Inakuwaje mtu anafikia uamuzi wa kuishi Pugu Dampo na harufu mbaya kiasi kile?

Inakuwaje mtu anafikia uamuzi wa kuishi Pugu Dampo na harufu mbaya kiasi kile?

Habari!

Harufu mbaya inapiga maeneo ya Dampo la Pugu almaarufu kama Pugu Dampo.

Ukipita barabarani maeneo hayo unapokelewa na harufu mbaya kali sana.

Najiuliza hivi Kati ya Dampo na makazi ya watu nini kilitangulia?

Je, kama Dampo lilitangulia ilikuwaje mtu na akili zake timamu ajenge makazi maeneo yenye harufu mbaya kiasi kile?

Je, viwanja wananchi walipewa bure?

Au wananchi wamepewa fidia lakini wamegoma kuhama?

Siwezi kuafiki kuwa mtu timamu anaweza kuweka makazi ya kudumu maeneo ya jalalani.
Kama ukipita barabarani tu harufu ni kali je huko ndani wanaoishi jalalani kabisa!!
Kuna yule alisema ametolewa Jalalani na Jiwe, so jua kuwa watu wanaishi jalalani.
 
Mimi mwenyewe sielewi Kwa Nini watu wanafuata maeneo hayo.

Kuna siku mwaka 2014 nikapita kiwanda Cha ngozi Moshi (sio Cha Kilimanjaro Leather) siku hiyo walikuwa wanatoa maji ya kulowekea ngozi. Harufu yake ni balaa, Ila pembeni ya kiwanda watu wanaishi kama kawaida.

Iringa eneo la Donbosco-Mawelewele Kuna mabwawa ya maji taka. Maji ya chooni yanamwagwa huko na harufu yake unaipata ukiwa mbali.

Huwezi amini ndo kwanza wenye serikali Yao wanajenga hukohuko. Inaonekana "hatujali"
Hapo Pasua nimepita sana nikienda mpirani. Kwa kweli siwezi kuishi yale maeneo hata nilazimishwe kwa ngumi. Harufu inakupoke kilometer moja kabla hujakifikia kiwanda dah!
 
Kuna sehemu niliwahi kuenda Morogoro mjini miaka ya 2014, ile sehemu kulikua na kiwanda cha kuprocess Katani. Ile sehemu inanuka kinoma hata nusu kukaa ni hatari.
Hahahahah hii ni kihonda veta pale njia ya kwenda kilimanjaro kambi ya magereza pale na wafungwa ndio hufanya kazi ya kuchakata mkonge kuwa katani
 
Haa kumbe,mie wa mikoani nikadhani hapo wanaishi maskini
Maeneo yale kuna nyumba nzuri kupita hata nyumba yangu, utasemaje ni umaskini ndio huwafanya waishi pale?
Nyumba inasimama 50 milioni -70 milioni.
 
Karibu vingunguti machinjioni.
Aisee... Ile sehemu inanuka kinoma.. Sijui watu wanaishije pale... Watu wamekaa halafu hapo mlangoni panapita mfereji unatiririsha maji yenye damu... Na harufu juu.... Afu jamaa wanapiga na ubwabwa hapohapo......
 
Wewe ndio umenusa harufu ..wenzio wamezoea na hawasikii na wanaona kawaida tu na maisha ya kila siku yanaendelea...ukihamia maeneo hayo utasikia harufu siku za mwanzo ila after that utazoea...Kuna wakati zamani nilipita keko ule mto unabeba maji yenye harufu Kali kutoka kiwanda Cha Serengeti...yaani Mimi nilisikia harufu Kali Cha ajabu wakazi wake hatua mbili tatu wanapika na kula maisha yanaendelea ..yaani wameizoea na hasikii harufu yeyote...
 
Mimi mwenyewe sielewi Kwa Nini watu wanafuata maeneo hayo.

Kuna siku mwaka 2014 nikapita kiwanda Cha ngozi Moshi (sio Cha Kilimanjaro Leather) siku hiyo walikuwa wanatoa maji ya kulowekea ngozi. Harufu yake ni balaa, Ila pembeni ya kiwanda watu wanaishi kama kawaida.

Iringa eneo la Donbosco-Mawelewele Kuna mabwawa ya maji taka. Maji ya chooni yanamwagwa huko na harufu yake unaipata ukiwa mbali.

Huwezi amini ndo kwanza wenye serikali Yao wanajenga hukohuko. Inaonekana "hatujali"
Mimi hata kujenda karibu na barabara sitowwza, naitajigi utulivu ninapolala.

Sehemu ambayo napangaga ni nje ya mji kidg, au pale mabibo na buguruni.

Watu wapo, nyumba bati zote zina kutu.
 
Back
Top Bottom