Uchumba unaweza kuvunjika wakati wowote kwa sababu za msingi kabisa ambazo hata vitabu vya dini vinazisema.Issue ni kumuacha mtoto wa watu bila sababu,labda ni kwa tamaa za kuvutwa upande mwingine kwa kuvutiwa na mambo ya nje ukiamini yaliyomo yamo.Haki ya nani machozi ya huyo binti wa watu yanaweza kukufanya ukapuyanga humu duniani miaka yote bila kujua wapi unakwenda bila kurogwa kwa yeye kwenda kwa mganga.
Kuumiza watoto wa watu sio kitu kizuri kabisa.Hapa ni kwa pande zote lakini inapokuja kuhusu wanawake Mungu anawapa u-special fulani sijui anajua kwakuwa sisi wanaume tuna misuli?
Ngoja niwawekee hapa tuone namna wanachukuliwa tena wenye wake ndio kabisaaa.
Malaki 2:14-15
[14]Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu BWANA amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.
[15]Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.
1 Petro 3:7
[7]Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
Kama mambo fulani hayaendi inawezekana somewhere Mwaajuma Kikoti ulimliza na hajakusamehe mpaka leo,vipi yule Eliza 😀😀😀 bila kujua ku-clear hiyo hali yaweza kukuletea shida kubwa katika maishao na hii ni nje ya bibi yake,mama yake aliyejua mahusiano yenu na kujua maumivu ya binti wao kuamua kukushikia mkia wa kenge mwekundu 😀😀😀.
Kuna jamaa wanasema haiwezekani kurogwa halafu hawana Mungu wala hawana kinga yoyote wapowapo tu wakitest mitambo kesho unamkia nyumbani kwa binti ukiwa huna nguo.