Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

Hiyo katiba iliwekwa na wanachama wa chama gani ili kumfeva Mbowe?
 
Ebu tuwekee hapa kifungu cha katiba ya Chadema unayosema imevunjwa na Mbowe ili kuhalalisha mantiki ya hoja yako
Rejea katiba ya mwaka 2004, iliyochakachuliwa kinyemela 2006 na kuondoa ukomo utawala.
 
Basi tusilalamike siku ccm wakipeleka hoja bungeni kuwa Magufuli atawale bila ukomo.
Until then,kwasasa msilopokelopoke kuwa katiba inavunjwa!
Hivi baba wa taifa alikuwa Mwenyekiti TANU na baadae CCM kwa miaka mingapi vile????
 
Hapa hata sijakuelewa!Na ambao hawana vyama waathirike na uminywaji demokrasia kisa tu CDM na CCM havina demokrasia?
 
Wanaona tu upande mmoja ila wao hawataki kabisa kukosolewa ama kusahihishwa kwa makosa yaleyale wanayoyapigia kelele.!
 
wengine hapa siyo wana Chadema wala CCM ila tunafuatilia kwa karibu haya yanayoendelea.

miaka yote hii nimekuwa nikiaminishwa kuwa Chadema wanao utaratibu wa kimchakato wa kuchagua viongozi wao wa juu.
kwa kauli yako hii inaonyesha kuwa kumbe si kweli. inaonekana kama mtu akiutaka say uenyekiti anasema "mimi mwenyekiti" halafu anakuwa mwenyekiti, nk.

yaani hapa unatupa picha kuwa akina Mbowe, Safari, Mnyika, Mdee, nk huwa wanajiwekaga wenyewe kwenye hivyo vyeo walivyo navyo chamani. ama?

embu tutoe tongotongo kidogo mkuu.
 
haa haa mkuu taratibu hizo ndani ya chadema zinasema mgombea wa nafasi ya uenyekiti taifa atakuwa mmoja tu? je demokrasia wanayodai chadema muda wote ni ipi? hivi mwanachama kutoa mtazamo tofauti dhidi ya mbowe kwenye chama ni usaliti?ilitakiwa tuone watu zaidi ya mmoja wanachukua fomu kugombea uongozi ndani ya chama kisha kura zipigwe. atakayekuwa na kura nyingi ndo mshindi. hizi tabia za kiccm hapana mgombea mmoja tu kupigiwa kura za hapana na ndio huyohuyo hazitaijenga chadema
 
Uliowataja wanafika bei hata kwa nguo ya ndani wanaachia madaraka
 
Mmmh mkuu naona hapa tumepisha uelewa tu, hapa nadhani hukunielewa vizuri, Chadema katiba yao iko bayana kabisa kuwa kila mwanachama ana haki na sifa ya kugombea nafasi ya uenyekiti, kinachokuwa kinagomba ni njia ipi unaitumia kufanya harakati za kugombea nafasi hiyo, ndio maana nikasema kila jambo liko na kanuni zake, hakuna jambo lolote lisilo na utaratibu wake
 
Hapa hata sijakuelewa!Na ambao hawana vyama waathirike na uminywaji demokrasia kisa tu CDM na CCM havina demokrasia?
Lazima waathirike maana maamuzi makubwa kuhusu nchi yetu yanaamuliwa na wanasiasa....CCM ni Chama cha siasa kilichounda serikali...au hukusikia juzi Magufuli anasema hataki kusikia mtumishi anasema yeye hana chama.

Sasa wewe amabae huna chama utashindwa vipi kuathirika na maamuzi ya watumishi/makada
 
Kwasababu mbowe kaimarisha chadema, wamejaribu kila njia kumrubuni ili waiue chadema wakashindwa, walimrununi Silaa, wakamrubuni Lipumba, wakamrubuni yule mama wa act wazalendo, Ila kwa mbowe wanagota, kwaiyo ndo wanataka aondoke ili wamlete wa kwao watakae mpeleka watakavyo.

Mwenye akili tu ndo atalitambua hilo, haswa akijiuliza toka lini ccm ilitakie mema chadema?
 
Siyo CCM tu hata Mungu anataka hivyo kwa sababu muda wake umekwisha na anapaswa kupisha wengine kama yeye walivyompisha pia, vinginevyo afute neno ,,demokrasia” kwenye chadema.
Wewe Shetani acha kumtaja MUNGU kwenye huu upuuzi wako, shetani mkubwa weee
 
Hili jambo la kutaka Mh.Mbowe aachie madaraka limekuwa likishinikizwa na wanaccm pekee na sio wana CHADEMA kama ilivyo tarajiwa .
Ccm yao imewashinda wanataka kuharibu upande wa pili .
Ila kwavile CHADEMA wanajitambua hawatafuata akili za Lumumba.

Over
 
Hujaelewa,kinachotokea ni kuwa mnasema CDM haina demokrasia ndio maana na CCM inalipiza kwa kutokuwa na demokrasia!
Inamaana CDM isingekuwepo,hiyo demokrasia ingekuwepo CCM????
Na ambao hawana vyama?
 
Mkuu tujuze utaratibu kwa mwanachadema yeyote anaetaka kugombea Uenyekiti taratibu zikoje....

Tuone kama Wenje, Zito na sasa Kubenea na Kom hawaujui ila Mbowe tu.
 
Kwanini chadema huwa wanataka raisi ajiuzulu
Wakati yeye ni wa ccm

Jibu la hili swali ndio jibu la swali lako
 
Nafasi pekee yenye utata ni Uenyekiti....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…