Inakuwaje mtu anagoma kufa mpaka amuone mtu anayemhitaji kumuona?

Asalaam!
Rejea mada tajwa hapo juu. Kuna suala moja nimejihoji kwa muda mrefu lakini sijapata jawabu kutokana na visa vikuu viwili nilivyovishuhudia mwenyewe.

Mwaka 2013 mkoani Mbeya, Baba yetu mkubwa aliugua sana. Alizungushwa hospital nyingi sana pasipo mafanikio.
Mara ya mwisho ilikuwa MNH ambapo alishauriwa kurudi nyumbani ili walau ndugu wahangaike na tiba ya upande wa pili.
Mzee yule alikuwa akisema natamani kufa lakini kabla sijafa nataka kumuona mwanangu wa mwisho Asubhisye ambaye alikuwa Tanga. Ilibidi aitwe na aliporudi nyumbani Asubhisye aliongea nae na Mzee akachangamka kweli. Cha ajabu kesho yake alifariki.

Kisa cha pili nilikishuhudia kwa baba mwenye nyumba enzi nafanya kazi Geita mwishoni Mwa mwaka 2013. Mzee yule aliitwa Kachila alikuwa Muha wa Kasulu huko. Aliugua sana na matibabu yalishindikana.

Alikuwa kila Mara akisema naombeni muende Ukerewe mkaongee na Mke wangu amlete mtoto nimuone. Miaka mitatu nyuma alitengana na mkewe ambaye alikuwa mjamzito na tangu aondoke hakuwahi kurudi hata baada ya kujifungua.

Baada ya matakwa yake kutekelezwa naye alifariki baada ya siku moja.
Sasa najiuliza...je kuna mahusiano gani kati ya kukata roho na kumuona MTU unayemhitaji?

Kwa visa tajwa hapo juu, je nawe umewahi shuhudia au ni coincidence tu niliyokutana nayo?

Karibuni tueleweshane na kubadilishana uzoefu katika hili!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kule kwetu kuna dawa wazee waliwahi kunisimulia kuwa ipo mtu analukula ile dawa hata augue vipi hafi mpaka ampate mtu ambae anampa kwa kuitema na kumlisha ndipo anakufa nje ya hapo hafi ndo maana unakuta anamtaka fulan aje ndo kipenzi chake fuatilia maisha ya hao walioitwa na marehemu waliogoma kufa mpaka mtu fulan aje wanakuwa na umri mrefu sana wengine dawa anaiweka chin ya ardh anapanda mti wa mwembe akishakuwazee na anaumwa hafi mpaka amwite mtu maalum anaemtaka yeye ndo ampe siri then utasikia tuukate mti huu jaman mzee kaagiza yapo mengi ngoja leeo niishie hapa sisi wahenga tunagomaga kufa sio mtu unakufa kufa tu dunia tamu hii ipo pia ya kugoma kuzeeka hahaaaaaa njoon wanaume wa dsm na wadada niwauzie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila cha msingi ni kusubiri siku yako ya kukaribia kukutana na Ziraili mtoa roho,kwani hiyo haina mazoezi wa uzoefu.
 
Nilisoma kwenye Bible kuna mzee mmoja alikuwa anakaa hekaruni akisubiri Yesu azaliwe,
Alipomuona tu akamshika mkononi akasema "sasa Bwana waweza kumruhusu mtumishi wako aende kwa amani" This means IMANI HUTENDA

a307db6a189556dbf810cd4c4d62aaff.jpg

Private geologist
Simioni
 
Bibilia ni Msitu, unaeza Potea bure.

Msichanganye washirikina na wacha Mungu.

Huyo Simeon alishaambiwa na Mungu kua hatakufa mpaka amuone Mtoto Yesu.
Hao wengine wanaambiwa na nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Cc youngkato
 
In short hao wote walikua wame sell their souls to the devil.
Wanachofanya ni kuacha maagizo na Mikoba iendelee kwa kizazi kijacho walichokikabidhi kama kanuni inavyowataka kwenye ukoo na mila za matambiko.
Na Roho zao wanazikabidhi baada muda mfupi waliokaa hapa duniani wakitumikia.
Na kinachowatokea sio natural death/God's plan.

Reason:- Hakuna mwanadamu mwenye uwezo WA kuamua afaje.
Cc mshana jr

Sent using Jamii Forums mobile app
Kinachotokea ni mawasiliano ya kiroho katika mwili uharibikao
Ufahamu ndani ya mwili uharibikao una utashi wa kuamua mustakabali wake, lakini si kwa nafsi ina uwezo huo
mshana jr

*R.I.P my fellow classmate Nassoro Kipande*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawaza siku ikitokea Hio roho akimuita adui wa marehem ntajiwa na wakati anafika kwa kuchelewa maana aligoma akalazimishwa then mgonjwa akafa wakati yupo na adui ake ndani wanaongea wawili hio kesi ya mauaji sijui itamhusu nani
 
Kweli mwenyewe mama angu mzazi aliugua lakini kwa mda akawa anadai niende nilipofika siku mbili akafariki
 
Kule kwetu kuna dawa wazee waliwahi kunisimulia kuwa ipo mtu analukula ile dawa hata augue vipi hafi mpaka ampate mtu ambae anampa kwa kuitema na kumlisha ndipo anakufa nje ya hapo hafi ndo maana unakuta anamtaka fulan aje ndo kipenzi chake fuatilia maisha ya hao walioitwa na marehemu waliogoma kufa mpaka mtu fulan aje wanakuwa na umri mrefu sana wengine dawa anaiweka chin ya ardh anapanda mti wa mwembe akishakuwazee na anaumwa hafi mpaka amwite mtu maalum anaemtaka yeye ndo ampe siri then utasikia tuukate mti huu jaman mzee kaagiza yapo mengi ngoja leeo niishie hapa sisi wahenga tunagomaga kufa sio mtu unakufa kufa tu dunia tamu hii ipo pia ya kugoma kuzeeka hahaaaaaa njoon wanaume wa dsm na wadada niwauzie

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha...you made my day!
Wanaume wa Dar mpooooo?

Kwa Hisani Ya Watu Wa Mbeya!
 
Asalaam!
Rejea mada tajwa hapo juu. Kuna suala moja nimejihoji kwa muda mrefu lakini sijapata jawabu kutokana na visa vikuu viwili nilivyovishuhudia mwenyewe.

Mwaka 2013 mkoani Mbeya, Baba yetu mkubwa aliugua sana. Alizungushwa hospital nyingi sana pasipo mafanikio.
Mara ya mwisho ilikuwa MNH ambapo alishauriwa kurudi nyumbani ili walau ndugu wahangaike na tiba ya upande wa pili.
Mzee yule alikuwa akisema natamani kufa lakini kabla sijafa nataka kumuona mwanangu wa mwisho Asubhisye ambaye alikuwa Tanga. Ilibidi aitwe na aliporudi nyumbani Asubhisye aliongea nae na Mzee akachangamka kweli. Cha ajabu kesho yake alifariki.

Kisa cha pili nilikishuhudia kwa baba mwenye nyumba enzi nafanya kazi Geita mwishoni Mwa mwaka 2013. Mzee yule aliitwa Kachila alikuwa Muha wa Kasulu huko. Aliugua sana na matibabu yalishindikana.

Alikuwa kila Mara akisema naombeni muende Ukerewe mkaongee na Mke wangu amlete mtoto nimuone. Miaka mitatu nyuma alitengana na mkewe ambaye alikuwa mjamzito na tangu aondoke hakuwahi kurudi hata baada ya kujifungua.

Baada ya matakwa yake kutekelezwa naye alifariki baada ya siku moja.
Sasa najiuliza...je kuna mahusiano gani kati ya kukata roho na kumuona MTU unayemhitaji?

Kwa visa tajwa hapo juu, je nawe umewahi shuhudia au ni coincidence tu niliyokutana nayo?

Karibuni tueleweshane na kubadilishana uzoefu katika hili!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nilihadithiwa, ndugu aliyekufa akafufuka, kisa hajamalizia kutoa ahadi yake kanisani na walipo mlipia akafa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom