpya!
 
Unadhani Mtu Anayejiua Anakuwa Anajua Kila Anachokifanya,ukweli Ni Kwamba Pale Anakuwa Amerukwa Na Akili Ndo Maana Anaamua Kufanya Maamuzi Magumu Pasipokujitambua Usifikirie Kuwa Wanaojiua Huwa Wanajitambua Jua Kuwa Hata Wewe Unaweza Ukajiua Subiria Siku Uvurugwe Na Akili
 
wadau habari zat weekend.
Natumaini ni wazima.
Leo naomba kuwekwa sawa kuhusu jambo hili.siku hizi vijana wengi wamekuwa wakijiua sababu ya mapenzi.Je ni sababu ya kupenda sana au ni kufikiri kwamba huwezi kupata tena mpenzi kama yule.
Hebu tujadiliane tupeane uzoefu.

Omba tu yasikukute, na hili jambo halina mzee wala kijana, halina umri kwa ufupi
 
Umefika Kanisani Na Shela Lako Halafu Mie Sijatokea Kwann Dunia Usiione Chungu MankaM

Kuiona dunia chungu ndio nijiue??? labda cha kufanya hapo ni kukutafuta popote pale ulipo nikuue wewe / nakupotezea
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom