Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

Inakuwaje CCM ndiyo wanauchoka uenyekiti wa Mbowe?

[emoji1] [emoji1]
Waambie hawa mbulula! Mbowe pamoja na uimara wake mkuu bado ni mnyenyekevu hata anapoonewa. Kiasi Fulani ndani ya Chadema wanamuona kuwa pamoja na kuwa na msimamo usioyumba lakini dini imemkaa sana hivyo mambo ya mbwai na iwe mbwai kwake hayataki vinginevyo pengine CCM ingekuwa out.
Hivi wanamjua yule Mkurya Heche? waniambie nani ambaye toka Jiwe ameingia madarakani ameweza kuambiwa hadharani maneno aliyojibu Heche kule Tarime hadi akasema mnyang'anye mic? Haki ya nani Heche akiingia madarakani CCM watamtafuta Mbowe wamlambe makalio arudi.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] Hizi akili utazikuta chadema pekee!

Nyumbu mnataabu sana.
 
Mkuu tujuze utaratibu kwa mwanachadema yeyote anaetaka kugombea Uenyekiti taratibu zikoje....

Tuone kama Wenje, Zito na sasa Kubenea na Kom hawaujui ila Mbowe tu.
Kuhusu Wenje siwezi kumzungumzia maana hajawahi kuwa na mgogoro na chama kiasi cha kufikia kamati kuu kumjadili mwenendo wake ndani ya chama

Kuhusu hao Zitto, Kubenea na Komu katiba na kanuni zote za chama wanazijua sana ila kimachofanya waamue kwa makusudi kuzikiuka ni ulafi wa madaraka na uchu wa maslahi binafsi

Waraka wa akina mm1, mm2 na mm3 kwa maana Mwigamba, Kitila Mkumbo na Waitara ulionesha kwa kiasi walivyokuwa watovu wa nidhamu kwa uwajibikaji wa pamoja kama viongozi wakuu wa chama

Hawa Komu na Kubenea siwezi kusema maana sijawa na uhakika na ile clip inayosambaa mitandaoni kama ya kweli, kama itakuwa ya kweli nao watakuwa wameamua kuwa waasi ndani ya chama kwa maslahi yao binafsi badala ya maslahi mapana ya chama
 
Kuachia uenyekiti wa chama rais wa nchi ni kwa maslahi mapana ya nchi na siyo ya ccm maana kufanya hivyo ni kuondoa mgongano wa kimaslahi kati ya serikali na chama tawala

Mbowe hana mamlaka yoyote ya kufanya marekebisho ya katiba ya chama, wenye uwezo huo ni wanachadema wenyewe
Si chadema wanataka aachie umwenyekiti wa chama kwa kigezo cha kusema anakofia mbili wanasahau kuona kama mbowe ameondoa kipengele cha ukomo wa uongozi wake
 
Ukiona hivyo ujue wamemshindwa na wameshindwa pia kumnunua.
Ameamua kumkataa 'shetani na';
mambo yake yote
na visa vyake vyote
na gilba zake zote
na uongo wake wote.
Hongera sana Comred Mbowe, bado kitambo kdg 'shetani' utamshinda kabisa.
 
Kwasababu mbowe kaimarisha chadema, wamejaribu kila njia kumrubuni ili waiue chadema wakashindwa, walimrununi Silaa, wakamrubuni Lipumba, wakamrubuni yule mama wa act wazalendo, Ila kwa mbowe wanagota, kwaiyo ndo wanataka aondoke ili wamlete wa kwao watakae mpeleka watakavyo.

Mwenye akili tu ndo atalitambua hilo, haswa akijiuliza toka lini ccm ilitakie mema chadema?
Kweli kabisa mkuu.. Afu cha kushangaza, mrema wa tlp, cheyo wa udp, lipumb (cuf) wana miaka kibao kama wenyeviti lkn huwezi sikia wanasema maana wanaitumikia sisiemu.

Dhambi ya Mbowe ni kukataa kununuliwa..

Na kwa mazingira ya sasa ni vigumu kupata mtu asiye nunulika na hawa mafisadi
 
Siyo CCM tu hata Mungu anataka hivyo kwa sababu muda wake umekwisha na anapaswa kupisha wengine kama yeye walivyompisha pia, vinginevyo afute neno ,,demokrasia” kwenye chadema.
Mleta mada ameuliza swali la msingi kwamba TANGU LINI CCM IKAITAKIA MEMA CHADEMA jielekeze kwenye kujibu hilo swali...
 
Kuachia uenyekiti wa chama rais wa nchi ni kwa maslahi mapana ya nchi na siyo ya ccm maana kufanya hivyo ni kuondoa mgongano wa kimaslahi kati ya serikali na chama tawala

Mbowe hana mamlaka yoyote ya kufanya marekebisho ya katiba ya chama, wenye uwezo huo ni wanachadema wenyewe
Mkuu tumejifunika USO tukihisi hatuonekani hivi ulisha wahi kujiuliza kwanini mbowe kama mwenyekiti alijitahidi kuondoa ukomo wa uongozi ndani ya chama

Tukijipa muda wa kufikiria sana kuna vitu unajiuliza mbowe ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kwani hizo ni kofia ngapi?
 
Bavicha mko kwa ajili ya Mbowe na siyo kwa ajili ya chama cha chadema.

Mko tayari chadema ife kabisa ila mbowe abaki salama.!!
Hapao ndipo usomi wenu unakuwa wa hovyo na wa kutia mashaka.

Pauline Gekul, Mwita waitara , Katambi, Zito Kabwe , Kitila Mkumbo ,Chacha Wangwe wote wamefukuzwa Chadema na kupata matatizo kwa kutaka Mbowe aondoke madarakani walikuwa ni ccm?
Ni ccm yupi anayetaka mbowe aondoke madarakani?

Bavichaa mmebuni mbinu ya kumlinda Mbowe kwa kujificha kwenye kivuli cha ccm??
Bado vibaraka wenu komu na kubenea nao wanawafuata hukohuko kuunga juhudi za mwenyekiti
 
Mkuu tumejifunika USO tukihisi hatuonekani hivi ulisha wahi kujiuliza kwanini mbowe kama mwenyekiti alijitahidi kuondoa ukomo wa uongozi ndani ya chama

Tukijipa muda wa kufikiria sana kuna vitu unajiuliza mbowe ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kwani hizo ni kofia ngapi?
Mbowe hana mamlaka yoyote ya kuifanyia marekebisho katiba ya Chadema, wenye mamlaka hayo ni Chadema wenyewe
 
Habari zenu wana jamvi. Mara nyingi nimefuatilia threads zinazomshinikiza Mbowe aachie ngazi. Tena hoja zinazotolewa ni za kitoto tu. Halafu nikifuatilia watoa threads naona ni wa mlengo wa kulia. Swali langu ni je, kama kweli kuachia ngazi kwa Mbowe kutakuwa na faida kwa CDM ni kwanini shinikizo litoke without na sio within? Tangu lini CCM ikaitakia mema CDM? najiuliza tu.
Komu na kubenea ni within au ni without?
 
wengine hapa siyo wana Chadema wala CCM ila tunafuatilia kwa karibu haya yanayoendelea.

miaka yote hii nimekuwa nikiaminishwa kuwa Chadema wanao utaratibu wa kimchakato wa kuchagua viongozi wao wa juu.
kwa kauli yako hii inaonyesha kuwa kumbe si kweli. inaonekana kama mtu akiutaka say uenyekiti anasema "mimi mwenyekiti" halafu anakuwa mwenyekiti, nk.

yaani hapa unatupa picha kuwa akina Mbowe, Safari, Mnyika, Mdee, nk huwa wanajiwekaga wenyewe kwenye hivyo vyeo walivyo navyo chamani. ama?

embu tutoe tongotongo kidogo mkuu.

huwa wanajiwekaga na wanatafuta watu wachache ku justify

museven Uganda anafanya hivyo hivyo

ifike wakati hawa tunaowapenda sana tuwakosoe ni kwa faida ya taifa

CDM ikifa leo sio afya kwa taifa
 
Siyo CCM tu hata Mungu anataka hivyo kwa sababu muda wake umekwisha na anapaswa kupisha wengine kama yeye walivyompisha pia, vinginevyo afute neno ,,demokrasia” kwenye chadema.
Bado mbowe kama mwl nyerere atakuwa MKT kwa miaka 25 mpaka CDM ichukue Dola
 
Habari zenu wana jamvi. Mara nyingi nimefuatilia threads zinazomshinikiza Mbowe aachie ngazi. Tena hoja zinazotolewa ni za kitoto tu. Halafu nikifuatilia watoa threads naona ni wa mlengo wa kulia. Swali langu ni je, kama kweli kuachia ngazi kwa Mbowe kutakuwa na faida kwa CDM ni kwanini shinikizo litoke without na sio within? Tangu lini CCM ikaitakia mema CDM? najiuliza tu.
Hivi cheyo ana wadhifa gani na wa tangu lini pale udp?
 
Back
Top Bottom