Inakuwaje kwa madaktari tuliowasomesha lakini wamekimbilia bungeni kufuata maslahi mazuri!

tindo alimuandikia mtu comment hivi, “mmeshasema elimu ni bure, kwanini usirudi shule ukajifunze kuandika”? 😀😀😀
 

Ndege za ATCL ni za serikali, je kila mtanzania mpaka wa hali ya chini anapanda kwakuwa ni za umma? Hapo ndio utajua haujui.
 

..Waanze na Dr.Hussein Mwinyi.
 

..Madaktari wamesoma kwa mkopo, ni makosa kusema serikali "imewalipia" masomo.

..serikali inaweza kusamehe mkopo kwa madaktari watakaokubali kutumikia ktk hospitali za serikali kwa kipindi fulani.
 
Hivi huyu si ndio aliropoka kipindi fulani kuwa mwajiriwa wa serikali asiyeridhika na mshahara anaolipwa basi aache kazi aende atakakolipwa mshahara wa kumridhisa?

..Na kuna kipindi Jpm alitaka kupeleka Madaktari wa Tanzania wakafanye kazi Kenya.

..alisema Tanzania inataka kuipa serikali ya Kenya msaada kukabiliana na mgomo wa madaktari waliokuwa wakidai waongezewe mishahara.
 
Bwashee kuna siku nyingine unakuwa na akili nyingi kama Tundu Lissu vile, halafu kuna siku ukiamka vibaya, huwa unakuwa kama Goodluck Mlinga!!

Hongera kwa hoja yako! Hakika maendelwo hayana chama. Leo kidogo nimekuelewa.
My God....yuko wapo huyo Bw Goodlucky Mlinga..???
 

Kukata mzizi wa fitina kazi zote za siasa ziwe na mishahara na marupurupu madogo kuliko za taaluma.

Waheshimiwa wote wa siasa hawa kodi stahiki ziwahusu kama mtu mwingine yeyote tu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Yuko sahihi kabisa.

Sisi tulipomaliza chuo ilikuwa ni lazima kuitumikia serikali kwa miaka 5 kabla hujaenda sekta binafsi au haujajiajiri!
Hii sera ilikuwa sahihi kwa maana ajira zilikuwepo nyingi serikalini.

Hivyo ilikuwa ni budi kujaza nafasi huko kwanza.

Leo soko huria,unaajiriwa hapa,kesho upo kule.

Maana ajira zimekuwa ni mapambano tu.

Huyu magu si alishapiga mkwara ataweza fukuza wote na kuajiri wengine.
 
Yuko sahihi kabisa.

Sisi tulipomaliza chuo ilikuwa ni lazima kuitumikia serikali kwa miaka 5 kabla hujaenda sekta binafsi au haujajiajiri!
Acha kupotosha, usidhan udaktar umesoma pekee yako. Sheria inasema ukimaliza masomo huruhusiwi kufanya kaz inje ya nchi mpaka uitumikie nchi yako kwa mda wa miaka 5. Na haijasemaHlazma ufanye kaz serikalin au private ila tu nchini. Hii sheria inatumika tu kwa madaktar waliopata grant/ ruzuku toka serikalin sio kwa madaktar waliosoma kwa kutumia mkopo.
 
Kwan huyo jamaa anatatibu wakenya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…