Uchaguzi wa ndani wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ni jambo linalofuatiliwa kwa ukaribu sana, na makada wa CCM, ndani na nje ya serikali, jambo ambalo wana CHADEMA wamekuwa kama hawaelewei elewi kwa nini hili jambo ni muhimu kwa wana CCM.
Wapo wana CHADEMA wanaodhani kuwa CCM wanafuatilia huu uchaguzi kwa kuwa wanataka Mbowe atoke madarakani, kwa kuwa et Mbowe amefanikiwa sana kukijenga chama kwa miaka 20 aliyokuwa mwenyekiti, bila kuyumbishwa na CCM, hivyo CCM wanataka wapandikize mtu ambae watamcontrol kwa urahisi.
Binafsi, naona hilo si kweli, Kwanza, si kweli kuwa Mbowe ni tishio kwa CCM, Mbowe kama Mbowe hajawai kuwa tishio kihivyo kwa CCM, ni Wazi kuwa mtu kama Dr Slaa, au mtu kama Lissu, japokuwa hawajawhi kushika nafasi za uwenyekiti, ila kwa nafasi zao, walikuwa tishio zaidi kwa CCM kuliko Mbowe.
Hizi ndo sababu nazoziona kwa nini CCM wanafuatilia uchaguzi huu kwa Umakini:-
- Uchaguzi wa CHADEMA, Utaondoa ile dhana ya kuwa CHADEMA ni chama cha kikanda,cha wachagga, cha asasi ya kifamilia:- CCM wamekuwa wakiitumia hili jiwe siku nyingi kuipondea chadema, na kuna utani mahali kuwa, kirefu cha chadema, ni "Chagga Development Manifesto" wana CCM huambiana hivi, na kuhamasishana umuhimu wa kujituma katika ajenda zao za kukizua chama hiki chenye mlengo wa kikanda na kikabila kushika hatamu.
Sasa imefika mahali, endapo uchaguzi wa huru haki utafanyika CHADEMA, na Akatokea mwenyekiti ambae, sio Mkaskazini, sio mchagga, sio mkwe wa Mzee Mtei, Ndesamburo wala sio mtu wa inner cycle ya founders, basi CCM itapoteza kete muhimu sana ambayo imekuwa ikiitumia kuipondea CHADEMA
Ukanda na CHAGALISM imekuwa jiwe la kuipondea CHADEMA, ambalo kwa bahati mbaya limefanya kazi vizuri sana kwa miaka yote hii, kama ambavyo Udini/UISLAAM ulifanya kazi kwa CUF Had kikapotea kabisa. Na namna pekee ya CHADEMA kuepukana na jiwe hili, ilikuwa ni kupitia mwenyekiti anae mrithi Mbowe, ambaye ni mkwe wa muasisi wa Chama.
CCM wanajua hilo, na wanafuatilia kwa umakini sana kuona kama risasi yao ya siku zote itaendelea kutumika au lah!.
- Magufuli for 2030 Ajenda: Kikubwa kingine kinachofanya uchaguzi wa CHADEMA hasa wa mwenyekiti ufuatiliwe kwa ukaribu na wakereketwa wa CCM , na hasa Nisema wakereketwa wa Magufuli, hasa wale wanaotaka mzee baba, atoboe had 2030 ikibidi na zaidi.
Ni kwa sababu, wana aamini kuwa, Wakiwapump CHADEMA, Chadema watajaa kwenye 18 zao, wakati huu wakati CHADEMA wanataka kuhalalisha kuwa na mwenyekiti mmoja kwa miaka 20 na bado wanataka miaka mingine,wakati ambao wanataka kuuthibitishia Umma wa Watanzania na dunia nzima kuwa,
"Akipatikana kiongozi bora, ni heri akae madarakani muda wote, hadi pale atakapopatikana wa kumtosha". Huo ujumbe unaotolewa na CHADEMA, ana wafuasi wa Mbowe, unatoa point nzuri sana kwa wakereketwa wa Rais Magufuli.
Na endapo kweli kama tutaenda kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 na Mbowe angali akiwa mwenyekiti wa CHADEMA, Basi amini nakuambia, kile kikundi cha watu ndani ya CCM na ndani ya Serikali ambao wanatamani kumuona Rais Magufuli akiongoza hadi achoke, watakuwa wamepata vitu viwili muhimu:
1. Watakuwa wamepata sababu rahsi na mifano ya kuhalalisha ajenda yao
2. Watakuwa wamepata precedence case, ya kutumika kufafanulia ajenda yao.
Wakereketwa wa CCM na Rais Magufuli wanajua kila linalosemwa kipindi hiki na viongozi wa CHADEMA, ni muhimu sana, kwani litatumika hapo usoni kuipush ajenda hii, Nasikitika kuwa, CHADEMA hawajui hilo, na wanadhani wao kubaki na Mwenyekiti Mbowe, ni muhimu sana.
Ni wakati sasa CHADEMA, ijipambanue, ikubali kuwa Mwenyekiti kakitumikia chama kwa muda, na sasa apishe wengine. Ni wakati wa kuonyesha kwa mifano ukuaji wa Demokrasia ndani ya chama chetu, ni wakati wa kuonyesha kwa vitendo kuwa tunapinga utaratibu wa viongozi wa kiafrika kujiongezea muda madarakani