Ukimpenda mwanamke huwezi kukimbia
Hii kauli huwa sitaki kabisa kuisikia.... Kuna binti mmoja nilionesha dalili za kumchumbia (umri atakuwa kagonga 28,,, maana ukimtizama waona kabisa gazeti jioni)
Ila kidume nikataka nijiweke hvyohvyo sababu vigezo vyangu baadhi anavyo halafu pia nikaona huyu hatutosumbuana kutokana na ukomavu wake...
Bwana bwana eeeh.... Si nikaamua kuweka mambo hadharani, na yeye akaanza nyodo (mara ninamtu wangu tena anadai kadum nae miaka 7,,, kimoyomoy nikasema Ni haki yake maana wanawake ndvyo walivyo)
Lakini cha ajabu akaendelea na sitaki na nataka .... Week iloisha nikamwambia dhamira yangu halafu mwisho nikamwambia ila kwasasa sitaki tena,,, pia nikamshauri siku nyingine akija mtu na mpango wa kuleta posa usimgusie swala la kunamtu kakukongoroa miaka 7, mwanaume atakimbia maana ataona wewe Ni mke wa mtu tayari!!!
Baada ya hayo nikamwambia mimi nimeshindwa aendelee na huyo anayejipanga kutafuta maisha mkoa jirani kwa mwaka wa7 Sasa, ili akiyapata ndo aje kujitambulisha kwao!!!
Nikainuka huyooo safari.... Huwezi amini baada ya hapo nikafuta namba nikajisemea mabinti wapo wengi tena wabichi kwanini nihangaike na limama... Toka hiyo week haishi kupiga simu, sms hazikauki na mimi nimekaza na msimamo wangu (yeye kauli aliyoishikilia Ni kwamba,,, sikumpenda Kama ningekuwa nimependa ningevumilia yote...... Pia Mimi namjibu kwa sauti ya upole kabisa
Kwamba "Mwanaume huwa haendeshwi na hisia... Sio lazima nikupende ili nikuoe, ukiwa na vigezo vya kuitwa mke hiyo inatosha... Kuhusu kukupenda ntajifunza kukupenda mbele kwa mbele🚶🚶